Mambo Matano Ziara ya Rais Samia Suluhu Msumbiji

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Amani
Rais Samia alisema amani iliyopo kati ya nchi hizo, inatokana na vyama vilivyopo madarakani hivyo aliomba tunu hiyo ilindwe.

“Sasa ili tuendelee kudumu madarakani lazima tuje na fikra mpya, tujifunze kwa vyama vilivyoondolewa madarakani…amani na utulivu ni matokeo ya vyama vyetu kuendelea kuwepo madarakani, vikiondolewa hakutakuwa na amani.”

Ushirikiano
Rais Samia alisema CCM itaendelea kushirikiana na FRELIMO kuhakikisha amani na utulivu inaendelea kuwepo baina ya nchi hizo.

“Nathibitisha utayari wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na Chama cha FRELIMO kuhakikisha amani na utulivu wa mataifa yetu unaendelea kuwa jambo muhimu,” alisema.

Lugha ya Kiswahili
Rais Samia alihimiza matumizi ya Kiswahili kwa kuwa kuna baadhi ya nchi baada ya kupata uhuru hazikufanya juhudi za kutosha kutumia lugha hiyo na kuendelea kutumia za kigeni.

“Tanzania tunayo kila namna ya kumpongeza Mwalimu Nyerere kwa namna yoyote na kukuza Kiswahili, lugha hiyo inaweza kutumika kama chombo cha kutuunganisha Waafrika, ninaamini kinaweza kuwaunganisha watu kimataifa,” alisema.

Uwekezaji
Rais Samia Suluhu amewataka Watanzania wanaoishi na kufanya biashara nchini Msumbiji kutumia fursa ya ushirikiano wa hizo mbili kuwekeza kwa faida ya pande zote mbili.

"Tunajua kwamba kuna Watanzania wengi wanaoishi na kufanya biashara Maputo, nikiwa na kaka yangu Nyusi tulikubaliana kuwaeleza watu wetu kushirikiana kufanya biashara na kuwekeza kwa manufaa ya nchi zetu,” alisema Rais Samia.

Ulinzi na Usalama
Rais Samia Suluhu ameshuhudia utiaji saini wa Hati mbili za Makubaliano zilizolenga zaidi kuimarisha usalama na amani ambapo saini hizo zilitiwa jijini Maputo siku ya kwanza ya ziara ya kisereikali nchini humo.
 
Tusiingizwe Tena kwenye vita visivyousha vya Msumbiji
Tuliwasaidia kupigana na Mreno kisha tukawasaidia vita na RENAMO kwa gharama kubwa ya fedha na damu. Sasa hii ya Al Shabab wapigane wenyewe.
 
Kuna juice tuliona ina tukio pqle.

Ilikuwaje na tueleweje hapo
 
Tusiingizwe Tena kwenye vita visivyousha vya Msumbiji
Tuliwasaidia kupigana na Mreno kisha tukawasaidia vita na RENAMO kwa gharama kubwa ya fedha na damu. Sasa hii ya Al Shabab wapigane wenyewe.
Tanzania na Msumbiji ni ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…