Mambo makuu unayotakiwa kufanya pale unapohisi kutengwa na wazazi, ndugu na marafiki

Unazungumzia familia bora zilizojengwa na msingi wa upendo na sio familia zetu za kibantu ambazo ndugu na wazazi wanakugeuza msukule .

🤓🤓
Alafu wanakutishia Laana.

Bahati nzuri Laana haivunji Kanuni.

Wazazi wengine hutumia Fursa waliyopewa vibaya. Na mtoto akiwa Mjinga asiyeelewa mambo hujikuta kwenye shida na mateso
 
MAMBO MAKUU UNAYOTAKIWA KUFANYA PALE UNAPOHISI KUTENGWA NA WAZAZI, NDUGU NA MARAFIKI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Vijana wengi wamejikuta katika hatua ngumu na Mbaya katika maisha yao baada ya kuhisi kutengwa na watu wao WA karibu kama vile Wazazi, ndugu na Marafiki.
Kutengwa ni Jambo kubwa Sana lakini tangu unapozaliwa maisha yanakufundisha kujitegemea na kuwa pekee yako.

Hata hivyo kutengwa na hata kutelekezwa Kabisa ukiwa bado unajitafuta, hujaweza kujimudu na kujitegemea kimaisha. Watu kukuacha ukiwa down, ukiwa broken, ukiwa huna mbele Wala nyuma inaumiza zaidi. Yaani unaachwa ukiwa katika wakati Mgumu. Wakati ukiwa unauhitaji wa ukaribu na watu.

Inaumiza ni Kweli
Inasononesha kwa hakika.
Lakini maisha ndio yanatufundisha hivyo kila Siku.

Ni lazima utambue mambo haya kwa uchache kuhusu maisha yako;

1. Maisha ni kwaajili yako MWENYEWE hasahasa matatizo yako.

2. Hakuna mtu yeyote wa kukupa furaha isipokuwa wewe mwenyewe. Furaha ya kweli inayodumu inatoka kwako mwenyewe. Wewe ndiye unajukumu la kuitafuta, kuzalisha na kuitunza furaha yako

3. Maisha kila siku yanakufundisha ujitegemee. Kuwa pekeako. Kwa sababu wewe ndio upo responsible, unawajibika na maisha yako kwa asilimia Mia moja na sio Mwingine.

4. Mtu mwingine kukupa furaha sio lazima. Ni hiyari yake(upendo wake) tuu.

JINSI YA KUFANYA PALE UNAPOHISI KUTENGWA NA WAZAZI, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

1. Usipende usipopendwa. Usimtafute asiyekutafuta.
Maisha ni mafupi Sana. Ishi maisha yako ya sasa. Usiishi Jana Wala usiishi Kesho. Ishi Leo. Ipende Leo. Tafuta kusudi la kuwepo siku ya Leo na sio Jana Wala Kesho.
Aliyekaribu yako kuwa karibu yake.
Anayekutafuta mtafute.
Anayekupenda mpende.
Anayekujali Mjali.

Usitafute kupendwa. Ikiwa Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki hawakupendi sio lazima wewe uwapende. Ikiwa hawakutafuti sio lazima uwatafute.

2. Usimuweke Karibu aliyetaka kuwa Mbali nawe wakati wa Dhiki.
Hata awe Nani. Iwe ni Mzazi, ndugu, jamaa au rafiki au mtu yeyote.
Mtu yeyote ambaye alikudharau, ulihitaji ukaribu wake lakini akakukatilia Mbali. Akataka ubaki shimoni. Ambaye hakutaka kukuokoa. Huyo usimuweke Karibu yako kwa wakati wowote ule.

Uhusiano wenu uendelee kuwa Mbali kwa Mbali. Narudia hata awe Mzazi wako kama hakutaka ukaribu na wewe ukaheshimu maamuzi yake. Muweke Mbali.

