Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa kampuni

Ni kweli kama ujapeleka penalty zipo ila hii amnesty ni lazima uombe ukionyesha hiyo penalty na fine ni ipi.

QUOTE="dickchiller, post: 28279058, member: 83999"]Kama ulianzisha ukaacha kufanya kazi hata mwaka bila kupeleka taarifa kuna penati au ndio msamaha kunausika?[/QUOTE]
 
Kama repoti ya world bank imetoka tunaendelea vizuri kiuchumi. Tujenge nchi yetu nzuri Tanzania
 
Mmoja ya issue kubwa inaonekana katika kuendesha biashara zetu ni kuzijengea mifumo ambayo itazifanya zifanye kazi hata kama wamiliki hawapo. Imeonekana kuwa jambo gumu kidogo kwa biashara nyinigi. Ushauri wangu anza kwa kuajiri watu makini ili biashara yako ikuwe ni ukweli usiopingika kwamba kuna wakati lazima utengeneze mifumo ili biashara ikuwe.
 
Habari zimebaki siku chache sana za kutumia msamaha wa Penalty na Interest jamii tufanye jambo
 
Kwa mfano nimesajili kampuni brela lakini haijafanya kazi(sijaanza biashara )mpaka mwaka umepita,je nitapigwa fine na brela ?

Kwa kuongezea ni kwamba kampuni itafikia tamati kisheria ikiwa haijaanza kufanya biashara mwaka mmoja tangu siku ya kusajiliwa. Hii ni kutokana na kifungu namba 279(1)(b) cha Companies Act.
279. (1) A company may be wound up by the court if:
(b) the company does not commence its business within a year from
its incorporation or suspends its business for a whole year;
 
Bado najiuliza hivi kweli wenye makampuni na wafanyabiashara wameelewa kweli kitu kikubwa ambacho serikali wametoa kuhusu kusamehe penaty na interest mwamko bado ni mdogo sana shime tujitokeze kuchukua hii fursa
 
SDL utalipa tu mpaka pale utakapokuwa na wafanyakazi wanne na zaidi hayo ndio matakwa ya sheria. Kwahiyo kama mko wawili tu hamna haya ya SDL. Na rate ya mwaka huu ni 4.5% Ahsante

Nini maana ya SDL? Please help
 
Nini maana ya SDL? Please help
SDLKirefu chake ni Skill Development Levy. Ni tozo inayolipwa kwa ajili ya kuendeleza watu ndio maana kila mwajiri mwenye kuajiri watu 4 na kuendelea anatakiwa kupeleka. Hii hela inaenda VETA kwaajili ya kusaidia watu wetu.
 
SDLKirefu chake ni Skill Development Levy. Ni tozo inayolipwa kwa ajili ya kuendeleza watu ndio maana kila mwajiri mwenye kuajiri watu 4 na kuendelea anatakiwa kupeleka. Hii hela inaenda VETA kwaajili ya kusaidia watu wetu.

Okay Asante sana. So mpaka uajiri watu zaidi ya wanne.
 
Kaka barikiwa sana. Mimi ni mhanga wa kodi, returns za VAT nazifanya vema, ila cash sijapeleka muda, hata makadirio yangu.. nataka kutumia hii nafasi ya msamaha nione nilipo....then nihakikishe nafanya yote niapaswayo hata biashara ikienda kombo.
 
Watu niwanne na kuendelea na sio zaidi ya wanne. Maana ukiweka hiyo itakuwa 5 na kuendelea ya zaidi ya wanne.
QUOTE="Jombii, post: 28986161, member: 30759"]Okay Asante sana. So mpaka uajiri watu zaidi ya wanne.[/QUOTE]
 
Tukiwa tunaelekea wiki ya mwisho kabisa ya kuchukua fursa kwa makampuni kusamehewa Riba na Adhabu naomba wadau mchukue fursa hii inaweza isirudi siku za karibuni. Nawatakiwa wiki njema
 
Tukiwa tunaelekea wiki ya mwisho kabisa ya kuchukua fursa kwa makampuni kusamehewa Riba na Adhabu naomba wadau mchukue fursa hii inaweza isirudi siku za karibuni. Nawatakiwa wiki njema
Habari mkuu nataka kusajili either kampuni au jina la bishara.
1. Nini tofauti ya hivyo na zinatumika vipi.
2. Sina partner ni Mimi mwenyewe ( sole proprietor) documents gani niwe nazo.
3.gharama za kusajili kampuni ni bei gani na jina la biashara ni bei gani.
4. Any info kujazia hapo.
Ahsante
 
Habarini za leo wanajamii,
Leo nimeona kidogo nitumie fani yangu ya ushauri wa maswala ya biashara na uchumi niweke mambo muhimu katika uendeshaji wa biashara kwa nchi yetu pendwa ya Tanzania.

