Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Hakuna kipindi kizuri kuweka mambo vizuri kwa wenye kampuni kama sasa kwasababu unaweza kutengeneza hizo hesabu ukapeleka na TRA ukapigwa faini ya kuchelewesha ukaomba msamaha uliotolewa na zile ambazo unatakiwa kulipa ukalipa mpaka June 2019. Hakika kwa aliye serious na kuclear mambo yake kuna hii golden opportunity iliyotolewa hakika ni vyema tukaitumia una mashaka ujuwi ufanyeje tuwasiliane tukusaidie kuweka mambo yako vizuri.

Shida ya wengi ni returns za nyuma hazijafanywa, pia hawana hesabu zilizo kaguliwa, sababu system inataka hizo nyaraka ndipo uupdate. au iko kivingine?
 
Muda wa kuupdate makampuni na Majina ya biashara ndio huu mwenye kutaka kusaidiwa hiyo tuwasiliane.
Ahsante
 
Vilevile kama kampuni yako inaugunduzi au umejikita kwenye mambo ambayo unaona unataka uwe na faida nayo usisahau kupata utaalamu kuhusu Copyright na Patents ni muhimu katika kuangalia biashara yako inakuwa kubwa na salama
halo kwenye copyright na patents nahitaji maelezo kidogo naijua but sio in deep sana
 
Kama unataka kufanya hii kitu ni vyema kupata mshauri wa sheria aliyebobea kwenye biashara inavitu vyake kidogo ni delicates huo ndio ushauri wangu.

halo kwenye copyright na patents nahitaji maelezo kidogo naijua but sio in deep sana
 
Katika fursa zinazojitokeza mara chache sana ni swala zima la kusamehewa penalti na fine. Kwa wale ambo walikuwawameazisha makampuni wakayaacha sasa unaweza kuyasafisha ukiangalia fursa ni wapi kwa kupata msamaha wa mambo kama kupeleka estimates na annual returns. Hakika siku zinakimbia lakini bado unanafasi yakuweka mambo yako vyema.
 
Kwasasa hili sio tatizo sana kama ujafanya hesabu za nyuma unaweza kufanya na kupeleka TRA na hii new TAX Amnesty ya interest na Penalty ni moja ya kitu cha msingi sana kimeshawahi kutokea Tanzania. Unaweza kutumia hii kuwa clean nakuweka mambo yako sawa. Ila sasa watu hawaitumii watusubiri wiki ya mwisho tutumie hii fursa sasa ikienda nachelea kufikiri kama itarudi siku za karibumi

Shida ya wengi ni returns za nyuma hazijafanywa, pia hawana hesabu zilizo kaguliwa, sababu system inataka hizo nyaraka ndipo uupdate. au iko kivingine?
 
Habarini za leo wanajamii, Leo nimeona kidogo nitumie fani yangu ya ushauri wa maswala ya biashara na uchumi niweke mambo muhimu katika uendeshaji wa biashara kwa nchi yetu pendwa ya Tanzania. Hapo miaka ya nyuma kulitokea na watu wengi waliosajili makampuni (LTD Companies) na wengine walienda mbali kidogo wakapata na Tax Indentification Number (TIN) kutoka mamlaka ya mapato (TRA). Sasa wanapotaka kuanza kufanya kazi wanakutana na penaty kubwa na fine. Ni Moja ya kushukuru Mungu sijui waheshimiwa walipita hapa katika budget ya mwaka huu wametoa TAX AMNESTY kwenye fine na penalty kwa kipindi cha miezi sita toka July 1 to Dec 31, Sasa Maelekezo yametoka na form ziko online na kwenye ofisi za TRA hii ni nia nzuri mno ya serikali na mimi natoa kongole kwa jambo hilo. Hii uliyo na rangi hii ni maongezo toka kwenye original post
Nikutokana na kadhia hiyo nataka kutoa ushauri kidogo kwa yeyote mwenye kampuni vitu hivi vitatu ni vya muhimu sana hata kama kampuni yako haiyafanya biashara.

Mosi hakikisha kila mwaka unapeleka majeresho yako (Annual returns) brela kwenye tarehe ile ambayo ulisajiliwa na hizi ni vyema ziambatane na hesabu zilizokaguliwa ( Audited financial). Kuanzia February 01, 2018 swala hili linafanyika kwenye mtandao wa Brela kama utahitaji msaada wa kufanya unaweza kuwasiliana nami PM .

