Japo binafsi napenda kusisitiza watu kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yao, Lakini mambo kama haya ndiyo yanayovunja mioyo ya walipa kodi wengi. Je, hii ni sawa?
Mlipa kodi baada ya kulipa kodi anaenda kumwangalia mtoto wake shule njiani anapishana na Toyota GxR V8 ya mkurugenzi iliyonunuliwa kwa kodi yake, anafika shule anamkuta mtoto wake qkiandika kwenye majivu! Karne hii! Miaka zaidi ya 60 ya uhuru!
Akiuliza anaambiwa pesa ya kodi uliyotoa imeenda kununua gari la mkurugenzi!
Nani ametuloga watanzania?
Mtu mwenye akili timamu anathubutuje kunyanyua kinywa kupongeza mambo haya?
Gharama kubwa zinazotumika kwa mambo ambayo si kipaumbele wala si mambo yanayogusa wananchi wengi hususan wa hali ya chini, Zingekusanywa na kuelekezwa panapostahili hakika kila mwananchi angeonja utamu wa nchi yake!
Si katika huduma na bima za afya (ambayo siku za karibuni imefutwa)
Si katika ajira
Si katika miundombinu
Si katika Elimu n.k
Kama fedha hizi zingeelekezwa kwa wahitaji na walengwa walau kwa 60% hakika kila mmoja wetu angepata walau neema ya nchi yake!
Lakini fedha hizi zinatumima kwa ziara za hovyo zinazodai kufungua nchi, kwenda wapi? Kulipana mishahara na posho kubwa, kufanya kampeni, kusafirisha na kuhonga wasanii n.k
Je, ni sawa? ewe mtanzania unaona ni sawa?
Ewe mpiga kura unaona ni sawa?
Ewe chawa unaona ni sawa?
Ewe mlamba asali unaona ni sawa?
Mnazungumzia haki, hii ni haki?
Nini kimetupata watanzania mpaka kuyafumbia macho mambo haya?
Lino tutaamka na kuwawajibisha viongozi tunaowachagua?
Japo binafsi napenda kusisitiza watu kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yao, Lakini mambo kama haya ndiyo yanayovunja mioyo ya walipa kodi wengi. Je, hii ni sawa...
Imewezekanaje hao kuwapiga picha?Maana wasaidizi wa Samia hawapendi picha zinazowaonesha wanafunzi wakiwa wamekaa chini.wanapenda zile za kusifiwa tu.mfano yule mwandishi ambaye alipiga picha za wanafunzi huko ubungo kama sikosei alipigwa na walimu na kupelekwa ofisi ya kata na penyewe akapigwa na akapelekwa Kwa mkuu wa wilaya na kwenyewe akapigwa na kuvunjiwa simu yake na kuambiwa awe anatafuta habari za kumsifu mama tu basii.
Ni vizuri Serikali ikaangalia suala hili kwa umakini zaidi. Kuboresha miundombinu ya kusomea ni jambo muhimu sana kwa maendeleo ya vijana wetu kimasomo.
Japo binafsi napenda kusisitiza watu kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yao, Lakini mambo kama haya ndiyo yanayovunja mioyo ya walipa kodi wengi. Je, hii ni sawa...
Sijui kama kule Zanzibar nako pia kuna shule zenye changamoto kubwa kama hii! Ukifanya uchunguzi utakuta kuna shule nyingi sana hapa nchi ambazo pia zina hali mbaya kama hii.
Halafu utashangaa kusikia watu bado wakisifu mambo mazuri tu ya utawala wa CCM. Ni aibu sana kwa watawala wanaoishi maisha ya anasa kubwa kuwaongoza wananchi ambao wametopea katika lindi kubwa la ufukara na umaskini uliopindukia.
Japo binafsi napenda kusisitiza watu kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yao, Lakini mambo kama haya ndiyo yanayovunja mioyo ya walipa kodi wengi. Je, hii ni sawa...
Nchi ni kubwa sana uzuri serikali Kila kukicha imekua ikiimarisha huduma za kijamii..ukisema miradi ya kijamii inayitekelezwa na mama iwekwe hapa hakika sever za jf zitalipuka Kwa wingi na uzito wa miradi inayotekelezwa Kila uchwao
Nchi ni kubwa sana uzuri serikali Kila kukicha imekua ikiimarisha huduma za kijamii..ukisema miradi ya kijamii inayitekelezwa na mama iwekwe hapa hakika sever za jf zitalipuka Kwa wingi na uzito wa miradi inayotekelezwa Kila uchwao
Mijitu myeusi sijui tukoje. Unaiba mabilioni ya hela halafu kizazi kipya ambacho ndicho msingi wako wa kesho unakifanyia hivi. Mahospitalini nako watu wanakufa kwa kukosa dawa kisa tu wewe umeiba unaendesha Vogue na kujenga maghorofa. Na unajiona mjanja!
Hata tukitupiwa maganda ya ndizi naomba tusiwe tunalalamika. Something is terribly wrong with us. Kwa nini tuna huu ufisadi wa kihayani? Kwa nini tuko wabinafsi hivi? Nenda Haiti. Nenda Visiwa vya Caribbean. Afrika yote...mambo ni yale yale. Tuna shida gani sisi?