#COVID19 Mambo niliyoyaona baada ya kupata chanjo leo

#COVID19 Mambo niliyoyaona baada ya kupata chanjo leo

Leo nimechanjwa katika mji mmojawapo wa wilaya. Nilifanya booking online na tarehe yangu niliyochagua ilikuwa jana bahati mbaya jana hawakufungua. Nilichokiona ni:
  1. Pamoja na kueleza kuwa nilikuwa na booking online lakini hiyo haikuwa na uzito ila nilipewa fomu ya kujaza.
  2. Mtumishi alikuwa mmoja huku akifanya kazi ya usajili na kuchanja na kuna wakati alizidiwa.
  3. Makundi maalum ya watu walioainishwa katika awamu hii hayajawa wazi sana kwani nimeshuhuida mtu wa umri chini ya 40 na ambaye hana ugonjwa wowote akiomba achanjwe (Picha za Jokate zimevuruga mambo)
  4. Hapakuwa na faragha na kila mtu alikuwa akiulizwa unatumia dawa yoyote au una ugonjwa wowote
  5. Mwamko ni mkubwa na vituo vya kuchanjia vijipange vizuri.
  6. Pamoja na kuchanja lakini sina kitambulisho chochote kuthibitisha kuwa nimechanja
  7. Kwa kuwa vitambulisho vya uraia na liseni za udereva zinatumika ingefaa pawe na app ambayo ingerahisisha kwani kwa ujazaji ule nina mashaka kuwa makosa yatakuwa mengi na data entry itakuwa na shida.
Ww ndio basi tena tushakupoteza
 
Back
Top Bottom