Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Mavazi yana mchango mkubwa refer wale manabii waliokuja na vinjungu walivyozua mjadala
 
Hii inakumbusha wasanii wa Band walivyokuwa wakiibwa kuhamia band nyingine au wachezaji wa soka most of times pesa matters kwenye maslahi hapo ndio pazuri
 
Uko sawa kabisa .

Kuna dogo alifanya kazi taasisi moja private miaka 3 boss anawaghost kila siku tu na story za hapa na pale kila akidai nyongeza ya mshahara kwenye kuhuisha mkataba.

Boss visingizio , ilhali dogo alikuwa anapiga kazi sana saa 11 alfajiri yupo job hata gari ya ofisi muda mwingine hapandi aliibeba ile taasisi kama ya kwake licha ya kuwa yule boss alijaza ndugu kibao waliokuwa incompetent na wavivu walichokuwa wanaweza ni kupeleka umbea na majungu.

Miezi michache iliyopita dogo aliamua kuacha pale kazi, akapata sehemu nyingie kama part time akiwa kapewa ahadi ya kupewa full time maana taasisi mpya inaajiri kwa awamu kila November basi wale wa zamani kujua alipo na msaidizi wa kule awali wakapika maneno kwamba kule aliharibu na uongo mwingine kibao basi huku boss mpya akadraft tangazo kama kawaida la maombi ya kazi mwezi November dogo akapigiwa kuwa afanye application akaapply vizuri hawakumshortlist ndio kuchunguza sana akajua kilichokuwa nyuma ya pazia.

Mind you kule walipotoka ilikuwa wanapitisha miezi saa nyingine 2 bila mshahara wala posho , ameondoka anawadai madeni kule almost 3 M bado akichunguza katika account yake NSSF michango imeinginzwa ya mwaka 1 na nusu tu ilhali alikuwa akikatwa mshahara wake kwa mujibu wa sheria kila jitihada alizokuwa akifanya kama kutuma email au kumpigia boss hakuwa anarespond siku kanipa story yake na kumuuliza huyo boss anaitwa nani nilishangaa sana yule mzee kwanza Professor maarufu tu kwenye taasisi moja , pia dhifa kubwa za kitaifa kwenye kada yao huwa yumo sura yake, kuongea na nilichoambiwa nilibaki ninashangaa maana nimekutana nae kwenye mikutano mingi tu yeye akiwa kiongozi wa mikutano hiyo mingine akiwa chief speaker.

Kama ambavyo Mungu habagui dogo alijikuta amepata kazi almost 3 baada ya kutoka pale na zenye pesa nzuri nyingine ikiwa ni nje ya nchi kabisa kwahiyo kazini kuna mengi sana.
 
hatari sana na ukitaka kutoka kwa boss make sure hajui yeyote unaenda wapi.. ukisaini mkataba ndo kidogoo uwe muwazi maana ni hatari kibongo bongo HR wengi wana rohoo za kwa nini sana yuko radhi waajiri mtu mpya ila sio kukuongezea mshahara
 
hatari sana na ukitaka kutoka kwa boss make sure hajui yeyote unaenda wapi.. ukisaini mkataba ndo kidogoo uwe muwazi maana ni hatari kibongo bongo HR wengi wana rohoo za kwa nini sana yuko radhi waajiri mtu mpya ila sio kukuongezea mshahara
Ndio kilichomkuta nilipomscreen sana alinambia waliondoka pia na wenzie 3 on the same day issue kubwa ikiwa ni maslahi na malimbikizo yao.

Concern yao kubwa ni kufanya kazi mazingira ambayo yana mshahara ule ule kwa miaka almost 3, NSSF michango haipelekwi wanatoka kazini muda mwingine almost saa 4 usiku na hakuna overtime, watu walikuwa na vyeo tu ila hakuna responsibility allowance waliyokuwa wanalipwa.

Ila boss kajaza almost 98% ya watumishi ni ndugu kazi yao kuu ndio hiyo kupeleka umbea na majungu tu.

Na waliahidiwa kulipwa ila hadi wa leo wameishiwa kupigwa danadana tu.
 
kazi zilizojaa ndugu ni msalaaa.
 
