Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
NI watu wachache sana ambao wakiandika vitabu kuhusu maisha yao, huwa wanaweka mambo yote makuu yaliyotokea katika maisha yao, kwa kuwa labda wanahofia yatawachafua au yatawapotezea umaarufu. Hivyo basi mara nyingi vitabu kuhusu maisha ya watu ambavyo vimehaririwa na wao wenyewe, hutokea kuwa kama namna tu ya publicity stunts za namna ya kujisafisha mbele ya jamii.
Je, tunaweza kusema hivyo kuhusu kitabu cha Mkapa? Mimi binafsi sijakisoma bado, lakini bado nina shauku sana kujua kama Mkapa ameweka wazi mambo ambayo sisi kama jamii tunaona yameacha maswali mengi kuliko majibu. Kwa mfano, amegusia jinsi alivyopishana vikali na Mwalimu Nyerere kuhusu suala la ubinafsishaji? Na je, Mkapa ameeleza ukweli kuhusu suala la rada iliyoleta mgogoro kama vile EPA? Je, suala la uuzaji nyumba za serikali? Suala la Mradi wa Makaa ya Mawe Kiwira?
Mkapa amegusia kuhusu maisha ya familia na tuhuma za uchawi kwa wazee wake, lakini vipi suala lake la maisha ya ndoa ambalo tumekuwa tukisikia kila namna ya habari, ameliongelea ili kuiweka jamii sawa? Ni kweli Mkapa alioa mtu ambae alikuwa mke wa Basil Mramba au ni porojo tu? Vipi hisia zake pale ambapo hadi watoto walimzomea "fisadi fisadi", ameeleza alijisikiaje kuona hadi watoto wakimtuhumu ufisadi?
Na vipi tuhuma zilizomkabili kuhusu uuzwaji wa NBC ambazo zilifanya karibu uasi wa Bunge utokee, amezigusia? Na vipi tuhuma na mkanganyiko kulelekea mwishoni mwa maisha ya Nyerere, akituhumiwa kumsusa Nyerere akiwa mgonjwa, je ametoa ufafanuzi juu ya hilo? Na vipi mgogoro wa Bulyanhulu watu kufukiwa na yeye kupewa kilo ya dhahabu, na pia kukubali asilimia 5% ya hisa kwa ajili ya Tanzania wakati Nyerere alikataa asilimia 49%, ametoa sababu zinazofanya watu waone kweli hakuwa muuza nchi? Vipi suala la kwamba katika uteuzi wa Kikwete kuwa mgombea wa uraisi wa CCM alikubali japo TISS walimpa taarifa iliyomuondolea sifa Kikwete kuwa mgombea wa wa uraisi? Je ni kweli alimpitisha Kikwete kwa nguvu kwa kuwa Kikwete alitishia kujiunga na Chadema, na wakakubaliana Kikwete amlinde atakapokuwa raisi?
Sasa haya ni baadhi ya mambo ambayo wengine tukisikia Mkapa kaamua kuandika kitabu, tunategemea ayagusie. Vinginevyo inakuwa ni kitabu cha kujikosha na kujisafisha mbele ya jamii. Na kama hajayaweka, basi mie binafsi labda niandike kitabu "Benjamini Mkapa: Your Life, Tanzania's Purpose".
Pengine wewe unajua mengine ya muhimu ambayo unahisi Mkapa alipaswa kuzungumzia katika hiki kitabu alichaoandika, "My Life, My Purpose".