Umenena Vizuri sana rafiki yangu,
Lakini binafsi ninaamini kuna mikopo mizuri na mikopo mibaya kama ambavyo nimetumia mlinganyo wa 30%.
Ni kweli vyanzo vingi vya maarifa ni ughaibuni.
Pia, kumbuka kuwa makundi mengi ya utaalamu tunategemea vyanzo vya maarifa kutoka ughaibuni kama Marekani, india, canada n.k.
Hii kwangu sio hoja. Hoja ya msingi sana uliyonena ni kuwa tuwe tunadigest maarifa ya kutoa kwa wengine kabla ya kuwashirikisha.
Muhimu; huwa siandiki kuhusu nyumba za kuishi. Nimelenga wawekezaji kwenye ardhi na majengo ambao wanahitaji kujenga utajiri mkubwa kupitia uwekezaji huu.
Na kutokopa kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo ni kipengele cha mbinu ya B-R-R-R-R ya nyumba za kupangisha.
Mbinu hii inawafaa ambao wanaweza kuweka kiasi kikubwa cha akiba kwa ajili kumiliki nyumba ya kwanza.
Nashukuru sana kwa kuandika maoni yenye ushauri mzuri ndani.
Karibu sana rafiki.
Rafiki yako,
Aliko Musa.