Sawa
 
EPISODE 16: Mthamini sana mtu anayeona una kitu ambacho wewe mwenyewe hukioni

Katika maisha yetu ya kawaida iwe kwenye ajira, mtaani au shuleni kuna wale watu ambao wanaweza wakakushauri au kukulazimisha ufanye mambo ambayo wewe jukuwa na wazo nalo au hukujua kama unauwezo wa kulifanya jambo husika. I want to talk about the importance of appreciating and valuing individuals who recognize qualities, potential, or aspects of yourself that you might be unaware of or underestimate, in supporting one's life.

Baada ya kumaliza kile kikao Dodoma tulirudi ofisini kuendelea na majukumu kama kama kawaida. Namshukuru Mungu nilimaliza probation period salama na officially nikawa full employed pale. Kwa ambao mnategemewa kuwa waajiriwa wapya msishangae nakazia kazia sana swala la kumaliza probation period salama, labda niwaambie tuu hiki ni kipindi muhimu sana kwa mfanyakazi mpya kwenye kazi yako au ajira yako mpya. Ni kipindi ambacho mwajiri wako anakupima kama kweli unaweza kuleta tija kwenye kampuni au ni mzigo. Hii inaenda sambamba na kukupima kwenye uwezo wa kutekeleza majukumu yako, uwezo wa kujifunza au kumasta mazingira ya kazi kwa haraka, namna unavyoshirikiana na wenzako pale kazini, maadili ya kazi na swala la nidhamu kwa ujumla, just to mention the few. Makampuni au mashirika mengi mara ntyngi wanatoa kati ya miezi mitatu mpaka sita kulingana na utaratibu wa ofisi husika. Na katika kipindi hiki mara nyingi unakuwa hupewi kwanza stahiki zako zote muhimu mfano bonus kazini na wengine wanakupa kwanza nusu mshahara. Ukifanikiwa kumshawishi mwajiri basi unakuwa unapewa barua yako kwamba you have been successfully completed your probation period and you are endorsed as full employee. So kwa mfanyakazi mpya hicho ni kipindi cha kuwa makini sana ili usiwape sababu ya kukupiga chini au kukuongezea muda wa probation (Probation extension period).

Basi bhana nikawa napiga mzigo pale kutekeleza majukumu yangu kama kawaida. Sasa kwenye ile program mimi nilikuwa na-lead social deparment. Lakini kulikuwa na department nyingine kama medical na M&E. Sasa kwenye kufanya fanya kazi pale karibia tunamaliza mwaka mmoja tangu ile program ianze, ikatokea msala wa mambo ya safeguarding issues pale ofisini. Kwa wasiofahamu, safeguarding issues are the actions or behaviors by employees that may harm or compromise the well-being, safety, dignity, or rights of the individuals the project aims to assist. Inaweza kuwa maswala ya upendeleao, kuomba ngono kwa wanufaika wa progamu, any form of harassment, fraud nk. Ili kupambana na maswala ya safeguarding issues mara nyingi mashirika au makampuni yanakuwa na sera au miongozo ya kuwalinda wafanyakazi na wanufaika wa miradi by providing regular training to employees, establish reporting mechanisms, and conduct thorough investigations when concerns are raised.

Baada ya investigation ule msala uliondoka na watu wengi tu pale ofisini akiwemo jamaa aliyekuwa ana-lead department ya medical. Ile ishu ilichafua hali ya hew asana pale ofsini na kulitokea kuwa na magepu mengi ya kazi. Wazungu wapo seriazi sana na mswala ya safeguarding yaani wanayachukulia kwa uzito mno. Sikuwahi kuexperience hasira za wazungu kwenye kazi lakini kwenye ile ishu walikasirika mno, ilitumwa timu ya investigators kutoka makao makuu Europe pamoja na Nairobi kuja kufanya uchunguzi pale. Nakumbuka shughuli za ofisi zilisimama kama mwezi kupisha uchunguzi na kila mmoja aliwekwa kitimoto hadi CD mwenyewe.

