Natoa analysis kama Dr. Riki:
Hapa tunajifunza kuwa courage ni muhimu sana katika kupambana na adui pia na namna ya kufanya na sio kuwa na mabavu tu. Game la tembo na mamba: tembo alitumia mbinu ya kumtoa mamba kwenye maji lakini alisahau kumkanyagakanyaga ingawje dogo alisaidia kumfanya mamba apate uzito usiokuwa wa kawaida; pia dogo alionekana kuwa mwepesi kuliko huyo mama mtu katika kuutoa mkonga au dogo kabla hajafanya kitu anafanya risk assessment kwanza kwani kwenye maji risk ya kushambuliwa na mamba is very high.
Haya game la pili: kwanza nyati wana nguvu sana na wana zana (pembe) za kujilinda lakini shida yao ni uwoga na uzito wa kufanya maamuzi na kutenda kazi kwa pamoja - wamerudi kwa pamoja lakini wanaachiana kuwashughulikia simba baada ya kuwasogelea. Pia nyati wanabahatisha tu ile pembe iliyomrusha simba ilibidi simba aishie kutumbukia kwenye maji na kuwa asusa wa mamba. Simba anasaidiwa na courage. Mamba na simba wote wana-courage na nguvu ila pia wote wako makini kuhakikisha hakuna ambaye anaingia kwenye anga za mwingine - land and water, simba wanamzidi mamba kwa ushirikiano - sidhani kama mamba wanaushirikiano.
Ma-game haya ninayafananisha na siasa za vyama vingi - wapinzani wasikubali kutengana, kukosa courage, kuwa wazito kwenye maamuzi na kuingia kwenye anga za CCM
Ila nasikia mamba na kiboko wana muafaka kama ule wa CUF na CCM; wanaishi pamoja lakini hakuna kudhuuliana!