Mambo matatu ya kujua kuwa Mchungaji fulani si Mtumishi wa kweli wa Mungu

Mambo matatu ya kujua kuwa Mchungaji fulani si Mtumishi wa kweli wa Mungu

jerry13

Member
Joined
May 24, 2024
Posts
14
Reaction score
20
Habari zenu wanajamii, siku hizi kuna makanisa mengi sana yanaibuka yenye wachungaji, manabii, mitume, walimu, n.k. Jambo linalopelekea upotoshwaji mwingi kufanyika kwa kutumia jina la Mungu na mwanae wa pekee Yesu Kristu.

Haya ni mambo matatu unayoweza kutumia kujua kanisa au mtumishi gani ni wa kweli na yupi ni tapeli wa imani.

1. Maudhui ya mahubiri yake.
Jambo la kwanza unaloweza kutumia kujua kama mchungaji huyu au kanisa hili ni la kweli sikiliza mahubiri yanayohubiriwa hapo. Jukumu la msingi la kanisa na watumishi wake ni kuwasaidia waumini wao. kuboresha mahusiano mazuri na Mungu wao. Njia kuu ya kuboresha mahusiano na Mungu ni kuwa na imani thabiti nae kwa kuzishika amri zake na kutenda matendo mema. Haya ndo yanatakiwa yawe maudhui makuu ya kanisa pamoja na watumishi wake.

Ukiona kanisa au mtumishi hahubiri kuhusu hayo basi huyo sio mchungaji wa kweli wa Mungu. Ukiona anahubiri zaidi kuhusu mafanikio ya kidunia kama vile kupata utajiri, kutopata shida, kupona magonjwa, uchawi, na mambo mengine kama maudhui yake makuu basi ujue kuna ulakini. Haimaanishi kuwa haya hayatakiwi kuhubiriwa makanisani, lakini lisiwe ndo madhumuni makuu ya mahubiri.

2. Maisha ya gharama na anasa ya wachungaji.
Ukiona mchungaji, mtume, nabii au pastor anayeishi maisha ya kifahari na anasa kwa kutumia sadaka za waumini wake ujue kabisa hapo unapigwa. Maisha ya kifahari na gharama ni kama vile kumiliki gari la mil. 200, nyumba ya milioni zaidi ya 100, na mambo mengine kama hayo basi ujue huyo sio mtumishi wa kweli wa Mungu bali ni mfanyabiashara anayetapeli wananchi maskini kwa kutumia jina la Yesu Kristu wa Nazareth.

3. Miujiza ya kila siku.
Kuna makanisa ambayo kila siku au kila wiki kuna msururu wa watu wanafanyiwa au kutoa ushuhuda wa miujiza. Makanisa ya aina hii hayafanyi kazi ya Mungu.
Hapa kuna mawili kwenye hayo miujiza. Aidha wanafanya usanii kwa kuwalipa watu waigize kutendewa miujiza au wanatumia nguvu zisizohusiana na Bwana Yesu Kristu (nguvu za giza au mazingaombwe).

Hapa sisemi kuwa makanisa na wachungaji hawatakiwi kufanya miujiza, la hasha, maana hata Yesu mwenyewe na mitume wake wa mwanzoni walifanya miujiza mara kadhaa. Lakini hawakufanya miujiza kila siku. Walifanya miujiza pale palipohitajika. Lakini kuna makanisa kadhaa ya sasa wana kipengele kabisa cha miujiza na ushuhuda kila siku au kila wiki ambapo watu hupanga mistari mirefu kupokea hiyo miujiza. Hapo lazima uwe na mashaka rafiki.

Kwahiyi ndugu zanguni, kuweni makini.

Mtume Paulo ameongelea kuhusu manabii wa uwongo katika baadhi ya barua zake. Mojawapo ya sehemu inayoelezea hili ni katika 2 Wakorintho 11:13-15, ambapo anasema:

"Kwa maana manabii wa uwongo ni kama mitume wa uwongo, wanajifanya kuwa mitume wa Kristo. Na hilo si jambo la ajabu, kwa maana Shetani mwenyewe anajifanya kuwa malaika wa nuru. Hivyo, si ajabu ikiwa watumishi wake nao wanajifanya kuwa watumishi wa haki. Mwishowe yao yatakuwa kulingana na matendo yao."
Katika kifungu hiki, Paulo anasisitiza kuwa manabii wa uwongo wanaweza kujifanya kuwa wa haki, lakini utambuzi wao unaweza kupatikana kwa kuangalia matendo yao, ambayo hayakuwa ya haki au ya kweli.

Vilevile, Bwana wetu Yesu Kristu kwenye injili ya Mathayo 7:15-20, ametuonya aliposema:

"Jihadharini na manabii wa uwongo, ambao wanakuja kwenu kwa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wauaji. Mta wajua kwa matunda yao."
Hii pia inaonyesha kwamba tunapaswa kutambua manabii wa uwongo kupitia matendo yao, kwani matunda yao hayaendani na mafundisho ya kweli.

Hivyo, Bwana wetu Yesu Kristu na mtume Paulo wote wanasisitiza kuwa matendo ya watu ndiyo yanaonyesha ukweli wa wao kuwa ni wa Mungu au la.
 
