Mambo mengine si muhimu lakini yakikosekana yanaboa

Mie huwa napenda kukaa na wadada zaidi nikisafiri. Niliwahi kukaa na mkaka, sijui ni nguo hazikukaukaπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈ ile harufu ilinitesaa nikahama siti.
 
Muombe konda akubadilishie seat, unaacha kuomba ufike salama unakokwenda unatamani yutiayi 😏
Mwezi wa saba nlienda Moshi safari ya usiku chuma BM nlikaaa na mzee swala 5++ yule mzee sijui Ile ni kama anatafuna vitunguu Swaum karafuu na manini sijui Yale hata sikufika mbali nliongea na konda akafanya maarifa
 
One time natoka Manyara naenda Dar safari ya usiku kwenye siti yupo binti wa kiIraqw na watoto wawili. Mmoja ni kachanga na mwingine yupo kwenye umri wa miaka 4 au 5 hivi.

Mwanzo nikaghafilika, halafu nikajiambia hakuna namna huyu angeweza mkatia mwanae siti halafu asimkatie. So nikaacha akae dirishani halafu nikakaa kalio moja ili mwanae awe anakaa angalau asipakatwe muda wote.

Nafikiri hicho ndiyo kitu best nimefanya nikiwa safarini.
 
Kwa hakika umefanya kitu kizuri sana boss, sometime hauhitaji gharama kubwa kushow love,naamini kabisa uliikamilisha siku yake vizur sana
 
Huyu mwamba analala balaa,tulipiga mwanzo mbili tatu story fresh tu,ila mwamba analala balaa,now kalala tena
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒHuyo itakuwa kakaaang kabisa nilivo na bahat mbaya nikikaa na mwanaume km hajaomba namba tukifika bas ataanza maongez nje ya safari ninachofanyaga ni kulala had kieleweeke Yani usingiz unaisha najifunika na mtandio usoni njifnya nimelala πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ukikaa na mimi ni Swagga mwanzo mwisho, utajikuta tu Mrembo unasema tuchukue room πŸ˜‚πŸ‘ŠπŸΎ
 
Ila mko wengi kuna mmoja jana alikuwa amekaa mbele mbele,dereva anasema tukitoka hapa mafinga tutachimba dawa morogoro,yeye hana habar kajifunika tu,nikajisemea kuna mwendo kama wa masaa matano muache ajikaushe akipata pee atajua pa kuchimbia dawa
 
Ukikaa na mimi ni Swagga mwanzo mwisho, utajikuta tu Mrembo unasema tuchukue room πŸ˜‚πŸ‘ŠπŸΎ
Huo mda huupati Yan nalala nikiamka kuchimba dawa Nachukua chakula nikimaliza kula nalala Tena Tena usiombe nikae dirishan nakuwekea mgongo kabisa napandisha najifanya usingiz umekolea πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Kuna mmoja uvumilivu ukamshinda akauliza dada unaumwa nikamwambia Jana nilikesha najiandaa safar Ilikuwa ghafla πŸ˜‚πŸ˜‚hivo nimechoka
 
Hali hii niliwahikutana nayo nimepanda gari pale chalinze kwenda mwanza , mara baada ya kukaa kwenye siti mama mwenye watoto wawili akaja , mtoto mmoja wa miezi huyu mwingine kama miaka miwili, daaa nikachoka akili nikasema safari imeshakua ndefu hii nikamsaidia mtoto naye akauliza nashuka wapi nikasema nyegezi naye pia akasema anashuka nyegezi nikajiambia moyoni hapa hakuna namna nilimbeba mtoto mpka tunafika mwanza niko hoi lkn hakukuwa na namna zaidi ya kumsaidia
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Mm nakuwa silali nasikia kilakitu navaa ushungi hivo nachofanya nausogeza usoni πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hahah nimekumbuka nilitoka dom mpka Moro nimelala yule baba ikabidi anaiulize Dada unaumwa malaria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…