RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
đź“–MHADHARA WA 13
Hello mjasiriamali mwenzangu. Naomba leo nishee mambo sita (6) muhimu ambayo ukiyazingatia hutopoteza wateja. Kama unataka kufungua biashara, au tayari umefungua biashara zingatia mambo yafuatayo;
1. UCHESHI NA MATUMIZI YA LUGHA
Jaribu kuwa mcheshi kwa wateja hata kama wewe ni mpole. Pia uwe na lugha nzuri ikiwezekana yenye ushawishi. Stress za ndoa usizipeleke kwenye biashara yako. Epuka mambo yafuatayo:
(a) Usiendelee kuchezea simu wakati unapomkaribisha au kumhudumia mteja.
(b) Mkaribishe tena mteja wako pindi anapoondoka, mwambie; "karibu tena".
(c) Usiwe na lugha fupi. Kwa mfano unauza nywele bandia, mteja ameuliza nywele ambayo huna, usimjibu "HAKUNA" halafu basi. Jaribu kumshawishi zaidi mwambie "Hiyo nywele sina lakini hata nywele fulani ni nzuri ukisuka itakupendeza" - Yaani jaribu kumshawishi kwenye bidhaa uliyokuwa nayo.
2. MUDA WA KUSUBIRI HUDUMA
Hakikisha mteja wako unampatia huduma kwa haraka. Usimkarishe mteja wako kwa muda mrefu. Usifurahie kuwaona wateja wengi wanakusubiri wewe. Kama unaona unazidiwa na wateja tafuta mtu (mfanyakazi) wa kukusaidia. Pia Hakikisha unakuwa na chenji (hela ndogo ndogo) za kutosha kuliko kila mara unaacha duka unakwenda kuomba chenji kwa jirani. Wateja wengi hawapendi kusubirishwa.
3. USIKOSE KUWEKA BIDHAA INAYOPENDWA
Mara kwa mara wateja wakiwa wanaulizia bidhaa fulani maana yake ni kwamba umezungukwa na wateja wanaopenda hiyo bidhaa, haraka sana weka hiyo bidhaa kama inaendana na aina ya biashara yako. Bila shaka wateja watakuhama pindi wanapouliza bidhaa moja kila siku bila mafanikio. Ngoja nikupe siri; Mtu akiona vocha za simu zinaulizwa sana dukani kwake, anaweka hata kama hazina faida akiamini kwamba atakayefuata hiyo voucher anaweza kununua na bidhaa nyingine hata kama hakupanga kununua.
4. MANDHARI YA ENEO/CHUMBA CHA BIASHARA
Hakikisha eneo/chumba chako cha biashara ni pakubwa, chenye mwanga wa kutosha, na mlango mpana. Hata kama huna mtaji wa kujaza chumba lakini pendelea chumba kikubwa. Ni moja ya kitu kinachowavutia sana wateja.
5. TUNZA WATEJA/USIWAPOTEZE WATEJA MUHIMU
Usikubali kuwa na mambo ambayo yatawakwaza wateja wako muhimu hatimaye kuwapoteza. Wateja muhimu ni wale ambao hawakosi kuja kukuungisha. Kwa mfano wale Mamantilie, Vibanda vya kahawa, maduka ya nywele bandia, n.k, huwa wanakuwa na wateja wao wa kila siku - Hakikisha huwapotezi hao wateja, sikiliza maoni yao na uyafanyie kazi. Mteja muhimu anaweza kukuletea wateja wengi, lakini pia anaweza kuwapoteza wateja wengine.
6. EPUKA KUKAA MBALI NA BIASHARA YAKO
Hii ni kwa wale ambao wanapenda kuacha milango yao ya biashara kisha wanakwenda kupiga stori kwa jirani. Mbaya zaidi mteja anafika hapo anaita mara kadhaa haoni mtu. Hii tabia inawachukiza sana wateja.
RIGHT MARKER
Mbezi Louis, DSM
Septemba 23, 2024.