1. Acacia
Hayati Rais John Magufuli alipiga marufuku usafirishaji mchanga kutoka machimbo ya madini kwenda nje ya nchi, Hayati Rais Magufuli alisema wawekezaji wamekuwa wakikiuka taratibu kwa muda mrefu na kusema Tanzania imeliwa vya kutosha na kumuagiza waziri wa nishati na madini kusimamia suala hilo, wakati tangazo hilo likitoka hisa za kampuni hiyo zikashuka kwenye soko la dunia.
2. Covid 19
Hayati Rais John Magufuli aliongea akiwa Chato akajibiwa toka Washngton Dc aliuliza iweje chanjo ya Ukimwi inafanyiwa majaribio toka mwaka 1985 lakini chanjo ya Corona imefanyiwa majaribio kwa miezi saba tu? pia akawaondoa hofu Watanzania akisema, "Watu tusitishane, tunatishana mno.
Niwaombe ndugu Wakristo na Watanzania kwa ujumla wa Madhehebu yote, huu ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea Mungu kuliko wakati wote, tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kuujenga uchumi wetu, hatuwezi kusalimu amri kwa ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea Mungu na tukashindwa kuendeleza uchumi wetu" amesema Rais Magufuli.
3. SGR
It is not clear why Magufuli’s government has decided to dangle only 400kms of the SGR on Turkey’s face. Some pundits think some sections of the Tanzania SGR might be considered for the Chinese, given China’s huge influence in the region, and its deep pockets for African governments. But it is also clear that Turkey is still interested in all, or at least some more of the sections.
At the January joint press conference with Magufili, Erdogan described the 400 Km request for funding put to him by the Tanzanians as “too small for me”- probably meaning he (Turkey) could do with some more –or all- sections of the SGR project.
4. Bwawa la Rufiji.
Tanzania ilikataa agizo la UNESCO la kuitaka kusitisha Ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge katika pori la akiba la selous, Tanzania ilisisitiza uamuzi wake wa kuendelea na mpango wa kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge Hydro Power Project) yaliyopo ndani ya pori la akiba la Selous mbele ya wajumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya Watanzania,
Hayati Rais John Magufuli alitangaza kutekeleza sera ya kujenga uchumi wa viwanda hali itayopelekea kuwa na mahitaji makubwa ya nishati ya umeme hivyo kwa kuzingatia vyanzo vilivyopo imekuwa ni muhimu sasa kufikiria tena ujenzi wa mradi huo kama chanzo kingine muhimu cha nishati kuwezesha kufikia azma hiyo.
Itakumbukwa kuwa mnamo mwaka 1982 wakati pori hili (Selous) limewekwa katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhifadhi wa Asili (IUCN) liliutambua mradi huo wa Stiegler's Gorge kutokuwa na madhara makubwa katika uharibifu wa mazingira ukizingatia ukubwa wa pori hilo na eneo litakalotumika kujenga mradi huo.
5. CCM
Ujio wa Hayati Rais John Magufuli kama Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama ulileta mabadiliko makubwa ndani ya Chama,moja ya mabadiliko hayo ni ukaguzi wa mali za Chama na kupunguza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama toka 500 hadi kufikia wajumbe 250.
.
Alijuwa pia kuwa 80% ya Watanzania ni wajinga, yaani hawana uwezo wa kuchambua ukweli na uwongo, hivyo basi kila alichosema wakakiamini na wanakiamini hadi leo. Kuna wajinga wanaamini eti aliishinda COVID-19 wakati yeye mwenyewe na akina Kikazi wamekufa kwa COVID-19 kwa jinsi walivyoipuuza.
Magufuli amefanya UFISADI mkubwa sana na kikundi cha wateule wake wachache lakini bado Watanzania wanamuona ni "shujaa" licha ya CAG kuonyesha discrepancies kubwa kwenye Ripoti ya 2020/21.
Magufuli aliiba mpaka uchaguzi wa vitongoji wa 2019 na uchaguzi Mkuu wote still watu wamesahau wanasema eti alikuwa mzalendo.
Kuna maeneo alisema kwa kuwa walichagua wapinzani basi hapeleki miradi ya maendeleo, nako kuna wajinga wakiambiwa eti mafuta yamepanda bei, wanasema angekuwako Magufuli yasingepanda.
No doubt Magufuli alimaster sana the art of propaganda. Alizishika media zote, hadi za nje kuna wakati ikatangazwa kwamba hazipaswi kurusha maudhui ya ndani bila kibali.
Media zote nchi, binafsi na zile za serikali hadi zile ambazo ziko tu online ambazo hazina usajili wa serikali zilijaa woga kumtaja Magufuli katika namna ambayo isingempendeza. Media nchini ziliimba mapambio ya kumsifu na kumtukuza mawizo mpaka machweo.
Propaganda za Magufuli zinanikumbusha propaganda za Adolf Hilter, Joseph Stalin na Mao Ze Dong. Hawa watu walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuaminisha mambo ambayo hayapo, walikuwa na uwezo wa kupandikiza nadharia zao na imani zao juu ya kadamnasi na ikaamini vivyo, huku nyuma ya pazia wakiwa na mauzauza yao kibao.
Magufuli alitupiga wapi? Kwanza alijifanya Rais wa wanyonge, akijua kwamba watanzania wengi over 40% tuko chini ya mstari wa umasikini wa $1 kwa siku, masikini wengi tulimpenda sana tukidhani ni mwenzetu lakini katu, hakuwa mwenzetu, JPM alikuwa tajiri sana.
Magufuli alijua kwamba watanzania hatupendi mafisadi, wengi tunadhani umasikini wetu kuna watu wanatuibia serikalini. JPM akaona atangaze nao vita kali, tukamsahau yeye ambaye alijilimbikizia mali nyingi sana, huku tukijua kwamba anapambana na mafisadi kwa ajili yetu, kumbe ni kwa ajili yake kwani kila alipotaifisha mali zao, zikawa zake na jamaa zake.
JPM master the art of public manipulation. Kwenye ziara zake alisimama barabarani, alizungumza na watu, akatoa fedha hadharani kwa watu wa hali ya chini, alitembelea hospitali na kutoa misaada hadharani kwa watu waliokuwa na hali ngumu huku kila media ikimulika. Vitendo vile vimewalevya wengi kudhani kwamba JPM was saviour, tukasahau kabisa na yeye ni mwanadamu mwenye tamaa na uchu, aliweza kufanya chochote pasi nasi kujua kuwa mali zetu zinaibwa na kuwekezwa kwenye hotels zake, real estate, mashamba na kuficha fedha nje ya nchi. Mtoto wa dada yake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya fedha Dotto James alifanya kazi kubwa sana kusafirisha fedha za mjomba wake nje.
Naona leo wakimkumbuka sana. Nasikitika sana kuona wengi wakimkumbuka JPM pasi na wao kujua kwamba bado wamo kwenye dimbwi la mning'inio wa propaganda za JMP. Ila kama tungejua uozo na madudu aliyofanya nyuma ya pazi, pengine tungezinduka kutoka kwenye hangover hiyo. Tuishie hapo.