Watu matumbo yaliwaka moto, yaani moja haikai mbili haisimami. Unajua kwenye haya mambo yanayohusisha uchunguzi usiwe unajiamini moja kwa moja hata kama hujafanya maana anaweza akaibuka mtu mwenye visa na wewe akakupigilia kitu kizito ukajikuta na wewe upo kwenye victims. To survive in such issues ni Mungu aingilie kati. Hata baadhi ya watu waliopigwa benchi akiwemo yule leaders wa medical department binafsi ilinguwa ngumu sana kuamini ila ndio hivyo majibu ya uchunguzi yaliomdaka na yeye. Wakati wote wa uchunguzi watu tulikuwa tunaogopana kama ukoma pale ofsini kifupi ilikuwa uwe umehusika au hujahusika kujiamini kulipungua kama sio kutoweka kabisa. Ni kama unapokuwa unasubiria majibu ya ukimwi hata kama ni bikra wa kiume au kike kale kamoment ka kusubiria kanakuletea kahofu flani ka kutokujiamini amini hahaaa.

Basi siku ya siku majibu yakakamilika, kikaitishwa kikao cha staff wote pale ofsini, tukaunganishwa na management ya Nairobi na makuu then report ikasomwa. Kisha maamuzi yakatolewa kwa waliokutwa na ule msala wanaachishwa kazi mara moja kwa mujibu wa sera ya safeguarding. Victims wakaaambiwa kama hawajaridhika na maamuzi wanaweza kwenda kwenye vyombo vya sheria ndani ya mwezi mmoja na kwa muda huo walitakiwa wakabidhi kila kitu cha ofisi. Kwa sisi survivors tulipigwa mkwara mzito kwamba ofisi haitakuwa na mswalie mtume kwa yoyote itakapothibitika kwamba mfanyakazi amejihusisha na violation of safeguarding policy.

Kwa kuwa maamuzi yalikuwa yameshatolewa mara paap wakaingia polisi pale, nafikiri waliandaliwa mapema ili kusimamia zoezi la kukabidhiana ofisi. Nadhani walijihami maana huwezi jua mtu atalipokeaje swala la kufukuzwa kazi tena gafla unaweza ukadundwa au kuuliwa hivi hivi. Basi zoezi la kukabidhi ofisi lilifanikiwa na kwa wale waliokuwa na madeni wanaodaiwa na ofisi wazungu waliamua kuwasemehe, yaani kama walikuwa wanaona kero hata kuendelea kuwadai. Nakumbuka kuna mshikaji mmoja ndio alikuwa ametoka kuchukua advance salalry ya miezi minne na alikuwa hajaanza hata kulipa/kukatwa akawa ametimuliwa na ofisi haikujali.

Nakumbuka baada ya wenzetu kuondoka na wale investigators kurudi kwao maisha yalikuwa magumu sana pale ofisi watu ni kama morale ilishuka sana. Hata shughuli nying zilikuwa haziendi kwa sababu nafasi nyingi zilikuwa wazi. Ikabidi makao makuu wafikiria kurestructure ofisi ya Tanzania ili kuangalia ni namna gani ya kurudisha ufanisi wa ofisi na kujaribu kudhibiti swala kama lile lisijirudie tena. Ikabidi CD na Head of Programs wasafiri kwenda makao makuu kwa ajili ya kulishughulikia hilo. Maana hao ndio walikuwa ndio mabosi wenyewe wa pale ofsini. Iko hivi pale ofisini kulikuwa na nanagement team na baadhi ya wafanyakazi tunaweza kusema ni kudumu kwamaana ya kwamba hawakuwa wanaajiriwa na miradi. Yaani ni hivi hapa tuwekane sawa kidogo, mfano mimi na wenzangu wengine tuliajiriwa na mradi ambao tulikuwa tunautekeleza kwa miaka minne. Kulikuwa pia na miradi mingine tofauti tofauti ambayo nayo pia ilikuwa inaajiri project team yake. Sasa project staff mnaajiriwa na mradi na mnaondoka mradi ukiisha, labda kama kuna mradi mwingine unaweza ukaomba endapo mradi wenu utakuwa umeisha. Lakini kulikuwa na wale ambao tunaweza sema ni wakudumu yaani wao wanaajiriwa pale bila kutegemea miradi ndio akiwemo huyo CD na huyo Head of Programs. Ndio ilivokuwa sijui kama nimeeleweka.

Kule ulaya kwenye kikao chao walikuja na strategies mbalimbali na mabadiliko kidogo ili kuendana na kasi ya utekelezaji wa mradi wetu. Baada ya two weeks walikuwa wamesharudi ofisini na wakaitisha kikao cha staff wote. One hour before the meeting CD akaniita niende ofsini kwake. Nilisthuka kidogo maana haikuwa kawaida CD kukuita ofsini. Mara nyingi kama kulikuwa na jambo anataka mjadiliane alikuwa anakuja mwenyewe kwenye ofisi yako. Ishu ya kuitwa ofsini wafanyakazi wa pale tuliichukulia kwa uzito kidogo. Kihoro kikanishika sana nikajisemea isije ikawa wale investigaors walilisahau jina langu na sasa ndio naenda kuhukumiwa. Usicheke ile situation ilikuwa ni ngumu mno kwa siku ile. Nikasema huyu labda anataka kuniandaa kisaikolojia ili kwenye kikao nikipigwa na kitu kizito isiwe cha kunishtukiza.

Basi nikaingia akanikaribisha pale na straight forward akanimbia “Taidume, the management has entrusted you with leading the medical department, and now you will serve as our medical-social coordinator”. Nikashtuka sana nikamtumbulia macho pale huku nikiwa nina maswali mengi sijui hata nianze kuuliza lipi lifate lipi. Maana nikawa nakiuliza mimi mtu wa massosholoji huko wapi na wapi leo kulead mambo ya madakatari? Alipoona nashangaa akagongomelea kwa kuniambia najua unashangaa hususani kwa kuwa wewe sio daktari na tunakutaka uchukue nafasi ya dakta ………… (akamtaja yule daktari aliyetimuliwa), lakini nikuhakikishie tuu sisi kama menejimenttumekujiridhisha kwamba utaweza.

Binafsi sikukubaliana naye kabisa nakumbuka kile kikao cha mimi na yeye kilichukua kama nusu saa nzima. Mimi nilikuwa nampa hoja zangu za kukataa ile nafasi lakini yeye anazipangua kwa kuniaminisha kwamba naiweza ile nafasi. Sasa, mimi sio kwamba nilikuwa tu siitaki ile nafasi lakini nilikuwa naona napwaya na italeta shida kwenye ufanisi wangu. Maana kwanza nilikuwa nawaza kwa harakaharaka pale namna yule dakatari alikuwa anafanya kazi zake. Yeye shughuli zake kubwa alikuwa anafanya na madakatari wenzake mikoani na wizarani, maswala ya kusimamia upimaji, utoaji dawa na ufuatiliajo wa maendeleo ya walengwa wetu. Kwanza nilikuwa namsikia tu hayo mabombastic ya kidaktari anaovoongea na madaktari wenzie basi mimi nikawa navurugwa tuu nikaona huyu CD vipi huyu naona ananitafutia tuu sababu ya kunitimua kazi maana performance ikiwa ndogo nayo ni ishu sana kufanya kazi na wazungu.

Nakumbuka tulivutana sana kwenye hilo. Mwisho wa siku CD akanipa job description ya ile position akasema tuzijadili moja moja. Yeye akawa anasoma kipengere kimoja kisha ananiuliza nimekiewlewaje? Nikawa naelezea kile kipengele nilivokielewa. Kwa ufuoi inaonekana aliridhika na jinsi nilivovielewa vile vipengere vya job description. Mwisho wa siku akaniuliza hapo sasa ni ni kigumu kwako? Kiukweli nilivyovipitia ile vipengere vya majukumu, asilimia zaidi ya 70 ilikuwa ni kuoragnize na kucoordinate the project implementation partners watekeleze majukumu yao within time and budget, baasi. Sikuhitajika kuwapima walengwa, wala kutoa dawa, wala kutoa ushauri wa kidaktari, hizi zote walikuwa wanatakiwa kufanya madakari wa mikoa husika huko tunakofanya kazi. Kwahiyo sikuhitajika kuvaa koti jeupe na Stethoscope kama madaktari wanavofanya. Yale mambombastic ya kidaktari zilikuwa ni mbwembwe za kututisha wengine hahaaa. Maana nakukumbuka kwenye zile reflection meetings au weekly feedback meeting na kupeana updates za mradi yule bwana daktari alikuwa anashusha vigongo sana mpaka wengine tukawa tunajisemea kumbe udaktari ni mgumu hivi na inaonekana wanaakili sana madaktari (jokes).

Basi nakumbuka CD akanikumbusha ile ishu niliyoorganize meeting na watu watu wa wizara ya afya wakati tunaenda kuutambulisha mradi, ile ambayo nilipata msala wa kusekwa sello. Akaniambia, that was an excellent entry point that the management team built trust in my coordination abilities. Nikajisemea laiti mngejua nililazwa selo sijui ingekuwaje hahaha. CD akaniambia “Taidume wewe una kitu kikubwa sana sema tuu hujijui. Naweza nikakuambia ilikuwa rahisi sana mimi kushawishi menejimenti kukubaliana tukuongezee hiyo idara kwa sababu naamini una skills na uwezo wa kudili na complex issues katika kudeliver project results”. Mimi nikamwambia kama vipi anipe muda nikafikirie, akanikatalia na kuniambia that was like an order to me and he is going to officially announce that to all staff in the meeting. Akaniambia tukimaliza mkutano atanipa my new contract.
Kwa upande mmoja nilikuwa na hofu lakini kwa upande mwingine nilikuwa nilikuwa na furaha. Hofu ilikuwa vipi je nitaweza kuhandle yale majukumu maana ilikuwa ni kama nafasi mbili kwa moja. Lakini pia niliassess the situation nikasema hapa lazima vijimaneno vitazuka maana wakati wa investigation kama ilivokawaida kunakuchomana sana, sasa nikawa nahofu kwamba lazima kuna watakaofikiria kwamba niliwachoma watu na asante yake ndio hiyo nafasi. Maswala ya uchawa hayo. Kwaupande mwingine nilifurahi kwa sababu hakuna kitu kizuri kama kuaminiwa tena wakati wewe mwenyewe ukiwa haujui kama una huo uwezo. Inakupa faraja sana, nilishawahi kuaminiwa katika maswala mbali mbali lakini haikuwa kwenye levp ya surprise kama ile. Nikajisemea mwenyewe let me take it, mambo mengine yatajiset juu kwa juu.

Basi tulikubalina hivyo. Muda wa kikao ulipofika staff wote tulikuwepo. Basi CD pamoja na mabo mengine akatoa mrejesho wa safari yao ya makao makuu. Akatoa feedback ya mikakati mbali mbali waliyokubalina na management team namna bora ya kuendesha ofisi ili swala lile lisijirudie tena. Watu wakauliza maswali na yakajibiwa na kusisitizana kuhusu hiyo mikakati mipya, mwisho wa siku CD akatangizia kwamba kuna baadhi ya nafasi zitatafutiwa watu wengine lakini kawaambia kuhusu ishu ya mimi kuwa appointed to lead also the medical unit of our project. Watu wengi hawakutegemea na walipigwa na mshangao, lakini ilibidi wakubaliane na ukweli huo maana ilikuwa tayari imeshaamuliwa na management tena kwa kupewa Baraka zote kutoka makao makuu. Basi walinipongeza pongeza pale na ndio ikawa stori kubwa ya siku.

Tulipomaliza mkutano, nikaenda ofisini kwa CD nikamkuta wakiwa na HR. basi nikakabidhiwa contarct yangu nikatakiwa niisaini by kesho yake maana ile position ilitakiwa ianze immediately. Nikaingia ofsini kwangu nikawa naipitia mdogo mdogo. Najua wengi mtataka kujua kama kulikuwa na nyongeza ya mshahara. Ofcourse kambuzi kaliongezeka kidogo japo kalikuwa bado hakajanona kiviile. Mimi nikausaini hapo hapo na kurudisha nakala moja kwa HR, officially nikaanza majukumu mapya. CD aliandika barua kuwasiliana na partners wetu hususani wale wapya kwangu (madaktari) kuhusiana na mabadiliko ya ile nafasi, huku akiwaomba ushirikiano.

Nikapanga mkakati wa kwenda kutembelea maeneo yote ya mradi ili kufahamiana na partners ili kwa pamoja tuweze kuweka mikakati mipya. Kwakweli nashukuru walinipa ushirikiano wa kutosha sana na tulifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa sana. Changamoto ndogondogo ni kitu cha kawaida na tulifanikiwa kuzimaliza na kusonga mbele.

