Mambo unayoweza kuyafanya kwa fedha kiasi cha Laki tano

Kwa haraka unaweza kuingia mkenge ukatoa hiyo hela ama ukakodi hilo shamba.. Lakini kuna mengi hapo yanakusubiri
Nguvu kazi
Madawa
Mahitaji mengine
Mahitaji yako ya kila siku
Gharama za kuvuna na kuhifadhi
Gharama za usafiri Mk
Kama unadhani ni laki 5 tuu. [emoji144][emoji144]
 
Ukweli. Watu wanazanai Kilimo au Ijasirimali kwa ujimla ni rahisi. Hapana kuna kazi kubwa sana.

Sio kazi ya kitoto kamwe
 
Unaweza anza na Laki 5 kweli au hata chini ya hapo kabisa but ni Safari ndefu sana ambayo inaweza kuluchukua miaka.

Kuanza na laki 5 kweli ni possible ila sio kirahisi na sio swala la leo leo. Kwamba baada ya mwaka mmoja au miwili uwe una Drive. Hapana.
 
Ameandika MASANJA MKANDAMIZAJI

AKILI YAKO UTAJIRI WAKO:

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.
Hii laki 5 haitoshi kulima tikiti Ekari 13 tuache uongo.
  1. Ukodi shamba ekari
  2. Ulisafishe
  3. Ulime
  4. Ununue Mbegu
  5. Ununue madawa na mbolea
  6. Ulipe wafanya kazi
  7. Matumizi yako na nauli

Mimi nilitumia 845,000 kwa heka moja hapo nilikuwa sijafikia hatua ya palizi. Iweje Ekari 13 utumie laki 5 tu??

Atakaeamini hii ni mtu ambae hajawahi kufanya kilimo, HAYA MAMBO SIO MARAHISI kama tunavyofikiria
 
watu wanasema laki tano haitoshi na wanatoa gharama ila mtu akikupa dondoo we ni ni jukumu lako kuona mtu kakapa fursa na kakupa wazo ni swala la kulifanyia utafiti uone lakitano inatosha kufanya nini ili upate kitu.

Maneno yake yamenifurahisha na yamenitia nguvu katika malengo na harakati zangu
 
mkuu yeye katoa wazo au mawazo ukiona ni fursa hutoenda na laki lazima ufanye utafiti, ka utajitoa uende kulima pasipo utafiti utakuwa ulopungukiwa. hii tunaita illustration
 
Ndio wale wale wanafikiri Faida lazima iwe pesa "toungible material"

kwa mawazo hayo hayo,atakae amua kuingia shambani akalima,hata kama akipoteza laki 5 yote

akirudi round two ana uhakika wa kurudisha ile laki 5 na zaidi,tatizo letu watanzania (sio wavumilivu)

mtu unatiririsha mlolongo mzimaaaaaa sjui madawa sjui nini sjui nini,hivi mmeambiwa vyote lazima mfanye?

Mimi nilianza lima mboga mboga bila kutia dawa yoyote zaidi ya kitalu changu na mbegu na mboga zilistawi na hela nilipiga

hela huna mtaji mdogo halafu unataka ulime kisasa (akili zenu za wapi nyie)

laki 5 kilimo inatosha kwa mwanzo vizuri kabisa,tusivunjane moyo hapa.

Mnaojitia wazoefu huo uzoefu mngeupata wapi kama sio kuamua ingia huko kilimoni?

au huo uzoefu mlitegemea nani angekuletea bure bure? Aseee kuna watu mnajua kukatisha wengine tamaa sana

Nasema HIVIIIIII

kijana kama una laki 5 tafuta Pori kalime achana na hao wakatisha watu tamaaaaa..Yamewashinda hao hawana lolote.
 
tatizo tunapenda kushinda insta ila mahali pa kuumiza kichwa hatutaki kabisa ndo maana watu tumemdondokea kuwa laki 5 haitoshi nani anaweza kuja kukupa taarifa zote muhimu A to B bureee? mkuu nimekuelewa sanaa, kufanya ni tofauti na kutokufanya
 


Andika yako tu inaonekana hujawah hata kulima!..binafsi nidanganywe kwingine sio kilimo!..ukilima mchicha unaishia kuuza fungu chache tu majority wana bustani nyumban mwao.eish!
 
