Mambo manne yaliyoafikiwa kwenye kikao cha dharura kuhusu kusudio la Manji kujitoa Yanga

Mambo manne yaliyoafikiwa kwenye kikao cha dharura kuhusu kusudio la Manji kujitoa Yanga

Jamjicho

Member
Joined
Jan 25, 2016
Posts
15
Reaction score
11
August 16 2016 ikiwa ni siku moja imepita toka kuenea kwa habari katika mitandao ya kijamii kuwa mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji amejiuzulu nafasi yake ya uenyekiti kwa madai ya kuandamwa na maneno na kujihisi mpweke kwani hakuna mwanachama yoyote wa Yanga aliyeonesha kuwa upande wake.

Baada ya taarifa hizo kuenea viongozi wa kanda wa Yanga walikaa na kuamua kufanya mkutano wa dharura leo August 16 makao makuu ya klabu yao, moja kati ya viongozi wa matawi ya Yanga mkoa wa Dar es Salaam anayeiwakilisha kanda ya Temeke Robert Liungu ametaja maazimio waliyofikia kutoka katika mkutano wa dharura.

1. Mambo Manne waliyokubaliana ni;
Wanachama wa Yanga wanatambua kuwa Manji bado ni mwenyekiti wao kwa mujibu wa katiba yao.

2- Wanachama wamemuomba mdhamini Mzee Katunda amtoe mzee Akilimali anayedaiwa kumpinga Manji atolewe katika nafasi ya katibu wa wazee wa Yanga.

3- Wanachama wanaiomba kamati ya utendaji ya Yanga imuite mzee Akilimali imuhoji na kumsimamisha uanachama kwa madai kuwa yeye ni Simba.

4- Wanachama wa matawi yote wanaendelea kumtambua Yusuph Manji kama mwenyekiti wao
 
Ukiwa na wazo tofauti Yanga uanachama wako u mashakani, lazima utaonekana Simba, hata kama mwanzo ukiongea wanapiga vigele gele.
 
Hapo tayari bundi kaishalia msimu Huyu unaokuja mjiandae kuchezea vitasa vya maana kutoka kwa wekundu
 
Vita mnayoinunua kwa mzee Akilimali siyo ndogo huyo mtu ni nuksi anazijua fitina sana..Mzee Katunda mwenyewe anamgwaya labda afanye kwa amri ya uongozi wa juu
 
Tatizo sio Mzee akilimali tatizo ni kutokufuatwa kwa katiba ya yanga Na kukurupuka kwa ndugu yetu manji kuikopa yanga kabla ya kutathmini kwanza , ushauri kwake ajue kwamba yanga inakatiba alafu Aache udikteta hawezi kuongoza yanga yeye mwenyewe lazima akubali changamoto ya kutoka kwa wenzie
 
Mzee Akilimali hapa naona atashinda kirahisi
Kwanza anayo sababu kwavile haikubaliki timu ikodishwe...hapo hata serikali itaingilia kama wanachama wameshindwa
Pili atawaroga na hapo wengi wataishia kusema nje.
 
Sasa huyo mzee wenu lini tulimpa kadi ya simba? Hii nayo kali isee!
 
teheee eti emekuwa simba mfyoooo watu wazima hovyo kabisa
 
Yaani leo hii mzee Akilimali kawa mshabiki wa simba?Kweli hii mpya.
 
Yaani leo hii mzee Akilimali kawa mshabiki wa simba?Kweli hii mpya.
 
Back
Top Bottom