Mambo makuu unayotakiwa kufanya pale unapohisi kutengwa na wazazi, ndugu na marafiki

Mambo makuu unayotakiwa kufanya pale unapohisi kutengwa na wazazi, ndugu na marafiki

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAMBO MAKUU UNAYOTAKIWA KUFANYA PALE UNAPOHISI KUTENGWA NA WAZAZI, NDUGU NA MARAFIKI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Vijana wengi wamejikuta katika hatua ngumu na Mbaya katika maisha yao baada ya kuhisi kutengwa na watu wao WA karibu kama vile Wazazi, ndugu na Marafiki.
Kutengwa ni Jambo kubwa Sana lakini tangu unapozaliwa maisha yanakufundisha kujitegemea na kuwa pekee yako.

Hata hivyo kutengwa na hata kutelekezwa Kabisa ukiwa bado unajitafuta, hujaweza kujimudu na kujitegemea kimaisha. Watu kukuacha ukiwa down, ukiwa broken, ukiwa huna mbele Wala nyuma inaumiza zaidi. Yaani unaachwa ukiwa katika wakati Mgumu. Wakati ukiwa unauhitaji wa ukaribu na watu.

Inaumiza ni Kweli
Inasononesha kwa hakika.
Lakini maisha ndio yanatufundisha hivyo kila Siku.

Ni lazima utambue mambo haya kwa uchache kuhusu maisha yako;

1. Maisha ni kwaajili yako MWENYEWE hasahasa matatizo yako.

2. Hakuna mtu yeyote wa kukupa furaha isipokuwa wewe mwenyewe. Furaha ya kweli inayodumu inatoka kwako mwenyewe. Wewe ndiye unajukumu la kuitafuta, kuzalisha na kuitunza furaha yako

3. Maisha kila siku yanakufundisha ujitegemee. Kuwa pekeako. Kwa sababu wewe ndio upo responsible, unawajibika na maisha yako kwa asilimia Mia moja na sio Mwingine.

4. Mtu mwingine kukupa furaha sio lazima. Ni hiyari yake(upendo wake) tuu.

JINSI YA KUFANYA PALE UNAPOHISI KUTENGWA NA WAZAZI, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

1. Usipende usipopendwa. Usimtafute asiyekutafuta.
Maisha ni mafupi Sana. Ishi maisha yako ya sasa. Usiishi Jana Wala usiishi Kesho. Ishi Leo. Ipende Leo. Tafuta kusudi la kuwepo siku ya Leo na sio Jana Wala Kesho.
Aliyekaribu yako kuwa karibu yake.
Anayekutafuta mtafute.
Anayekupenda mpende.
Anayekujali Mjali.

Usitafute kupendwa. Ikiwa Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki hawakupendi sio lazima wewe uwapende. Ikiwa hawakutafuti sio lazima uwatafute.

2. Usimuweke Karibu aliyetaka kuwa Mbali nawe wakati wa Dhiki.
Hata awe Nani. Iwe ni Mzazi, ndugu, jamaa au rafiki au mtu yeyote.
Mtu yeyote ambaye alikudharau, ulihitaji ukaribu wake lakini akakukatilia Mbali. Akataka ubaki shimoni. Ambaye hakutaka kukuokoa. Huyo usimuweke Karibu yako kwa wakati wowote ule.

Uhusiano wenu uendelee kuwa Mbali kwa Mbali. Narudia hata awe Mzazi wako kama hakutaka ukaribu na wewe ukaheshimu maamuzi yake. Muweke Mbali.

Msamaha upo lakini Msamaha haumaanishi uwaweke Karibu.
Hata Yusufu alipouzwa na kukatiliwa Mbali na ndugu zake aliwasamehe lakini hakuwaweka Karibu. Aliwatafutia eneo ambalo lipo Mbali na MAKAZI yake.
Hata Adamu na Hawa walipotaka kuwa Mbali na Mungu. Mungu aliwafukuza kwenye macho yake. Aliwasamehe lakini akiacha mahusiano ya Mbali kwa Mbali.
Hiyo ni Kanuni usijichanganye

3. Fanya KAZI kwa juhudi na akili. Jitegemee na unda familia yako lakini usirudie Makosa ya Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wako kwa watoto wako.
Wafundishe watoto wako umoja na ushirikiano kupitia kuonyesha umoja huo na mwenza wako. M
Mke na Mume mkiwa karibu hata watoto nao watakuwa karibu, kuwa wamoja na wenye kushirikiana.
Kutengana na mwenza wako, kutokuwa na mahusiano yenye afya na mwenza wako ndio mwanzo wa utengano wa kifamilia.

Wazazi wenye upendo, umoja na ushirikiano baina Yao huwezi sikia Watoto wakitengwa, kutelekezwa n.k.

4. JIUNGE na jumuiya za Kanisani au Misikitini.
Unahitaji Kampani. Umetengwa kwenu.
Nenda Kanisa unaloabudu. JIUNGE na Kwaya au vikundi vya Kanisani. Tengenezeni mahusiano ya Kiroho. Huwezi jihisi upweke tena.

Roho iliyojazwa na utukufu wa Mungu huwezi jihisi umetengwa.

5. Fanya mazoezi

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Unabidi utafute hela ule bata usimsaidie baba ,mama wala ndugu .

Na pia Mtaani unapokaa usimsaidie mtu yeyote

Kama Roho yako inakutuma kuwasaidia wasaidie kadiri ya hiyari yako.

Kama wakiomba Msaada wasaidie kadiri ya uwezo wako.

Lakini aliyetaka ukae Mbali na hakukutaka kamwe usimweke Karibu yako.

Mahusiano yawe mbali kwa Mbali
 
Mi nimejitenga baada ya kuona hawana msaada kwangu lakini bado wananifatilia kuona wapi naangukia
Kwa maelekezo haya wewe ndo unaonekana bado unawafuatilia au umejuaje wao wanakufuatilia...kama umejitenga jitahidi usitake kujua ata wao wanfanya/watafannya nini juu yako yaan assume kama hakuna viumbe kama hao uliwajua zamani
 
Kama Roho yako inakutuma kuwasaidia wasaidie kadiri ya hiyari yako.

Kama wakiomba Msaada wasaidie kadiri ya uwezo wako.

Lakini aliyetaka ukae Mbali na hakukutaka kamwe usimweke Karibu yako.

Mahusiano yawe mbali kwa Mbali

Unazungumzia familia bora zilizojengwa na msingi wa upendo na sio familia zetu za kibantu ambazo ndugu na wazazi wanakugeuza msukule .
 
Back
Top Bottom