Mambo matatu yanawezekana kuhusu Nchimbi na kauli zake.

Mambo matatu yanawezekana kuhusu Nchimbi na kauli zake.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Kauli tata za Nchimbi tangu awe makamu wa Rais zinaweza kuwa zinasukumwa na yafuatayo

1. Inawezekana amegundua hayuko kwenye mbio za urais 2030, kwamba tayari wenye chama wameshaamua ni kati ya Mwigulu, Ridhiwani na wengine ila sio yeye hivyo ameamua kujilipua kwa maslahi yake binafsi akiwa hana cha kupoteza tena.

2. Ni mkakati uliokubaliwa na kupitishwa ndani ya chama chake kwamba yeye achukue upande huo wa kujifanya kiongozi wa mabadiliko ili kuwapooza raia ila ukweli ni kwamba hakuna mabadiliko yoyote anayoyakusudia.

3. Ametumwa au anatumika na Watanganyika mashuhuri wanaoona Tanganyika inazidi kupoteza huku Zanzibar ikizidi kushamiri na kuwa na mamlaka makubwa sana kuliko na hadi juu ya Tanganyika.
 
1. Inawezekana amegundua hayuko kwenye mbio za urais 2030, kwamba tayari wenye chama wameshaamua ni kati ya Nchimbi, Ridhiwani na wengine hivyo ameamua kujilipua kwa maslahi yake binafsi akiwa hana cha kupoteza tena.

2. Ni mkakati ulioukubaliwa na kupitishwa ndani ya chama chake kwamba yeye achukue upande huo wa kujifanya kiongozi wa mabadiliko ili kuwapooza raia ila ukweli ni kwamba hakuna mabadiliko yoyote anayoyakusudia.

3. Ametumwa na Watanganyika mashuhuri wanaoona Tanganyika inazidi kupoteza huku Zanzibar ikizidi kushamiri na kuwa na mamlaka makubwa sana hadi Tanganyika atibue maji tu.
Chama cha Mijitu mizandiki
 
Hayo makubaliano kuna uwezekano mkubwa yakavunjwa 2030 na huenda hiki ndicho kinamsumbua Nchimbi
Sijaona kosa la nchimbi au sijakuelewa mana katiba kufanyiwa marekebisho ni ilani ya ccm yenyewe anacho kusema nchimbi kipo kwenye ilani haja kengeuka chochote labda mnataka kutu hadaaa tu
 
Sijaona kosa la nchimbi au sijakuelewa mana katiba kufanyiwa marekebisho ni ilani ya ccm yenyewe anacho kusema nchimbi kipo kwenye ilani haja kengeuka chochote labda mnataka kutu hadaaa tu
Mambo mengi tu yako kwenye ilani ya CCM hata yale aliyokuwa anazungumza Polepole na Gwajima ila hayatakiwi kuzungumzwa au kuzungumzwa namna Nchimbi anazungumza, wanaCCM wanataka yazungumzwe kwa lugha ya Wasira.
 
Huyu Baba kachoshwa kuna michezo ya kuitafuna kwa kasi Tanganyika mfano issue ya kupeleka road funds za Tanganyika Zanzibar.. Kwa tetesi zaidi ya Billion 250 Tshs zinapelekwa Visiwan kila Mwezi. Huku kukiachwa patupu..Ila kwa story za ndaniiii nikama kajishtukia mwezi huo ujao fungu laweza baki bara.
 
Huyo kaona kwenye mbio za kupokezana kijiti ndani ya chama uwezekano wa kupewe yeye haupo.
Ndo maana kaamua kujilipua kupush hoja ya takwa la KATIBA MPYA ili kama itatokea imetiki, basi apite katika mlango wa MGOMBEA BINAFSI maana hii kwenye ile rasmu ya WARIOBA ilipendekeza.

Mi naona mikakati yake ipo steady and smart. Hataki yamkute ya kaka yake(LOWASSA) kukurupuka kuhamia upinzani akaambulia patupu.
Awamu hii CHADEMA hawanunui huo ujinga wa kuokota "watengwa"
 
Kwani aliepo mfumo uliotumika upo kwenye katiba?
Yaj, ipo kwenye katiba kwamba Rais aliyepo madarakani akifariki basi Makamu wake ataapishwa kuwa Rais.

Ndivyo ilivyotokea na baada ya hapo akaamua kugombea kama haki ya kikatiba inavyomruhusu kila mtanzania mwenye sifa.
 
Kauli tata za Nchimbi tangu akiwa makamu wa Rais zinaweza kuwa zinasukumwa na yafuatayo

1. Inawezekana amegundua hayuko kwenye mbio za urais 2030, kwamba tayari wenye chama wameshaamua ni kati ya Nchimbi, Ridhiwani na wengine hivyo ameamua kujilipua kwa maslahi yake binafsi akiwa hana cha kupoteza tena.

2. Ni mkakati ulioukubaliwa na kupitishwa ndani ya chama chake kwamba yeye achukue upande huo wa kujifanya kiongozi wa mabadiliko ili kuwapooza raia ila ukweli ni kwamba hakuna mabadiliko yoyote anayoyakusudia.

3. Ametumwa au anatumika na Watanganyika mashuhuri wanaoona Tanganyika inazidi kupoteza huku Zanzibar ikizidi kushamiri na kuwa na mamlaka makubwa sana kuliko Tanganyika.
I liked your reasoning japo namba 3 sikubalini nayo sana. Nina hili la kuongezea ili kunogesha mjadala zaidi. Kama ulikuwa unamsikiliza Polepole kabla hajauawa, alisema kuwa Samia alitaka kumbadilisha Nchimbi kama makamu wake wa rais kabla ya uchaguzi. Hata mwana dada Mange hili alilisema, kuwa walikuwa wamekosana i.e. Nchimbi na Samia. Je, kuna ukweli kwenye hili? Kinachofanyika sasa ni matokeo ya huo mgogoro au ni geresha yao? Be informed kuwa gazeti maarufu la African intelligence siku kadhaa zilizopita liliandika kuwa kuna mgororo kati ya Samia na Nchimbi. Kama kuna mgogoro wa kweli, je, Nchimbi ana backup ya kutosha kupimana nguvu na Samia plus Kikwete? ( Yes, Samia mama wa nyumbani mwenye elimu ya kuungaunga, kutoka Zanzibar, asingeweza kuwa na jeuri aliyonayo sasa hivi bila backup ya Kikwete). All in all, kama hivi vita ni genuine, na Nachimbi ana backup ya kutosha, basi ni suala linalofanana na mchezo wa chess, kila mmoja anasukuma kete yake kwa uangalifu, na kosa moja kutoka upande wowote, linaweza kumaliza mchezo haraka na bila kutegemewa.
 
Hayo makubaliano kuna uwezekano mkubwa yakavunjwa 2030 na huenda hiki ndicho kinamsumbua Nchimbi
2030 mwinyi,miaka 69 ya uhuru wazanzibar wametoa rais miaka 20 tu, huwezi acha kipaji cha mwinyi kipite tu
 
Back
Top Bottom