Mbili hakikisha unapelewa returns zako TRA zile za provisional returns ambazo zinatakiwa kupelekwa kuanzia tarehe 01 January mwisho wake ni tarehe 31 March. Haya ni makisio unayotegemea kuwa nayo kwa kipindi cha mwaka huo. Na hapa ndio kumekuwa na mtihani kwa wale waliokuwa na kampuni lala kuwa mimi sijafanya biashara kabisa, Kama hutegemei kufanya bishara weka au fill Nil returns ( RETANI ZERO) inakubalika ila unajulikana na kutofanya hivyo inakarabisha fine. Na haya makadirio unaweza kuyabadilisha kwa wakati wowote hali yako ya biashara itakapobadilika. Hivyo hivyo kwenye VAT unatakiwa kupeleka returns zako za VAT kila mwezi hata kama ujafanya biashara kama umesajiliwa kwa VAT. Na Vile vile hakikisha kuwa mahesabu yako ( Audited Financial) zinawakilishwa kila mwaka kabla ya tarehe 30 June.

Tatu kodi zote nyinginezo kama withholding tax, PAYE na SDL zinapelekwa ila hapa utata umekuwa mkubwa kwenye withholding tax kwenye pango (rent) kwa mujibu wa sheria ni yule anayelipa ndio anatakiwa kukata na kupeleka TRA kwahiyo kama pango lako kwenye mkataba ni laki tano kwa mwezi na wewe umelipa miezi mitatu. Unatakiwa umpe mwenye nyumba 1,350,000/ halafu hiyo 150,000/ Unapeleka TRA, hivyo ndio sheria inavyotaka.
Naomba kuwakilisha
Hii mkuu imekaa vizuri
 
Muda wa kutoka clean ndio huu mkuu kama ulifanya makosa sasa unaweza kurekebisha ukasonga mbele mkuu


QUOTE="Raymond Thomas, post: 28141556, member: 418785"]Hii mkuu imekaa vizuri[/QUOTE]
 
Yaani natamani kila mwenye kampuuni kuchukua hii fursa serious ila naona watu wanakuwa kama hawaelewi nini serikali imeamua kufanya ili kuhakikisha watu wanabaki kufanya kazi. Tuchukulie hii fursa ya Tax Amnesty serious.
 
Mkuu ni namna gani nyingine ya kukupata tofauti na hapa JF maana mtandao huu umekuwa tia maji tia maji sana unaweza kubuma siku yoyote na watu wasijue namna ya kukupata
 
Naweza kupatikana kwa email info@franainvestment.com Karibu Ahsante

QUOTE="Mkaruka, post: 28147706, member: 123346"]Mkuu ni namna gani nyingine ya kukupata tofauti na hapa JF maana mtandao huu umekuwa tia maji tia maji sana unaweza kubuma siku yoyote na watu wasijue namna ya kukupata[/QUOTE]
 
Nikiangalia jinsi watu wachache sana wanochukua hii fursa ya kwenda kujaza kwa ajili ya tax Amnesty wakati watu wenye shida ni wengi nashangaa tu. Yaani sasa hivi unahudumiwa vizuri sasa sijui ni ile watu wanasubiri dakika za mejeruhi wanakuja na mambo lukuki au vipi.
Ahsante
 
Tunaingia third Quater kesho katika mwezi ambao majukumu mengi ya kodi yanasahaulika huu umo kwenye list kwahiyo usijisahau ukakutana na penalty. Moja kwa kuwa kuna robo ya mwaka wa makadirio tafadhali hakikisha unapeleka. Na ni muda mzuri pia kwa wewe uliyejikadiria kujitazama kama ubadilishe makadirio yako kama yatakuwa juu au chini
 
Tunaingia third Quater kesho katika mwezi ambao majukumu mengi ya kodi yanasahaulika huu umo kwenye list kwahiyo usijisahau ukakutana na penalty. Moja kwa kuwa kuna robo ya mwaka wa makadirio tafadhali hakikisha unapeleka. Na ni muda mzuri pia kwa wewe uliyejikadiria kujitazama kama ubadilishe makadirio yako kama yatakuwa juu au chini
ubarikiwe sanaaaa
 
Vile vile katika mwezi huu wa Tisa ambao tunaelekea kufikia robo tatu mwaka ni vyema vilevile kuona kama unaweza kupata picha yako ya kikodi yaani tax planning kujua kwa mwaka huu utalipa kodi kiasi gani kama mapato yako yatakuwa hivyo na vile vile ni muda wa kuadjust estimate ili usije ukapigwa penalty ya kuunderestimate mapato yako
 
Habari za asubuhi siku zinakimbia kwa wale ambao wanatakiwa kuupdates online Brela ni muhimu sana kufanya hivyo sasa.
 
Katika fursa zinazojitokeza mara chache sana ni swala zima la kusamehewa penalti na fine. Kwa wale ambo walikuwawameazisha makampuni wakayaacha sasa unaweza kuyasafisha ukiangalia fursa ni wapi kwa kupata msamaha wa mambo kama kupeleka estimates na annual returns. Hakika siku zinakimbia lakini bado unanafasi yakuweka mambo yako vyema.
Kama ulianzisha ukaacha kufanya kazi hata mwaka bila kupeleka taarifa kuna penati au ndio msamaha kunausika?
 
Back
Top Bottom