Uchaguzi 2020 Mambo Kumi niliyoyasikia leo kwa mara ya kwanza kuhusu Tanzania kutoka kwa Tundu Lissu akiwa Mbarali

Hahaha sera ni nini?! Madaraja au kubambikia watu kesi?!

Hivi siku hizi hagawi pesa barabarani tena au zimeisha?!
Jiwe akili zake anazijua mwenyewe na kina Bashiru+ Poleslow! Kwanza juzi kwenye dk45 ITV Bashiru alipanic vibaya full jazba.
 
Ndio shida hiyo, wakati wengine tumeanza safari ya kuendea uchumi wa kati, wengine bado wana taswira ya usafiri wa Dar Mtwara siku nne😂😂
 
Unaposema sio sehemu ya maswali umetumia akili kufikiri au unaendeshwa na mihemko! Unakwenda kinyume na Bashiru, aliwaambia jibuni hoja (maswali) wewe unajitoa akili eti maswali bungeni grow up dude!!
 
Kageuza mkutano wa kampeni kijiwe Cha story badala ya kunadi sera
Toka mwanzo Hadi mwisho wa hizo point kumi Ni story tu hamna Cha sera Wala nini
Kwani maana na umhimu wa sera ni nini? Sera ni kurekebesha ubovu na kujenga mikakati ya kuenenda mbele kwa usahihi.
 
una maswali fikilishi[emoji3][emoji3]

Viva JPM
Kwa hiyo hayo mambo kumi aliyoongea ndio mnahitaji wanayohitaji watanzania akichaguliwa kuwa Raisi?

Na hizo ndizo sera za Chadema aalizowaambia Wana Mbarali?
Zote naona porojo tu hamna sera hata Moja Hapo kawapotezea muda tu watu wa mbalali
 
Hii ni hatari sana na inatoa mwanya wa ubadhilifu mkubwa kwanza ni ngumu kumwadhibu mtoto wa dada yako anapofanya kosa wanasema damu ni nzito kuliko maji, lakini pia ni ngumu mtoto wa dada kukunyima pesa hata kama ni za magumashi, na hii haikubaliki sehemu yeyote, je waliandika conflict of interest?
 
lazima hajibu inatoka wapi wakati tumesha muhalikishia ushindi wa 92%

Viva Magu
 
Chorus: Tumeibiwa kura
 
Baada ya Lisu kumaliza kueleza hayo mambo kumi ukimuuliza mwana mbalali sera za Chadema Ni Nini atajibu Nini hapo?
Atajibu Hivi; Jiwe sio wa kwanza kutamba na madaraja, SGR etc. Asitumie mgongo wa madaraja kuminya uhuru wa habari, kunyanyasa wanaokosoa utawala wake as if yeye ndo Mungu wa Tz. Mwambie aache kusujudiwa kama yeye ndo mtoa oxygen
 
kula 5 za nguvu[emoji3][emoji3]

Viva JPM
Tumeyasikia ila bado rais atakaechaguliwa na watanzania ni John Pombe Magufuli
Tukutane hapa kuanzia asubuhi ya October 29, tukiwa tunaendelea kupata matokeo ya uchaguzi
 
Kwa hiyo hayo mambo kumi aliyoongea ndio mnahitaji wanayohitaji watanzania akichaguliwa kuwa Raisi?

Na hizo ndizo sera za Chadema aalizowaambia Wana Mbarali?
Zote naona porojo tu hamna sera hata Moja Hapo kawapotezea muda tu watu wa mbalali
Tumeshafika 801 ,ongeza wazaz au walez wawiliwawili ,ongeza wadogo zetu ,ongeza wake zetu na madem wetu ,na wote walio guswa na ukosefu wa ajira kwa watoto wa wanyonge. Kwa upepo huu ccm ijiandae kuanza kutumia pension.
 
Ongezaaaa alisikika YEHODAYA, mkuu hawa wamevurugwa mbaya. Mara upinzani umekufa saa hizi wanasema tukutane 28/10/2020 nawacheka Sana asee
 
Lissu anastress nyingi sana ndo maana anaacha kunadi sera anatoa lawama mwanzo mwisho.
hayo mambo kumi angefafanua yeye angefanya yepi mazuri kuzidi hayo na nijinsi gani atakavyo yafanya pindi kama akipewa Urais.
 
Lissu asipotoshe dhana ya Uhuru na Maendeleo aliyoijadili kwenye kitabu chake Mwalimu Nyerere mwaka 1968. Kimsingi mwalimu aliamini katika falsafa kuwa uhuru wa bendera tuliopata baada ya kumwondoa mkoloni ulikuwa hautoshi kutoka na kuibuka na ukoloni mambo leo unaosababishwa na mabeberu (imperlists)wa ulaya na Marekani baada ya kugeuza mbinu za kiunyonyaji na kuibuka kwa minyororo ya ugandamizaji kwenye maeneo ya uchumi,siasa na ustawi wa jamii na kiutamaduni baada ya uhuru wabendera 1961.

Hivyo aliona wazi kuwa maendeleo ya taifa ni pamoja na kuutafuta uhuru huo dhidi ya unyonyaji huo mpya ulioibuka na kujificha kwenye misaada na mikopo ya wazungu kwa dhima ya kutuletea maendeleo-Soma kitabu cha Walter Rodney -How Europe Underdeveloped Africa,Cabral, na Silent Class Strugle cha Issa Shivji na wengine. Kimsingi hapa ndipo hoja ya Mwalimu ya kujitegemea kiuchumi ilipoanzia na kujikita akiamini kuwa iwapo tunataka uhuru wa kweli wa kujinasua na unyonyaji wa kiuchumi, na kuingiliwa kisiasa, na kiutamduni ni budi kuacha kutegemea wajomba nje ya nchi kwa kutumia raslimali zetu na si vinginevyo. Siyo dhana ya uhuru anaousema Lissu. Asipotoshe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…