Mambo tano ya kujiuliza kabla ya kuchukua fomu ya kugombea cheo cha kisiasa

Mambo tano ya kujiuliza kabla ya kuchukua fomu ya kugombea cheo cha kisiasa

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
15,923
Reaction score
40,246
Ikiwa kweli una utimamu wa akili, madaraka ya kisiasa siyo jambo la kukimbilia kama hauna dhamira ya dhati ya kutumikia jamii yako.

Uongozi ni kuacha alama, kuwaongoza watu waweze kufikia mafanikio wanayoyatamani ya kiuchumi na kijamii

KIongozi atadaiwa mengi na atapimwa kwa mengi, hivyo uongozi unaweza kukujenga au kukubomoa, kupandisha au kushusha heshima yako

Kuwania nafasi mbali mbali za kisiasa kusiwe ni fasheni au chaka la kutafutia riziki au la kufichia uovu au la kujinufaisha kibiashara.

Watia nia ya uongozi wawe watu wazalendo, wenye uweledi na nia ya dhati kuwasidia wananchi

Kwa muktadha huo, ninatoa mambo matano ya kuzingatia kabla ya kuchukua fomu:

1. Uwe ni mtu uliyefanikiwa kiuchumi usiwe mtu njaa njaa;
2. Uwe ni mtu mwenye uzalendo usiotiliwa shaka(machawa waachane na hii biashara)
3. Uwe ni mtu unayejua matatizo ya wananchi wako na unao mpango mkakati wa kwenda kuyatatua:
4. Uwe ni mtu mwenye haiba nzuri, jamii inaweza kuchangamana na wewe; na
5. Uwe na plan B, pale utakapo kosa uongozi wa kisiasa bado uendelee kusaidia jamii yako itatue matatizo uliyoyaona

Kama unahisi una mengine ya kuwahasa watia nia, karibu
 
Back
Top Bottom