Msamaha upo lakini Msamaha haumaanishi uwaweke Karibu.
Hata Yusufu alipouzwa na kukatiliwa Mbali na ndugu zake aliwasamehe lakini hakuwaweka Karibu. Aliwatafutia eneo ambalo lipo Mbali na MAKAZI yake.
Hata Adamu na Hawa walipotaka kuwa Mbali na Mungu. Mungu aliwafukuza kwenye macho yake. Aliwasamehe lakini akiacha mahusiano ya Mbali kwa Mbali.
Hiyo ni Kanuni usijichanganye

3. Fanya KAZI kwa juhudi na akili. Jitegemee na unda familia yako lakini usirudie Makosa ya Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wako kwa watoto wako.
Wafundishe watoto wako umoja na ushirikiano kupitia kuonyesha umoja huo na mwenza wako. M
Mke na Mume mkiwa karibu hata watoto nao watakuwa karibu, kuwa wamoja na wenye kushirikiana.
Kutengana na mwenza wako, kutokuwa na mahusiano yenye afya na mwenza wako ndio mwanzo wa utengano wa kifamilia.

Wazazi wenye upendo, umoja na ushirikiano baina Yao huwezi sikia Watoto wakitengwa, kutelekezwa n.k.

4. JIUNGE na jumuiya za Kanisani au Misikitini.
Unahitaji Kampani. Umetengwa kwenu.
Nenda Kanisa unaloabudu. JIUNGE na Kwaya au vikundi vya Kanisani. Tengenezeni mahusiano ya Kiroho. Huwezi jihisi upweke tena.

Roho iliyojazwa na utukufu wa Mungu huwezi jihisi umetengwa.

5. Fanya mazoezi

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Hujawahi kuniangusha.

Vijana wakishapata vihela tu basi huwa wanabadilika, huwa hawaaminintena kwenye umoja wa kindugu for the fact that hawahitaji msaada.

Sasa mambo yanapokwenda kombo wanataka kurudi tena kwa ndugu na familia. Familia nayo imeshasusa. Ndio hapo sasa depression.

Samw scenario huwa zinatokea kwa wasichana wazuri.

Mdada Mkali, Kigori cha kwenda, piki piki na Mark X zinapishana, smart boys na wazee wenye hela hawakatiki.

Lakini Kama Mwanafamilia mnamshauri Dada apunguze speed maana wanaume wengi wana madhara.......Weeee!!! Thibutu anaseoma mnamwonea wivu, zaidi anawambia maisha yake hayawahusu na msimfate fate.

Baadae anapigwa mimba, wazee wote hadi bodaboda wanakimbia.....mara UKIMWI huo.

Anarudi sasa kwa wanafamilia na marafiki wale wale aliowakejeri kwa nguvu nyingi.
 
🤓🤓
Alafu wanakutishia Laana.

Bahati nzuri Laana haivunji Kanuni.

Wazazi wengine hutumia Fursa waliyopewa vibaya. Na mtoto akiwa Mjinga asiyeelewa mambo hujikuta kwenye shida na mateso
Hamna laana yeyote inayoweza kutolewa na Binadamu .

Isipokuwa kila mtu huwa anahukumiwa kupitia karma. What you sow you shall reap .

Wazazi
Ndugu
Watu wa mtaani

👆

Hawa ndo wameleta maanguko Kwa watu wengi kiuchumi ,kiroho.

Pia nature au universe huwa hairuhusu kuwasaidia watu mnaoshare damu moja

Msaada na nguvu yako unabidi kuitoa Kwa watu wa mbali na wewe

NB ndugu au mzazi Kama Ana uhitaji msaidie Ila usimsaidie ili aje akusaidie . utaumia bure baadae
 
Kujitenga haijawi kuwa suluhisho kwa maana nguvu yetu hapa Duniani ipo kwenye umoja yani Universality.

Kuna jambo mwalimu mkuu ya St' Anthony Secondary ya mwaka 2013 aliniambia "Ukitaka kufika mbali nenda peke yako lakini ukitaka kufika mbali zaidi nenda na wenzako. Ukichunguza ni kweli, ndio maana kuna umoja wa nchi matajari yaani G20, kuna umoja wa nchi za ukanda fulani yaani Umoja wa European Countries, Umoja wa African Countries na kuendelea.

Kabla ujataka kujitenga jaribu kujifanyia Self-Inventory yaani kujichunguza wewe mwenyewe kujua Character Assets (Mambo yale mazuri uliyonayo ambayo unajivunia nayo) pamoja na Character Defects (Kasoro ulizonazo). Baada yapo orodhesha kasoro zako na kuanza kuzifanyia kazi moja kwa nyingine. Hapo utafanikiwa na utaweza kujipata na kujijua vizuri Who you are?
 
