Mambo manne ya muhimu unayotakiwa kua nayo wakati wa kusajili kampuni

Mambo manne ya muhimu unayotakiwa kua nayo wakati wa kusajili kampuni

Kusajili Kampuni Kuna hitaji taarifa nyingi sana, kwenye thread hii nimekuandikia mambo manne ya Muhimu zaidi Kuwa nayo.

1. Namba ya NIDA
Bila namba ya NIDA hutaweza hata kujisajili kwenye mfumo wa Brela, kwahiyo taarifa ya kwanza itakayo kupa next step kwenye usajili wa Kampuni ni namba ya NIDA.

2. Passport ya kusafiria, hii ni kwa ajili ya mgeni anayetaka kusajili Kampuni Tanzania au mgeni anaye partner kusajili Kampuni Tanzania.

3. Katiba ya Kampuni
Ni lazima uwe na MEMARTS au katiba ya Kampuni, yaan memorandum of association na articles of association, hizi unaweza tengenezewa na mwanasheria.

4. Taarifa za Shareholders angalau wawili, directors wawili na secretary.
Sheria za Tanzania Bado haziruhusu single person companies, hivyo ni lazima uwe na taarifa za mtu mwingine ambaye atakua mwanahisa namba mbili, na director namba mbili.

Bila taarifa hizi huwezi kusajili Kampuni.

Hey, naitwa Luhamba Mimi ni mwanasheria na agency freelancer nawasaidia wafanya biashara kama wewe kusajili biashara leseni na Kampuni, kwa Tips za muhimu kama hizi usiache Kuni follow.

Your Favorite Lawyer.
Hivi kama unataka kua na kampuni ya kuchukua vitu nje ya nchi na kusambaza nchini pasipo kuwa na ofisi rasmi kwa maana ya eneo la ofisi,nichukue na kuja kuweka store tu
 
Hivi kama unataka kua na kampuni ya kuchukua vitu nje ya nchi na kusambaza nchini pasipo kuwa na ofisi rasmi kwa maana ya eneo la ofisi,nichukue na kuja kuweka store tu
Kwenye office details unaweka address ya nyumbani kwako
 
Kampuni ilisajiliwa brela mwaka 2016 lkn ukisearch ukingia kwenye website ya brela ukisearch haionekani . Msaada mwenye kujua
Kampuni zote zilizosajiliwa kabla ya 2018 zilisajiliwa offline hivyo haiwezi kuonekana online mpaka ufanye update ya hio Kampuni.
Kufanya update unaweza kufanya kwa siku mbili tuu kama kila kitu kipo sawa.

Nicheki WhatsApp kupitia namba hizi
0678131068 nikusaidie.

Ahsante
 
Back
Top Bottom