Mambo matatu yanawezekana kuhusu Nchimbi na kauli zake.

Kama wana mgogoro kwa vyovyote vile utakuwa kuhusu urais wa 2030, sidhani kama Nchimbi anajali sana ukandamizaji wa Samia na CCM kwa wapinzani na wakosoaji ili mradi yeye ataupata urais.

Kuhusu backup ya kutosha kupambana na Samia na JK anaweza asijali sana pia kama ameona wameshamtoa kwenye mbio, kwa sababu hakuna nafasi nyingine tena anayoweza kushika zaidi ya Urais na akiukosa mwaka 2030 ndio imetoka hivyo wakati wenzake wanaweza kijipanga kugombea 2035 na 2040.
 
Katika mbinu 1000 za kuendelea kubaki madarakani za ccm wametumia 6 tu ya saba ndo hii mnayoiona mtastukia ilikuwa ni mbinu mwaka 2031
 
Reactions: Oho

Hili👆🏾ndiyo liko more likely.
 
katika watu wa kudhania muondoe ridhwani hana mpango wa kugombea,mimi na yeye tina uhusiano ameniambia waziwazi
 
Kwa tafakari yangu naona kama si namba 2 basi namba 3 itakuwa anyway vice versa is true.
 
La tatu ndiyo ukweli wenyewe
 
Katika mbinu 1000 za kuendelea kubaki madarakani za ccm wametumia 6 tu ya saba ndo hii mnayoiona mtastukia ilikuwa ni mbinu mwaka 2031
Hawana mbinu zozote za maana zaidi ya matumizi ya polisi na jeshi kukandamiza upinzani.
 
Nchimbi misimamo yake imenyooka tokea akiwa katibu mkuu, hiyo nadharia ya kasema ametumwa binafsi sina Imani nayo labda kama ilikuwa ni long range planning tokea akiwa katibu mkuu wa chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…