Unazungumzia familia bora zilizojengwa na msingi wa upendo na sio familia zetu za kibantu ambazo ndugu na wazazi wanakugeuza msukule .
Misingi bora ni mtazamo ,inakuwa unakaa kwenu miaka yote tangu unasoma mpaka unaend mkoani na likizo unarudi...Baadaye ukipata kazi kama ya kuajiriwa unataka ukaishi mbali kwa sababu hazina kichwa wala miguu ni ubinafsi tu.

Hakuna ndugu anakuchukia ila vijana wengi wanajishtukia akipata pesa ,kama kuwanyima unaweza kuwanyima maana ni maamuzi yako ,pesa ni yako.

Siku zote ukijitenga basi kwisha habari yako ,unachukia watu wala hawana muda na wewe.
 
Wewe Una uzoefu mdogo wa maisha .

Mimi naamini katika UPENDO ,umoja na hii ndo falsafa yangu namba moja since day one .

Ndugu , wazazi ni watu muhimu Sana Ila umuhimu wao utakuepo endapo wakajua na kutambua thamani ya kila mmoja.

Watu wengi wenye Upendo wa asili wenye kupenda kujitoa Kwa ndugu zao wengi wameishiwa kuumizwa na nddugu kaisi cha kuwarudisha walipotoka.

So unapokaa na ndugu ni vizuri Sana Ila kwq zile familia bora na sio familia za kibantu ambazo zinakaa kumtegemea mtu mmoja ndo awe game changer wao
 
Mi nimejitenga baada ya kuona hawana msaada kwangu lakini bado wananifatilia kuona wapi naangukia
Kujitenga haijawi kuwa suluhisho kwa maana nguvu yetu hapa Duniani ipo kwenye umoja yani Universality.

Kuna jambo mwalimu mkuu ya St' Anthony Secondary ya mwaka 2013 aliniambia "Ukitaka kufika mbali nenda peke yako lakini ukitaka kufika mbali zaidi nenda na wenzako. Ukichunguza ni kweli, ndio maana kuna umoja wa nchi matajari yaani G20, kuna umoja wa nchi za ukanda fulani yaani Umoja wa European Countries, Umoja wa African Countries na kuendelea.

Kabla ujataka kujitenga jaribu kujifanyia Self-Inventory yaani kujichunguza wewe mwenyewe kujua Character Assets (Mambo yale mazuri uliyonayo ambayo unajivunia nayo) pamoja na Character Defects (Kasoro ulizonazo). Baada yapo orodhesha kasoro zako na kuanza kuzifanyia kazi moja kwa nyingine. Hapo utafanikiwa na utaweza kujipata na kujijua vizuri Who you are?
 
Kwann usitafute upatanishi
Na kwann ndugu na familia ikutenge inamaanisha ww ndo unamattzo

Mara nying tuna tabia ya kusikiliza story upande mmoja lakin ni vema kusikiliza pande zote mbili kbla ya
Kutoa maamuzi

Kaka au dada yako akikuchukia apo unaweza jieleza ila baba na mama yako wakikuchukia jua ww ni ttzo
 
Wewe Una uzoefu mdogo wa maisha .

Mimi naamini katika UPENDO ,umoja na hii ndo falsafa yangu namba moja since day one .

Ndugu , wazazi ni watu muhimu Sana Ila umuhimu wao utakuepo endapo wakajua na kutambua thamani ya kila mmoja.

Watu wengi wenye Upendo wa asili wenye kupenda kujitoa Kwa ndugu zao wengi wameishiwa kuumizwa na nddugu kaisi cha kuwarudisha walipotoka.

So unapokaa na ndugu ni vizuri Sana Ila kwq zile familia bora na sio familia za kibantu ambazo zinakaa kumtegemea mtu mmoja ndo awe game changer wao
Maamuzi ya kuwasaidia ni juu yko sio lazima ,ila kiasilia ni watu mnaendana kwa namna moja...Ukishaanza kuamini hayo nj yale yale ya uchawi .

Sio lazima upate msaada kama mtu uwezo wake umemzidi na yuko pale pale,unafikiria utafanyaje?

Maisha ni kuishi mambo ya kuchukiws ,kalaumu ni mawazo ya mtu binafsi ,hayana uhalasia.
 
Hujawahi kuniangusha.

Vijana wakishapata vihela tu basi huwa wanabadilika, huwa hawaaminintena kwenye umoja wa kindugu for the fact that hawahitaji msaada.

