MAMBO NAYOYA EXPERIENCE BAADA YA KUMILIKI GARI

MAMBO NAYOYA EXPERIENCE BAADA YA KUMILIKI GARI

Hahahaha,nina waswas huu uzi umetunga tu maana inawezekana hujui mafuta ya elfu 5 ni kiasi gani
 
Hahahaha,nina waswas huu uzi umetunga tu maana inawezekana hujui mafuta ya elfu 5 ni kiasi gani
 
Hayo mafuta utakuwa unachanganya na maji wewe! Ndio maana kila siku unaenda kuliosha hilo gari
 
Laki kuosha,parking yako shi ngapi kwa mwezi
 
Hamkumwelewa mleta mada..

Jamaa kasema huwa kwa siku mafuta yanayotumika ni sh 5000, sio kwamba ndo anaenda sheli kuweka mafuta!!!
 
5000 imekuwa pikipiki? Heee
Mimi namiliki RAV 4 Old Model, budget yangu ya mafuta ni TZS 120,000 kwa mwenzi. Najaza TZS 60,000 mwanzoni mwa mwezi na TZS 60,000 nyingine katikati ya mwezi. Kwa matumizi ya kwenda kazini na ofisini yananitosha.

Huyo wa TZS 5,000 kwa siku bado iko juu kulinganisha na bajeti yangu. Anyway nyie wa Dar es Salama mnaishi mno mbali na eneo la kazi ndio maana mnaona TZS 5,000 haitoshi
 
Duuh umeamua kuongeza matumizi wakati huu wa serikali awamu ya 5 ,pole sana siye tumeishayazoea .
 
Mimi namiliki RAV 4 Old Model, budget yangu ya mafuta ni TZS 120,000 kwa mwenzi. Najaza TZS 60,000 mwanzoni mwa mwezi na TZS 60,000 nyingine katikati ya mwezi. Kwa matumizi ya kwenda kazini na ofisini yananitosha.

Huyo wa TZS 5,000 kwa siku bado iko juu kulinganisha na bajeti yangu. Anyway nyie wa Dar es Salama mnaishi mno mbali na eneo la kazi ndio maana mnaona TZS 5,000 haitoshi
Dar watu wanaendesha over 60 km kila siku ya kazi mkuu
 
Kama ulivyosema ktk uzi wako mkuu haters lazima waonekane, bahati mzuri ulisema tutawaona hapa na kweli tunawaona.......

Mafuta ya 5000 (2.5Ltr) ni mengi kama upo mkoani na kwa ratiba ya kila siku ya kazini na kwenda bar au beach week-end, hata ukimiliki Rav 4 ya 4-Cylinder yenye 1998cC inayokula 1L kwa 8km full AC bado uko poa tu,

Tulichokuelewa ni kwamba umetoa hesabu ya mzunguko wako wa kila siku ukiacha ile ya dharula pale inapojitokeza umuhimu au Luxury ya makusudi........

Kumiliki gari tu ni hatua mzuri, waliotengeneza Starlet, Ist, Passo, swift n.k wana akili kuliko wengi tunaoropoka hapa.......[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hongera kwa kununua gari... Uendeshe vizuri, kitunze kidumu usije rudi kupanda dala dala... Epuka ulevi wakati unaendesha... Pia usiwe mvivu kufanya service...
 
Siku zote hapa bongo Ukimiliki gari tu iwe starlet, swift, passo au ist hadhi yako lazima itapanda tu kwa jamii kwa sababu wengi hawana magari ingawa ukiwa sehemu kama dar unaweza kudhani kila mtu anamiliki gari.

Watu ambao wanaweza kukudharau kwa kumiliki gari mdogo ni wale ambao wana magari makubwa au ya gharama zaidi yako (ambao ni wachache) ila sio wale ambao hawana magari (ambao ndio wengi)

Hata humu jamii forum tusio na magari ni wengi kuliko nyie wenye magari bila kujari ukubwa wa gari.

Kumiliki gari ndogo ingelikuwa rahisi basi kila familia ingelikuwa na kagari angalau kamoja maana kibongo bongo kila familia isiyo na gari ni lazima ins tatizo la uhakika la usafiri [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji13]
 
Back
Top Bottom