Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Japo binafsi napenda kusisitiza watu kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yao, Lakini mambo kama haya ndiyo yanayovunja mioyo ya walipa kodi wengi. Je, hii ni sawa?
Mlipa kodi baada ya kulipa kodi anaenda kumwangalia mtoto wake shule njiani anapishana na Toyota GxR V8 ya mkurugenzi iliyonunuliwa kwa kodi yake, anafika shule anamkuta mtoto wake qkiandika kwenye majivu! Karne hii! Miaka zaidi ya 60 ya uhuru!
Akiuliza anaambiwa pesa ya kodi uliyotoa imeenda kununua gari la mkurugenzi!
Nani ametuloga watanzania?
Mtu mwenye akili timamu anathubutuje kunyanyua kinywa kupongeza mambo haya?
Gharama kubwa zinazotumika kwa mambo ambayo si kipaumbele wala si mambo yanayogusa wananchi wengi hususan wa hali ya chini, Zingekusanywa na kuelekezwa panapostahili hakika kila mwananchi angeonja utamu wa nchi yake!
Si katika huduma na bima za afya (ambayo siku za karibuni imefutwa)
Si katika ajira
Si katika miundombinu
Si katika Elimu n.k
Kama fedha hizi zingeelekezwa kwa wahitaji na walengwa walau kwa 60% hakika kila mmoja wetu angepata walau neema ya nchi yake!
Lakini fedha hizi zinatumima kwa ziara za hovyo zinazodai kufungua nchi, kwenda wapi? Kulipana mishahara na posho kubwa, kufanya kampeni, kusafirisha na kuhonga wasanii n.k
Je, ni sawa? ewe mtanzania unaona ni sawa?
Ewe mpiga kura unaona ni sawa?
Ewe chawa unaona ni sawa?
Ewe mlamba asali unaona ni sawa?
Mnazungumzia haki, hii ni haki?
Nini kimetupata watanzania mpaka kuyafumbia macho mambo haya?
Lino tutaamka na kuwawajibisha viongozi tunaowachagua?
TAFAKARI. CHUKUA HATUA