Mambo usiyoyajua kuhusu msitu wa Amazon

Mambo usiyoyajua kuhusu msitu wa Amazon

(....Usipite bila Kusoma......)

1: Msitu wa Amazon ndio msitu mkubwa zaidi duniani unaopatikana huko America kusini.

2: kama ulifikiri msitu huu unapatikana Brazil pekee jibu ni hapana msitu huu umegawanyika katika nchi tisa nchi hizo ni Blazil 60% peru 13% colombia 10% na mataifa mengine kama Venezuela, Ecuador, bolvia, guyana, suriname na France guiana.

3: Msitu huu una eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,500,000 ( Milioni 5) yani kwa ukubwa huu nchi ya TANZANIA iingie mara 6 kwenye msitu huo.

4: kwa mujibu wa wanasayansi wa mimea msitu wa Amazon una umri wa miaka zaidi ya million 55

5: Msitu wa Amazon unakadiriwa kuwa na miti billion 400 na aina mbalimbali za miti zaidi ya 160,000 pia kuna miti ya matunda tofauti tofauti elfu tatu katika msitu huo.

6: Mchanga wa jangwa la sahara hupeperushwa na upepo hupita juu ya bahari Atlantic hadi katika msitu wa amazon ambako hurutubisha katika msitu huo.

7: katika msitu wa amazon kuna mto umekatisha mto huo unaitwa mto amazon huu ndio mtu mkubwa zaidi duniani na unaingiza maji baharini mara 5 ya mito mingine maajabu ya mto huu kuna muda haueleweki kuna kipindi unapeleka maji kinyume badala ya maji kwenda mashariki yana kuwa yana toka mashariki kwenda magharibi.

8: Asilimia 20% ya oxygen iliyopo dunia inatengenezwa katika msitu wa amazon👏 acha hili pia zaidi ya asilimia 70% ya madawa ya kisasa yana tengenezwa kwa kutumia miti inayo patikana ndani ya msitu wa amazon. Ndio maana unaitwa mapafu ya dunia.

9: katika msitu wa amazon kuna makabila zaidi ya 50 yana ishi hapo watu wameishi kwa maelfu ya miaka iliyo pita lakini watu hao wamekuja kuonekana miaka ya hivi karibuni.

10: Green anaconda
Hawa ndio nyoka wakubwa zaidi duniani kwa sasa ni aina ya nyoka wanao patikana msitu wa amazon pekee wana rangi ya kijani na madoa meusi.

11: poison dork frog
Ni aina ya vyura wanaopatikana msitu wa amazon pekee wana sumu kali katika migongo yao ..

C&P
Amazing Amazon
 
The fact kwamba Tanzania inaingia mara 6,imenifanya nikatafakari dkk kadhaa.

Ndio sababu kipindi umeshika moto likawa swala la lazima kila nchi duniani yenye uwezo kwenda kushiriki kuzima moto.
Mwenyewe imenifikirisha kwa kiasi chake, safari yangu ndefu niliwahi kusafiri ni dar kwenda songea, kwa umbali ule Tanzania ni kubwa vya kutosha, sasa iingie sehemu mara sita !
 
Nchi ya Amerika Kusini, ambako viumbe hai vya Andes hukutana na vile vya Amazon, inapoteza utajiri mkubwa wa asili wa kilomita za mraba 1,500 kila mwaka, hasa katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa chini ya udhibiti wa waasi.
Hakuna nchi inaitwa Amerika Kusini, sio kila kitu unacopy na kupaste tu uwe unashughulisha ubongo mzee mjuaji.
 
Nimeipenda namba sita, na hiyo namba 11 imenikumbusha kipande cha movie ya Apocalypto hao vyura wenye sumu migongoni.
 
Hebu toa maelezo zaidi kwa namba 6. Nataka nijuwe mchanga wa jangwa la Sahara unasafiri vipi juu ya Atlantic ocean Mshana Jr
Huo mchanga utakuwa unasafirishwa kwa small particles kwa muendelezo, so unakuta kwa siku kiasi cha hizo particles kutoka jangwani kwenda baharini kinakuwa kingi, ukipiga hesabu ya miaka yote iliyopita utaona huo mchanga toka jangwani kwenda msitu wa amazon kinakuwa kingi zaidi.
 
Hiyo namba 7 sasa!


Vipi kaka mkubwa kuhusu stori za makomandoo na majasusi wa dunia kupitishwa huko kwa ajili ya mafunzo jambo hili lina ukweli
Ni ngumu kuhakiki japo hilo jambo linasemwa sana
 
Alafu atakuja mtu atasema hayo yametokea kwa bahati tu hakuna aliyefanya
 
Vipi zile Almasi za msitu wa Congo zipo kweli na masokwe mizimu?!
 
Anaconda ndo nyoka wakubwa zaidi duniani? Kwa kutumia kipimo kipi? Urefu? Uzito? Mzingo?

Kwa sababu reticulated pythons may have something to say about that….
 
Back
Top Bottom