Andika yako tu inaonekana hujawah hata kulima!..binafsi nidanganywe kwingine sio kilimo!..ukilima mchicha unaishia kuuza fungu chache tu majority wana bustani nyumban mwao.eish!
yawezekana unanijua kuliko nijijuavyo na yawezekana kweli sijawahi kulima kama usemavyo

wewe ulie beep kilimo na kukimbia upo humu kutisha watu umelima,haukua na experience na kilimo upo kufata pesa,naonaga sana michango yako negative kwenye kilimo,hunaga jipya Unachosemaga ni eti "mtu unapotezaa milioni then unapata faida ya laki"

kwako unaonaga hela ndio mafanikio na ndio mana upo humu kudanganya watu kujitia unakijua kilimo kuliko wengine wote,eti nidanganywe kilimo sio kwingine umelima mazao mangapi wewe?? usitake jitia expert wa kilimo hapaaa huna lolote,umezoea hela za madini upepete mchanga huko upate vi mawe viwili ukauze ndio kwako unaona hela.

wewe akili yako ipo kwenye "pesa za haraka haraka" kilimo haitaki hayo mawenge yako uliyonayo,unakazi kutoa mawazo as if umelma kilimo miaka mi 5, huna lolote ujualo kwenye kilimo,kama ulilima Nyanya usifikiri kila mkulima wa nyanya anapata hasara,wewe na mawenge yako na kutokua na connection ndio kumekufanya uangukie pua.

Ukipenda shortcut usitegemee kuipata kwenye kilimo,baki huko huko pepeta mchanga tafuta punje za madili,uza michanga,maana ndio passion yako ilipo na sio kwenye kilimo na uache kujitia unajua kilimo saaanaaaa as if wewe ndio umepataga hasara na klimo kuliko wote waliopita,

Huna ujualo kuhusu kilimo,niishie hapa.
 
Laki 5? Ngoja niendelee zangu kubeti tu.
 


😅😅mbona povu mkuu!pambana unapotaka utafika, !!
 
You have a point mkuu, shida watu kusikia hio laki 5 wanaanza kutengeneza imagination kuhusu production kua lazima iwe modern and large scale agriculture ukiwa mtafutaji lazima uwe tayari kutembea sehemu tofauti tofauti, na Tanzania hii ni kubwa sana katika zunguka zunguka kuna sehemu niliwahi fika kuna watu wa vijijini wana mashamba mengi balaa halafu wametanguliza pesa mbele kupita kiasi kana kwamba hata elfu 30 unaweza kupata hekari moja kwa kukodi,, then managament zote za shambani hata laki 3 haifiki ukiifanya local, I mean hapa utumie samadi, spray ukiwa na pampu hata mwenyewe unaifanya + dawa zake unatumia hata hizi za kuogeshea ng'ombe chupa moja around 5k,, issue za palizi pia ni cheap within hio laki tano inaweza kutosha na kama itaongezeka haiwezi kuzidi laki sita (japo kwa baadhi ya maeneo niliyotembe tembea haiwezi kufika kote huko)

Always utamu wa ngoma zama ndani ucheze, muhimu ni kuanza kidogo kidogo sio kisa Masanja analima ekari 100 za mpunga basi na wewe lazima ulime ekari mia hapana, even knowledge is expensive kama katika hio laki 5 utalima na ukapata hasara nina uhakika kabisa kuna vitu vingi utakua umejifunza kuliko usingefanya utekelezaji wowote.

Sio upande wa kilimo tu kwenye jambo lolote hakuna siku itatoke tu paah ukapata mtaji kwa100% ndio uanze kutekeleza ndoto zako kwa mazingira yetu kibongo bongo ni ngumu sana, siandiki hapa ili kuonekana mjuaji hapana ila nina uhakika kabisa hio laki tano ukiamua kulima Tanzania hii kuna sehemu unapata kabisa eneo (ekari 1 kama kima cha chini) ambayo haizidi hata elfu 50 (around 30-40+)
 
😅😅mbona povu mkuu!pambana unapotaka utafika, !!
hii ndio point

usikatishe wengine tamaa kwa sababu tu ulifeli ukashindwa

huwezi jua mwenzako atafanyaje na akatoka kupitia hicho unachomkatisha nacho tamaa

sio kwasababu unaona unachofanya kina faida ukafikiri kila mtu atafanya hicho

jiulize unasema kilimo hasara ila watu wanalima na wana ushuhuda nacho kwa kilivyowatoa

unakazanaje kukomalia eti mtu asikudanganye chochote kwenye kilimo,wewe sema ulifeli

then tulia zako, watu hawashuhudiii Failures zao watu tunashuhudia Ushindi Tu ili alie chini ainuke,apate nguvu ya kusimama

sasa kila mtu akisema changamoto anazopitia kwenye kile anafanya unafikir nani atakua "mjasiriamali"

Jifunze kukaaa kimya kwa mambo uliyojaribu kufanya yakakushinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…