Sasa mambo yanapokwenda kombo wanataka kurudi tena kwa ndugu na familia. Familia nayo imeshasusa. Ndio hapo sasa depression.

Samw scenario huwa zinatokea kwa wasichana wazuri.

Mdada Mkali, Kigori cha kwenda, piki piki na Mark X zinapishana, smart boys na wazee wenye hela hawakatiki.

Lakini Kama Mwanafamilia mnamshauri Dada apunguze speed maana wanaume wengi wana madhara.......Weeee!!! Thibutu anaseoma mnamwonea wivu, zaidi anawambia maisha yake hayawahusu na msimfate fate.

Baadae anapigwa mimba, wazee wote hadi bodaboda wanakimbia.....mara UKIMWI huo.

Anarudi sasa kwa wanafamilia na marafiki wale wale aliowakejeri kwa nguvu nyingi.

Yeah kuna wanaotengwa kwa Sababu ya kiburi cha mafanikio

Wapo wanaotengwa kwa kukosa maadili

Na wapo ambao wanatengwa Kisa wapo down
 
Kwann usitafute upatanishi
Na kwann ndugu na familia ikutenge inamaanisha ww ndo unamattzo

Mara nying tuna tabia ya kusikiliza story upande mmoja lakin ni vema kusikiliza pande zote mbili kbla ya
Kutoa maamuzi

Kaka au dada yako akikuchukia apo unaweza jieleza ila baba na mama yako wakikuchukia jua ww ni ttzo
Kuna sababu tu il watu hawataki kukaa pamoja kusikilizana.
 
Kwann usitafute upatanishi
Na kwann ndugu na familia ikutenge inamaanisha ww ndo unamattzo

Mara nying tuna tabia ya kusikiliza story upande mmoja lakin ni vema kusikiliza pande zote mbili kbla ya
Kutoa maamuzi

Kaka au dada yako akikuchukia apo unaweza jieleza ila baba na mama yako wakikuchukia jua ww ni ttzo

Usiishie kusema Baba au Mama yako. Malizia Baba au Mama muadilifu.
 
Yeah kuna wanaotengwa kwa Sababu ya kiburi cha mafanikio

Wapo wanaotengwa kwa kukosa maadili

Na wapo ambao wanatengwa Kisa wapo down
Mfano Diamond na Ali kiba ni kiburi tu hawajawahi kugombana hata siku moja ,yaani kiburi tu ila siku wakikaa wakaongea utajua hamna tatizo ...Messi na Ronaldo walishinda huu mtego mapema.
 
Maamuzi ya kuwasaidia ni juu yko sio lazima ,ila kiasilia ni watu mnaendana kwa namna moja...Ukishaanza kuamini hayo nj yale yale ya uchawi .

Sio lazima upate msaada kama mtu uwezo wake umemzidi na yuko pale pale,unafikiria utafanyaje?

Maisha ni kuishi mambo ya kuchukiws ,kalaumu ni mawazo ya mtu binafsi ,hayana uhalasia.
Wewe Kama unatoka familia bora na mmekuzwa katika Upendo unabidi kushukuru Mungu Sana .
 
1740640782902.jpg
 
Kujitenga haijawi kuwa suluhisho kwa maana nguvu yetu hapa Duniani ipo kwenye umoja yani Universality.

Kuna jambo mwalimu mkuu ya St' Anthony Secondary ya mwaka 2013 aliniambia "Ukitaka kufika mbali nenda peke yako lakini ukitaka kufika mbali zaidi nenda na wenzako. Ukichunguza ni kweli, ndio maana kuna umoja wa nchi matajari yaani G20, kuna umoja wa nchi za ukanda fulani yaani Umoja wa European Countries, Umoja wa African Countries na kuendelea.

Kabla ujataka kujitenga jaribu kujifanyia Self-Inventory yaani kujichunguza wewe mwenyewe kujua Character Assets (Mambo yale mazuri uliyonayo ambayo unajivunia nayo) pamoja na Character Defects (Kasoro ulizonazo). Baada yapo orodhesha kasoro zako na kuanza kuzifanyia kazi moja kwa nyingine. Hapo utafanikiwa na utaweza kujipata na kujijua vizuri Who you are?

Umoja inakanuni zake. Kuu Kabisa ni upendo
 
Back
Top Bottom