Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Jitahidi kila mara kwenye biashara yako kuongeza ubunifu na kwenda extra mile kwenye kila unachokifanya. Maana ukitatuta kwa usahihi na kwa right attitude wateja watakutafuta siku zote.
 
Napenda leo nisisitize kwa mara nyingine umuhimu wa kuandaa mahesabu yako mapema kwanza mida kama hii uwezekano wa kupata bei nafuu na kazi yako kufanyika kwa umakini mkubwa ni rahisi kuliko ukingojea wakati kila mtu anawatafuta hao watu bei lazima itakuwa umepanda.
 
Intergrity ya shughuli na biashara yako ni kitu muhimu kuliko maelezo nacho kuwa na tabia ya kukiangalia kuna mambo ambayo yanaweza kuishusha au uko kwenye hatari ya kukubwa na kasfa yoyote ni vyema uwe na viashiria vya kuangalia kama kweli kila wakati shughuli zako zinaendeshwa kwa kufuata taratibu za nchi na mazingira sahihi ya biashara yako.
 
Muda mzuri wa kujaza annual estimates returns ndio huu hapa, ambapo foleni sio nyingi na unaweza kupata watu wa kukushauri vizuri. Tafadhali tumia muda huu kufanya hivyo.
Ahsante
 
Mwezi huu nao watu wengi huwa wanasahau sana mambo mengi ya kodi hasa zile za mishahara ambazo zilikatwa mwezi wa kwanza na VAT return kwa sababu hainaga deadline kubwa. Ukilinganisha na mwezi tunaouendea lakini jua kuwa mambo yote unayoyaweza kufanya mwezi wa tatu na huu unaweza kufanya. Na mara nyingi ofisi za mapato zinakuwa sio busy sana unaweza ukapata hata nafasi ya kushauri na wafanyakazi wa mamlaka na hata kusikilizwa vizuri zaidi kwa nafasi. Nawasihi mtumie muda huu vizuri
 
Mkuu naomba kujua kuhusu service levy, huku mkoani kwangu nimeona wanafungiwa na watu wa halmashauri, na mimi nina company yangu hapa ina mwaka sasa sijawahi lipia.
 
Service levy hii inachargiwa kwenye halmashauri unayofanyia biashara na mara nyingi ilikuwa haifuatiliwi sana sasa katika kwenda kwenye uchumi wa kati hii nayo lazima ifuatiliwe na inatakiwa itokane na mauzo na kila robo ya mwaka inabidi ipelekwe. Soma kwako katika sheria ndogo za Halmashauri wewe unatakiwa ulipe nini upeleke kwa wakati. Halafu hapa nafikiri halmashauri zingiweza kufanya vizuri kwa sababu wao ni miongoni wanatoa leseni za biashara wangeweka kama ujalipa hii hupati license mara moja hii hela ingekuwa inakusanywa kwa wakati ili na walimu wetu na huduma kwenye halmashauri ziwe bora.

Mkuu naomba kujua kuhusu service levy, huku mkoani kwangu nimeona wanafungiwa na watu wa halmashauri, na mimi nina company yangu hapa ina mwaka sasa sijawahi lipia.
 
Wandugu naomba ndio tunaeelekea mwisho wa mwezi wa tatu ni moja na mwezi muhimu sana kwasababu tunaelekea mwisho ya robo ya mwaka ya kwanza.
Hapa kwa mfanyabiashara makini unatakiwa kuwa umeshafanya estimates returns na sasa unajipanga kulipa kabla ya deadline ambapo huwa kuna foleni nyingi na unaweza usiwe ukaudumiwa katika level unayotakaa maana watu wanakuwa wengi.
Tarehe 31 March ni siku ya mwisho kuwa umeshalipa ila unaweza kulipa muda wowote ule na hata kidogo kidogo mifumo ulioko siku hizi imeenda mbele tutumie fursa hii sasa tusije tukagombania goli mwishoni.
Ahsante
 
Nimesoma na kuelewa, ofisi zako zapatikana wapi?
 
Kwa kukurahisishia makadirio ya mwaka huu hata kama ujafanya hesabu zako pitia kwa haraka kujua kama mwaka jana ulitegeneza loss au faida na kwa asilimia ngapi kama imekuwa au kupungua kulinganisha na mwaka uliopita. Halafu angalia biashara yako kwa kipindi hiki cha miezi mitatu yaani December mpaka February biashara imefanyaje unaweza kwa kiasi fulani kuwa na namba halisia zaidi ya kukadiria. Filling njema ni vyema haya mambo ukafanya kabla ya deadlines za mwezi wa tatu mwishoni ambapo kuwanakuwa na foleni kubwa.
Ahsanteni
 
Naomba kwa mara nyingine tena niwakumbushie wiki hii inayoanza kesho itapendeza kama utaenda kupata makadirio yako ya kodi na kulipa au kwa kampuni kama utajikadiria na kulipa kabla foleni hazijawa kubwa. Fanya vitu kwa wakati ni vyema na ni nzuri sana
 
Back
Top Bottom