Mkuu nitafutie kanisa wanapotoa sadaka ya kuteketezwa twende jumapili😂😂😂
 
Mkuu nitafutie kanisa wanapotoa sadaka ya kuteketezwa twende jumapili😂😂😂
Mi najua wanapotoa sadaka za kujimaliza😂😂. Hapo unatoa hadi nauli unarudi kwa miguu nyumbani😄
 
Sema wazee wawe wanasaidia raia pia, unakuta inakuja kujengwa shule alafu bei hata sio rafiki kwa asilimia 60% ya waumini wake.

sinaga tatizo na wao kuchukua sadaka, kwa namna moja au nyingine warudishe kwa raia.
 
we utakuwa mchawi sio bure
sasa watu kuponywa magonjwa, kuna shida gani

kuwa tajiri kuna shida gani. Abrahamu alikuwa tajiri na Mungu ndiye alimpa
 
Wawakatie hata bima wazee na watu wenye magonjwa ya muda mrefu. Sio mchungaji yuko na J care Premium alafu waumini wake hawa eleweki.

Unaanza tu na watu 25 au 50 kila miaka inavyoenda idadi inaongezeka, naamini hata Mungu mwenyewe atafurahi.
 
we utakuwa mchawi sio bure
sasa watu kuponywa magonjwa, kuna shida gani
Mkuu, kuna wagonjwa ujue wa kweli ukiacha hao bongo movie wanaopanda huko majukwaani!

Kama watu wanaweza kwenda kwa waganga, isingeshindikana watu kuwajaza wagonjwa wao kwa hao waponyaji! Hakuna hao WATUMISHI hata wakutuliza tu maumivu.

kuwa tajiri kuna shida gani. Abrahamu alikuwa tajiri na Mungu ndiye alimpa
Hao matajiri wa kwenye maandiko, hawakuwaibia waumini sasa! Abraham unayemtaja, alikuwa na mifugo na ukulima wakutosha tu, hakukusanya sada, zaka wala michango!
  • Hakuwapanga waumini kwa magrupu kulingana na uwezo wa kifedha.
  • Hakuwaombea kulingana na dau!

Hawa ni wezi aisee.
 
niliingia chachi moja pastari akaanza kupanga safu za utoaji kuchangia ununuzi wa gari la milioni arobaini. Alianza na safu ya kutoa milioni moja, laki tano, laki mbili na elfu hamsini mpaka mwenye hamsini hakuacha hata senti moja. Nikaona hii si fair kwa waumini wanatoa tu kwa kuburuzwa
 
Mkuu, kuna wagonjwa ujue wa kweli ukiacha hao bongo movie wanaopanda huko majukwaani!

Kama watu wanaweza kwenda kwa waganga, isingeshindikana watu kuwajaza wagonjwa wao kwa hao waponyaji! Hakuna hao WATUMISHI hata wakutuliza tu maumivu.

Hao matajiri wa kwenye maandiko, hawakuwaibia waumini sasa! Abraham unayemtaja, alikuwa na mifugo na ukulima wakutosha tu, hakukusanya sada, zaka wala michango!
  • Hakuwapanga waumini kwa magrupu kulingana na uwezo wa kifedha.
  • Hakuwaombea kulingana na dau!

Hawa ni wezi aisee.
nenda kamsome vizuri Abrahamu maana huelewi chochote
 
Haingii akilini kumchangia pastari ambaye ni tajiri hana shida. Unakuta pastari hana aibu kuchangisha masikini wakati yeye ana majumba ya kifahari, ana magari, ana vitega uchumi lakini anachangisha waumini wasio na kitu. Ifike muda hao mapastari nao waanze kusaidia wahitaji
 
we utakuwa mchawi sio bure
sasa watu kuponywa magonjwa, kuna shida gani

kuwa tajiri kuna shida gani. Abrahamu alikuwa tajiri na Mungu ndiye alimpa
Kwani Abraham alikuwa nabii au mtume? Pili, Abraham alipata utajiri wake kwa kukusanya sadaka au zaka za watu?
Kulingana na mafundisho ya Yesu Kristu, utajiri unaweza ukawa shida kwa mtu kuingia ufalme wa mbinguni. Unakumbuka kuna sehem Yesu akisema, “ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 19:24). Kuna sehemu nyingine Yesu alisema “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au atashikamana na mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kutumikia Mungu na mali.” (Mathayo 6:24). Tafakari hiyo mistari kwa makini ujue maana zake

Hii mada ya utajiri na ukristu ni pana sana na watu wengi, wakiwemo wachungaji, hupotosha sana watu
 
nenda kamsome vizuri Abrahamu maana huelewi chochote
Abraham hakuwa nabii. Angalia manabii kama vile nabii Isaua, Yeremia, Daniel, Ezekiel na wengine. Je walikuwa wanaishi maisha ya kifahari na anasa? Angalia mitume wa Yesu; Petro, Yakobo, na mtume wa mataifa Paulo, je walikuwa wanaishi maisha ya kifahari na anasa? Sanasana walikuwa wanagawana mali zao na maskini na wahitaji. Kwanini wanaojiita manabii n mitume hawafanyi kwa kiwango hicho
 
Haingii akilini kumchangia pastari ambaye ni tajiri hana shida. Unakuta pastari hana aibu kuchangisha masikini wakati yeye ana majumba ya kifahari, ana magari, ana vitega uchumi lakini anachangisha waumini wasio na kitu. Ifike muda hao mapastari nao waanze kusaidia wahitaji
kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom