Mambo mbugani hapo...Vita ya Tembo na Mamba!!!!

Mambo mbugani hapo...Vita ya Tembo na Mamba!!!!

Aaa wapi, tembo hawezi kuuliwa na mamba, Wakongo wanasema "nguvu ya mamba kumai", na mamba kesha tolewa majini. Ila picha ya kwanza dogo kafyata mkonga wake!

Unachokisema ni sawa,lakini kumbuka kuwa tembo tayari ameshajeruhiwa vibaya kwenye mkonga wake na uwenda baadaye alipoteza maisha,kwa kuwa tembo hutegemea kwa kiasi kikubwa mkonga wake katika maisha yake ya kila siku!
 
Hapa kakuta mamba mtoto

Elephant+lizard.jpg
 
Unachokisema ni sawa,lakini kumbuka kuwa tembo tayari ameshajeruhiwa vibaya kwenye mkonga wake na uwenda baadaye alipoteza maisha,kwa kuwa tembo hutegemea kwa kiasi kikubwa mkonga wake katika maisha yake ya kila siku!

A wapi mkonga bado uko fiti...ni kitu sturdy sana mkonga si rahisi kuujeruhi
 
Natoa analysis kama Dr. Riki:
Hapa tunajifunza kuwa courage ni muhimu sana katika kupambana na adui pia na namna ya kufanya na sio kuwa na mabavu tu. Game la tembo na mamba: tembo alitumia mbinu ya kumtoa mamba kwenye maji lakini alisahau kumkanyagakanyaga ingawje dogo alisaidia kumfanya mamba apate uzito usiokuwa wa kawaida; pia dogo alionekana kuwa mwepesi kuliko huyo mama mtu katika kuutoa mkonga au dogo kabla hajafanya kitu anafanya risk assessment kwanza kwani kwenye maji risk ya kushambuliwa na mamba is very high.

Haya game la pili: kwanza nyati wana nguvu sana na wana zana (pembe) za kujilinda lakini shida yao ni uwoga na uzito wa kufanya maamuzi na kutenda kazi kwa pamoja - wamerudi kwa pamoja lakini wanaachiana kuwashughulikia simba baada ya kuwasogelea. Pia nyati wanabahatisha tu ile pembe iliyomrusha simba ilibidi simba aishie kutumbukia kwenye maji na kuwa asusa wa mamba. Simba anasaidiwa na courage. Mamba na simba wote wana-courage na nguvu ila pia wote wako makini kuhakikisha hakuna ambaye anaingia kwenye anga za mwingine - land and water, simba wanamzidi mamba kwa ushirikiano - sidhani kama mamba wanaushirikiano.

Ma-game haya ninayafananisha na siasa za vyama vingi - wapinzani wasikubali kutengana, kukosa courage, kuwa wazito kwenye maamuzi na kuingia kwenye anga za CCM

Ila nasikia mamba na kiboko wana muafaka kama ule wa CUF na CCM; wanaishi pamoja lakini hakuna kudhuuliana!
 
Nafahamu hapa ni habari za picha. Ngoja nitoke nje kidogo kwa wapenzi wa hizi vita.

Angalia hii vita ilivyokuwa ngumu maana hiyo ya Tembo na mamba ni cha mtoto......

Video imeangalia na watu zaidi ya milioni 50.



Nimechekea mpaka jirani yangu hapa ofisini ananishangaa. Lol! kumbe simba nyati ni koboko yao.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom