Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Heri ya Mwaka Mpya wakati tunajiandaa kuanza kazi katika wiki ijayo baada ya likizo ya Mwisho wa mwaka ni kipindi kwanza kujua kama mahesabu yako ya mwaka jana yamekaa vyema kwa kuanza kuandaa final accounts wakati ukiangalia ni Kodi kiasi gani utakuwa unatakiwa kulipa mpaka hapo itakapofika mwezi wa sita.
Pili kikubwa ni kuanza kufuatilia mipango yako uliyoiweka mwaka jana naamini umepata some clarity ya nini kinachotakiwa kukifanya kwenye biashara yako ili ifanye vizuri zaid.

Tatu ambacho ni muhimu ni mapngo wako wa kodi (tax planning) ambayo itakuwa kama utafanya vizuri hapa au vibaya nini kinaweza kuwa kadirio zako la kodi zote kwa pamoja yaani kodi ya mapato( Income Taxes), Withholding taxes, SDL, VAT na nyinginezo zinazokuangukia ila iwe na uwezo wa kuzilipa pale zinapokuwa zinatakiwa.

Nawatakia Mwaka Mwenye mafanikio Tele.
 
What's the difference between partnership and limited company??
The main difference is Corporate tax inachajiwa kwenye Company profit while kwny partnership kodi haichajiwi kwa partnership bali inachajiwa kwa wale individuals wanao form hio p/ship yani(partners)
 
Safi na nyingine na nyongeza ni madeni (liability) vile vile inaenda mpaka kwa wamiliki ila kwenye kampuni inaishia kwenye umiliki wa kampuni hayawezi kwenda kwa wamiliki. Ukomo wa madeni au madhara yoyote ya kampuni yanaishia kwenye ukwasi wa kampuni.

Sawasawa kabisaa mkuu.
 
karibu ndugu

QUOTE="mng'ato, post: 25151377, member: 255832"]Sawasawa kabisaa mkuu.[/QUOTE]
 
Kama ulipata usajili brela itapidi mupeleke returns Brela yaani ya 2016 tarehe ile mliopata usajili. Vilevile napenda kujua ulipata TIN?
Mkuu nimesajili kampuni Dec 2016 sijawahi kupeleka hizo returns Brela, je fine yake hapa imekaaje?
 
Hiyo unaweza inatakiwa upeleke sasa ada ni tshs 22,000 kwa mwaka na hapo ni kama umechelewa mwezi mmoja kwahiyo fine yake ni Tshs 2,500/ so itakuwa kama 24,500 Tu.
Ahsante

Asante sana mkuu
 
Mojawapoo ya jambo muhimu katika kipindi hiki ni vyema kujua kwa karibu makadirio yako ya kodi katika kipindi kijacho kitakuwaje. Wakati unasubiri kuweka vyema mahesabu yako ya mwaka jana ni vyema kabla ujaenda kuweka makisio yako ya kodi kupata hata ushauri kwa wataalamu ili ikusaidie kufanya makisio yaliyo sahihi. Ili usipate shida ya kukadiria juu sana au kukadiria chini (Over and Under Estimates) maana itakugarimu katika kufanya biashara.
 
Wekeza kwenye biashara yako ili ikupe matunda. Fikiria kila wakati jinisi ya kuimarisha na jinsi ya kubadilika kutokana na wakati uliopo.
Mkuu mwaka 2016 wakati nafanya makadirio, TRA waliniambia kama mauzo ya kampuni kwa mwaka hayafiki milioni 50 siruhusiwi kusajiliwa na VAT.

Naomba ufafanuzi kwenye hili.
 
Sharti la kwanza la kusajiliwa kuwa VAT ni kwamba uwe na mauzo yaakuanzia 100m kwa miezi kumi na mbili au uwe umeshafikisha mauzo ya 50m kwa miezi sita ya kwanza . Ndio maana hao maofisa wa TRA walikueleza kuwa kigezo hicho hukufikia na hivyo afisa wa TRA hakuweza kukusajili kama VAT entity. Exceptional iko tu kwenye professional services provider au Government entity.

Mkuu mwaka 2016 wakati nafanya makadirio, TRA waliniambia kama mauzo ya kampuni kwa mwaka hayafiki milioni 50 siruhusiwi kusajiliwa na VAT.

Naomba ufafanuzi kwenye hili.
 
