Mambo matatu kwa Rais Samia yatakayoimarisha utawala wa awamu ya 6

Mambo matatu kwa Rais Samia yatakayoimarisha utawala wa awamu ya 6

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari jf ,binafsi nimefanikiwa kuishi na wazanzibar wengi sana ,kitu kikubwa nlichokiona kwanza hawana tamaa ya Mali na ni wa aminifu sana.

Hivyo basi binafsi Nina Imani kubwa sana na Rais Samia na kama atayashughulikia haya mambo matatu basi utawala wake utakuwa wa mafanikio sana :-

1.Kuacha kupambana na utawala uliopita ,kiukweli ukiachana na hapa JF huku mtaani na kwingineko asilimia kubwa ya watu wanaukubari utawala wa Hayati Magufuli hivyo kupingana watu wanachokiamini kwa wingi inaleta ugumu kuwaongoza kuliko Ku focus kuongoza taifa.

Kifupi watu huwa wanapenda kusikia kitu kitakacho wafurahisha, ndio maana kina Erythrocyte na wengine Furaha yao ni kusikia utawala uliopita unasemwa vibaya iwe kweli au uongo hawana haja ya ushahidi vivyo hivyo kwa wananchi waliopo mtaani hawataki kusikia JPM anasemwa vibaya .

2. Vetting ifanyike kikamilifu kwenye teuzi mbalimbali ,tunahitaji viongozi bora lakini pia ielewe CCM kwa sasa kuna watu wanaandaa pesa kwa ajiri ya uchaguzi wa 2025 na 2030 watu kama hawa ukiwapa teuzi watatuibia sana .

3. Dhibiti wizi na ubadhirifu ,ukiweza kuwa mkali kiasi kwamba viongozi wataigopa pesa ya serikali utakuwa umetusaidia sana wananchi .

Mwisho kabisa wale waandishi wachumia Tumbo waliandika kitabu i am a STATE , hawakujua Rais ndio state yenyewe wasisikilizwe kikubwa kazi ifanyanyike .ukitaja Russia kuna Putin ,ukitaja USA kuna Biden ,ukitaja Kenya kuna Ruto n.k....

Hivyo basi ukifanyika wizi na ufisadi tutalaumu rais ,nchi ikienda vizuri pongezi kwa rais .
 
Back
Top Bottom