Mambo makubwa uliyowahi kuyafanya utotoni wazazi wakasena wamepata mtoto

Mambo makubwa uliyowahi kuyafanya utotoni wazazi wakasena wamepata mtoto

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
373
Reaction score
895
Wasee mko musuri!

Mada iko open, taja mambo unayoyakumbuka makubwa ya kipekee uliyowahi kuyafanya utotomi mpka wazazi au wakubwa kiujumla wakajivunia wewe.

Nianze namimi.

1. Nakumbuka hili tukio lilitokea nikiwa darasa la tatu kama siyo la nne, nilikuwa chalii sana.
Ilikuwa pumziko saa nne asubuhi, skuli ipo karibu na soko sasa nikaenda sokoni kuzuga zuga maana nilijua kabisa nikienda home ni mbali nitachelewa na nitapigwa na pengine naweza nikaenda home nikakuta apeche alolo nikaishia kunywa maji nakurud skul.

Nipo sokoni nikaokota tsh 100, hiyo mia moja niliyoiokota sikununua andazi, kitumbua wala kishet nilinunua sabuni nikampelekea mama. Asee mama alishukuru sana na mbele yangu nakumbuka maneno yake mpka leo alisema wewe mwanangu ni wa pekee sana.

2. Baba alikuwa mlevi sana kupindukia na pesa alikuwa nayo kimtindo. Sasa alikuwa akitoka home siku nyingine haachi pesa ya kununua mahitaj including msosi, Baba alikuwa ananikubali sana na ningeweza kumkosea pakubwa na aishie kufoka tu.

Alipokuwa anarudi home nilikuwa nampiga sachi kwenye mifuko pesa nayoikuta naenda kununua mahitaji ya home tunakula mimi mabrother masista na mama. Mama na familia kiujumla (ilikuwa) inanitegemea kuongea na wazazi awe mama au Baba kuweka mambo sawa and I'm the last born, nothing can happen or be decided in my absence au bila mimi kuhusishwa.

3. Mwaka 2006 darasa la4 Baba alisafiri na pikpik kuelekea Kijiji cha tatu kutoka Kijiji chetu, alichelewa sana kurudi home siku hiyo ilikuwa siyo kawaida yake kabisa. Home tulikuwa mimi na brother wangu.

Miaka hiyo baba alikuwa na simu flan aina ya Siemens, mimi na bro tukaamua kwenda kwa mtendaji wa kijiji kupiga simu ya baba kumuliza yupo wapi. Namba nilikuwa nimeishika kichwani huwezi amini hiyo namba ya baba ya kwanza kabisa ya Airtel mpaka leo nimeishika kichwani.

Tulivompigia baba akasema ameharibikiwa na pikipiki na ni porini bahati nzuri tu ni maeneo ambayo mtandao ulikuwa unakamata ila baba hakuwa na salio na kulikuwa hakuna vifurushi ni kuweka vocha na kupiga, kipindi kile kupiga simu vijijini ilikuwa inambidi mtu aende kwenye sehemu maalumu hasa za miinuko ili apate mtandao.

Mtendaji alikuwa na pikipiki akamfata baba alienda na spea then wakarud wote. Baba alinishukuru sana.

4. Tulivokuwa darasa la nne tena walikuja watu wa semina kuhusu mambo ya magonjwa ya zinaa. Tulichaguliwa wanafunzi wachache kama wawakirishi kwanzia darasa la4 mpka la7.

Sasa kwenye ile semina mwishoni walikuja kuwa wanauliza maswali. Wakauliza swali kuhusu njia muhimu kuitumia ili kujiepusha na magonjwa ya zinaa huwezi amini wote walishindwa kujibu kwa ufasaha mpaka darasa la saba lakini nilijibu kwamba kuacha ngono nzembe.

Wale jamaa walinichukua nilitembea nao shule zote katika ile kata wakanirudisha home jioni kabisa na wakanipa na tsh elfu15 mwaka huo 2006 ef10 haikuwa kitu ndogo mchele kilo tulikuwa tunanunua tsh mi4 mpaka mia 5 unaweza refer hapo kuona uzito wa ef10. Wenzangu walipewaga elf5 baada tu ya semina kuisha means palepale tulipewa sote buku5 tano then baadaye wakaniongezea 10.

Na mengine mengi siwezi kuyamaliza yote.
 
 
We umenishinda tabia
 
Back
Top Bottom