Mojawapoo ya jambo muhimu katika kipindi hiki ni vyema kujua kwa karibu makadirio yako ya kodi katika kipindi kijacho kitakuwaje. Wakati unasubiri kuweka vyema mahesabu yako ya mwaka jana ni vyema kabla ujaenda kuweka makisio yako ya kodi kupata hata ushauri kwa wataalamu ili ikusaidie kufanya makisio yaliyo sahihi. Ili usipate shida ya kukadiria juu sana au kukadiria chini (Over and Under Estimates) maana itakugarimu katika kufanya biashara.
Mkuu Asante sanaa umetoa somo zuri sanaa tena for Free. Aisee Mungu akulipe

Mie nilisajili jina la kampuni likawa approved Brela lakini before sijasaini ile document nikapata wasi kidogo na sikua na uelewa vizuri na mambo flani flani ylinipata stuck kidogo

1. Kwa mfano nimefungua kampuni ya mtaji wa 50M fee Brela ni 440K je nitailipa kila mwaka?
2. Kama sijafanya biashara au Return ni Zero Nitadaiwa kodi TRAvipi 30% cprate Tax?
3. Ukipewa Leseni maanake ni kwamba ulipe kodi TRA je haihusiani na 30% Corprate tax at the end of year kwa kampuni
4. Makadirio ya kodi yanafanyikaje ni kwenye mtaji au laa

Naomba msaada wa haya maswali yananipa utata mkuu
 
Ahsante sana nashukuru kwa baraka zako ila naamini kuna siku italipa ndio nimeanza na hiyo free . Ingawa karibu ya mambo yote hayo uliouliza mengi yameajadiliwa humu ngoja nilijitahidi kujibu inaweza kuwa summary nzuri kwa hapa tulipofika.
Majibu chini kwa rangi nyekundu na majibu hayo ni kwa elimu tu haindoi kupata ushauri wa kitaalamu au haitausika na madhara yoyote yatakayotokana nayo. Cavier nazo muhimu siku hizi.

Hapana hiyo ni ada ya kufungulia kampuni yenye mtaji huo na inalipwa mara moja kila mwaka kwa sasa utalipa Tshs 22,000

2. Kama sijafanya biashara au Return ni Zero Nitadaiwa kodi TRAvipi 30% cprate Tax?

Hapana Kodi hii ya cooperate tax inachargiwa tu kwenye faida yaani kwa ufupi (Mauzo kutoa matumizi yote yanayokubalika kwenye biashara)

3. Ukipewa Leseni maanake ni kwamba ulipe kodi TRA je haihusiani na 30% Corprate tax at the end of year kwa kampuni

Ukipewa leseni maana umekubaliwa kufanya biashara husika na ili upata leseni inabidi upite TRA ambako huko utaulizwa documents zako za usajili, na hapo utapewa namba ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN number). Na utapewa tax clearace ambayo itakuwa ni kitu muhimu cha kukusaidia kupata leseni. Maana bila hiyo tax clearance huwezi kupatiwa leseni. Na leseni ziko mbili zipo hizi zinazotolewa na Manispaa kwa biashara class B ambazo ni ndio nyingi, bali pia ziko zinazotelewa na wizara ambazo kwa sasa wamehamishia kitengo kwenye jengo la Ushirika. (Hizi ni kwa biashara ambazo zinaweza kucover Tanzania na vile vile zimeaanishwa kuwa leseni zake ni kwenye level hii.)

4. Makadirio ya kodi yanafanyikaje ni kwenye mtaji au laa

Kwa kuwa kodi za mapato inatagemeana na faida kwahiyo unavyojifanyia makadirio unaangalia ni faida kiasi gani unategemea kupata kwa mwaka halafu unagawanya kwa robo mwaka nido utaijaza kwenye hayo makadirio

Naomba msaada wa haya maswali yananipa utata mkuu
 
Ahsante sana nashukuru kwa baraka zako ila naamini kuna siku italipa ndio nimeanza na hiyo free . Ingawa karibu ya mambo yote hayo uliouliza mengi yameajadiliwa humu ngoja nilijitahidi kujibu inaweza kuwa summary nzuri kwa hapa tulipofika.
Majibu chini kwa rangi nyekundu na majibu hayo ni kwa elimu tu haindoi kupata ushauri wa kitaalamu au haitausika na madhara yoyote yatakayotokana nayo. Cavier nazo muhimu siku hizi.
Barikiwa sanaa mkuu. Mungu akuongozee siku zote uaminifu ni mtaji ukianzisha ata consultation naimani watu hawatosita kukupa kazi kwa sababu umejipambanua vizuri na umejitolea sanaa kusaidia watu openly. wengine ungesikia Njoo PM
 
Nakushukuru sana ila mimi ni kweli mimi ni mshauri wa biashara ( Consultant) kaka hii kwangu ni kama huduma kwa jamii na katika hili napata mkate namshukuru Mungu. Na kitu kikubwa nilichojifunza ni kwamba kanuni ya kupata ni kutoa. Maana watu wanalipwa kwa kutatua matatizo ya watu.

Barikiwa sanaa mkuu. Mungu akuongozee siku zote uaminifu ni mtaji ukianzisha ata consultation naimani watu hawatosita kukupa kazi kwa sababu umejipambanua vizuri na umejitolea sanaa kusaidia watu openly. wengine ungesikia Njoo PM
 
Nimekuwa nikiskia kampuni haimilikiwi na mtu mmoja, je nitafanyaje kama nina mtaji wa kutosha kufunga kampuni ninyohitaji lakini ama sitaki kuwa na wanahisa wengine kwenye kampuni yangu au sina watu wengine wa kuwa wanahisa wa kampuni yangu?

Ahsante.
 
Back
Top Bottom