Hapo miaka ya nyuma kulitokea na watu wengi waliosajili makampuni (LTD Companies) na wengine walienda mbali kidogo wakapata na Tax Indentification Number (TIN) kutoka mamlaka ya mapato (TRA). Sasa wanapotaka kuanza kufanya kazi wanakutana na penaty kubwa na fine.

Ni Moja ya kushukuru Mungu sijui waheshimiwa walipita hapa katika budget ya mwaka huu wametoa TAX AMNESTY kwenye fine na penalty kwa kipindi cha miezi sita toka July 1 to Dec 31, Sasa Maelekezo yametoka na form ziko online na kwenye ofisi za TRA hii ni nia nzuri mno ya serikali na mimi natoa kongole kwa jambo hilo. Hii uliyo na rangi hii ni maongezo toka kwenye original post

Ni kutokana na kadhia hiyo nataka kutoa ushauri kidogo kwa yeyote mwenye kampuni vitu hivi vitatu ni vya muhimu sana hata kama kampuni yako haiyafanya biashara.

Mosi hakikisha kila mwaka unapeleka majeresho yako (Annual returns) brela kwenye tarehe ile ambayo ulisajiliwa na hizi ni vyema ziambatane na hesabu zilizokaguliwa ( Audited financial). Kuanzia February 01, 2018 swala hili linafanyika kwenye mtandao wa Brela kama utahitaji msaada wa kufanya unaweza kuwasiliana nami PM .

Mbili hakikisha unapelewa returns zako TRA zile za provisional returns ambazo zinatakiwa kupelekwa kuanzia tarehe 01 January mwisho wake ni tarehe 31 March. Haya ni makisio unayotegemea kuwa nayo kwa kipindi cha mwaka huo. Na hapa ndio kumekuwa na mtihani kwa wale waliokuwa na kampuni lala kuwa mimi sijafanya biashara kabisa, Kama hutegemei kufanya bishara weka au fill Nil returns ( RETANI ZERO) inakubalika ila unajulikana na kutofanya hivyo inakarabisha fine.

Na haya makadirio unaweza kuyabadilisha kwa wakati wowote hali yako ya biashara itakapobadilika. Hivyo hivyo kwenye VAT unatakiwa kupeleka returns zako za VAT kila mwezi hata kama ujafanya biashara kama umesajiliwa kwa VAT. Na Vile vile hakikisha kuwa mahesabu yako ( Audited Financial) zinawakilishwa kila mwaka kabla ya tarehe 30 June.

Tatu kodi zote nyinginezo kama withholding tax, PAYE na SDL zinapelekwa ila hapa utata umekuwa mkubwa kwenye withholding tax kwenye pango (rent) kwa mujibu wa sheria ni yule anayelipa ndio anatakiwa kukata na kupeleka TRA kwahiyo kama pango lako kwenye mkataba ni laki tano kwa mwezi na wewe umelipa miezi mitatu. Unatakiwa umpe mwenye nyumba 1,350,000/ halafu hiyo 150,000/ Unapeleka TRA, hivyo ndio sheria inavyotaka.


Naomba kuwakilisha
Mkuu hili wazo ni pana sana. Kwa manufaa ya wengine ningeomba mjadala huu uendelee hapa hapa. Swala la kodi ni swala pana na linatutesa wengi mno, ningependa uendelee kudadavua hapa hapa.
 
Kuna jamaa alikuwa anajsifia kuwa wao wanakampuni afu hakuna walichokuwa wanakfanya ingawaje wamesajili kampuni,nahis sahv wanaisoma namba
 
Dah Nina kampuni mfukoni yapata miaka sita Sasa, nilihofu Sana kwenda brela kuisajili, kwa sabb za mwenendo was biashara nchini. Mkuu biashara kufa au kuimarika inaeza tegemea na utawala unaoongoza dola wakat huo? Na je ktk indicator za uchumi kuimarika, kudorola au kudumaa ..tz Sasa hivi uchumi wetu ukoje?
 
Back
Top Bottom