Kiufupi na kwa ile ofisi ya wazungu nilifanikiwa kujiimarisha au kuongeza ujuzi katika maeneo yafuatayo
  • Experience in designing and implementing projects.​
  • Skills in project planning, budgeting, and resource management.​
  • Understanding of project lifecycle from inception to evaluation.​
  • Knowledge of fundraising strategies and techniques.​
  • Leadership skills in supervising personnel and resources.​
  • Ability to coordinate with implementing partners including government officials​
  • Skills in monitoring program effectiveness and impact.​
  • Relationship-building with community leaders, government, and local organizations.​
  • Identifying and addressing training needs for staff, partners, volunteers, and local organizations.​
  • Presentation skills for sharing program reports and findings with management, donors, and stakeholders.​
Nilifanya ile kwa muda wa miaka minne na tukafanikiwa kuhitimisha na kuumaliza ule mradi salama salmini. Mradi uliisha tangu Disemba 2022 lakini mimi niliombwa kubakia pale ofsini kwa miezi mingine mitatu kusaidia kukamilisha baadhi ya mambo hususani mfadhili wa mradi alikuwa anayahitaji. So officialy nilirudi uraiani mwezi wa tatu na kuanza harakati mpya za kusaka ajira nyingine.

MWISHO:
Wadau wangu yapo mengi sana ambayo ningeweza kushea nanyi naomba mniwie radhi kama haya machache hayakuwatosha. However, as I reflect on the chapters of my professional journey, each episode has been a lesson with the vibrant sort of experience. Your time invested in reading my story is sincerely appreciated. In sharing these moments of growth, challenge, and achievement, my hope is that you have found inspiration and some thing to takehome as an assignment.

Nimesoma na nitaendelea kuzisoma koments zenu kwa umakini mkubwa na binafsi nimefarijika kwa maoni, maonyo, mafunzo na mijadala ambayo imekuwa ikiibuka katikati ya stori, hahaa hii ni kawaida. Kwa pale nilipoweza nilitoa na nitaendelea kutoa ufafanuzi na kwa wale wanaonifata PM for more detals, I respect and salute you guys.

Kwa kipindi hiki ambacho nahangaika huku na huko kusaka sehemu nyingine nafanya kazi za kujitolea kwenye maeneo mbalimbali hususani vile viNGO vidogo ambavyo ndio vinaanza. Pia kuna watu hata humu JF wapo tunasaidiana kudizaini concept notes na kuandika full project proposals. Huwa najitolea kwa wale ambao nimehakikisha hawana uwezo, maana hata mimi nikiangalia nilikopita pita mpaka hapa nilipo sijawahi kutoa hata sh10 ili kusaidiwa.

Nipo hapa pia kuendelea kutoa uzoefu wangu kwa yeyote ambaye anaona nitafaa kushea naye ninachokifahamu muda na wakati wowote. Na pia ninawaahidi kama nitafanikiwa kupata sehemu nyingine ya kupiga mzigo basi niatwashirikisha hapa hapa. Kwa sasa bado natafuta kazi.

Thank you guys niwatakie maandalizi mema ya sikuku za mwisho wa mwaka na heri sana ya mwaka mpya 2024 kwenu woote. Na kama kuna mtu kwa namna moja ama nyingine nimemkwaza naomba anisamehe, Mungu awabariki sana.

MIALIKO YA SIKUU INAKARIBISHWA PIA

TaiDume 0748 586 059​
 
Hongera kwa uandishi makini.

Na pia kwa kutoa muda wako kuweka taarifa hizi ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwa wanaoanza au wanaotarajia kupata ajira.

Nami nakutakia kila la kheri na , ninaamini 2024 hautofikisha mwaka tena utakuwa umepata kazi.
 
Nice mkuu, good experience to share, umetufungua macho wengi mno na timeishi kwa niaba yako maisha tuliokuwa tunapenda kuishi hususani Mimi binafsi nilikua na kiu sana ya kufanya kazi kwenye NGO za kimataifa nipate experience na kufill maisha yanaendaje ila kwa hii experience yako nimeishi hayo kwa uchache na hata duku duku la kukosa kazi za miradi ya mashirika limeisha, salute sana mkuu. All the best in your new upcoming endeavors. Peace🙏
 
Shukrani mkuu! Nitakutafuta.
 
Hatari sii mchezo
 
🔥🔥🔥👊
 
Mbona kama imekua fupi sana... Anyway Asante sana mkuu kwa kutenga muda wako na kushare na sisi madini haya. Wish you all the best on your endeavors.
 
Mradi uliisha tangu December 2023 au 2022??nadhani umechanganya hapo
 
Mimi naona yuko sawa tuu sio kila sehemu uhitaji kuwa loyal …kwenye kazi ni kuchapakazi na kutafuta hela tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…