Mambo usiyoyajua kuhusu nyota Jua na mwisho wa sayari Dunia

View attachment 356025

Jua ndio kitu pekee ambacho kiko katikati ya mfumo wa jua. Jua ni 99.86% ya uzito(mass) wa mfumo wa jua.

Kimsingi jua ni mkusanyiko wa hydrogen na helium, 74.49% hydrogen na 23.8% helium.

Joto la kitovu cha jua linakadiriwa kufikia nyuzi joto milioni 15, wakati tabaka la nje lina nyuzi joto 5500.

Jua huchukua mwezi mmoja kumaliza mzunguko wake katika mhimili wake, na hii inakadiriwa tu na sababu kubwa umbo la jua ni kama mpira wa plasma. Kutokana na umbile lake, mzunguko hutofatiana tabaka na tabaka.

Mathalani, sehemu ya tabaka la nje karibu na ikweta yake, humaliza mzunguko wake kwa siku 25.4 wakati karibu na "poles" huchukua siku 36. Imethibitika tabaka la ndani la jua huzunguka sana kuzidi tabaka la nje.

Wastani wa umbali kati ya jua na dunia ni km milioni 150 na mwanga husafiri kwa spidi ya km 300,000 kwa sekunde, ukiwa mwanahisabati na ukikokotoa utagundua mwanga wa jua hutumia dakika 8 kusafiri kutoka katika jua na kutufikia duniani.

Cha kufurahisha hapa, hii nishati hutumia dakika nane kutufikia duniani, lakini pia hutumia mamilioni ya miaka kusafiri kutoka katika kitovu cha jua na kufika katika tabaka la nje la jua(ambapo kutoka hapo ndio hutumia dakika 8 kufika duniani)

Hii ina maanisha nini? ina maanisha mwanga wa jua unao uona sasa si wasasa bali ulianza safari yake hadi kukufukia hapo ulipo mamilioni ya miaka.

Katikati ya kitovu cha jua asilimia kubwa ya nishati ya jua huzalishwa kutokana na mlipuko wa kinyuklia ambao huvunja(converts into) hydrogen kuwa helium. 99% ya nishati ya joto(thermal energy) inayotengenezwa na jua hutokea katika kitovu chake.

Wanasayansi wanasema kuwa jua liliundwa(formed) miaka bilioni 4.57 iliyopita kutokana kupasuka na kusambaratika kwa "giant molecular cloud" lilosheheni kwa wingi hydrogen na helium. Mpasuko huo ndio ukazaa nyota nyingi ikiwemo na nyota jua

Ikiwa sasa na umri wa miaka bilioni 4.5 jua iko nusu ya umri wake kama vile mtanzania akiwa na miaka 30 yuko nusu ya umri wake. Dunia imeshachoma nusu ya akiba yake ya hydrogen na kiasi kilichobaki kinakadiriwa kumalizika miaka bilioni 5 ijayo.

Kwakuwa nyota jua iko katika jamii ya nyota zinazojulikana Yellow Dwarf, hivyo kuisha kwa hydrogen hakutasababisha kutokea kwa supernova(mlipuko mkubwa wa nyota), bali jua litabadilika na kuwa jekundu na kubwa zaidi kiasi cha kumeza sayari za karibu kama zebaki, zuhuru na dunia.

Kwa vyovyote vile hatutashuhudia kumezwa kwa kudunia, sababu kabla hata ya dunia kumezwa maji yote juu ya uso wa dunia na chini ta ardhi yatakuwa yatapotelea angani kama gesi, dunia haitakuwa na maji tena na joto lake litakuwa kubwa sana kiasi kila kiumbe hai afe. MWISHO WA DUNIA.

Hydrogen ikiisha na helium itaendelea kuchomeka kwa miaka milioni 130, kwa kipindi hicho jua na mfumo wa jua utakuwa umebadilika sana, na hilo likitokea orbiti ya dunia inakuwa si sehemu salama ya dunia.

Mambo yatakayo weza kufanyika ili kuwe na usalama ni kwa orbit hiyo kuahamishwa kabisa kutoka ilipo sasa, na kwakuwa jua litapoteza kabisa nishati yake ya sasa na kama tujuavyo uhai uliopo duniani unategemea sana nishati ya jua, hivyo salama zaidi ni kwa dunia na orbiti yake kuahamishwa kutoka katika mfumo wa jua na kwenda katika nyota nyingine ili mradi tu hiyo nyote iwe katika kundi la nyota za likenia katika galaxy ya milky way.

Inasemekana katika galaxy zote, ni galaxy ya milky way ndio kuna uhai(milky way is only known galaxy dat support life).

Wanaanga bado wanaendelea kuifanyia utafiti anga na ulimwengu kwa ujumla, tafiti zao huenda zitakuwa msingi mzuri kwa vizazi vijavyo kujua namna ya kuihamisha dunia au kugundua nyota nyingine yenye sayari inayoweza kuwa sawa na dunia hata watu wapate kuhamia huko pindi dunia ikifikia mwisho.

Wanasayansi wanakubali uwepo wa mwisho wa dunia na wanakubali kuwa nyota jua ina mwisho wake, lakini hawakubali kuwa hayo yanasabishwa na Mungu. Hata hivyo wakati wewe uko busy kufikiria ngono, kula bata, na kuwazia sukari ya Magufuli, wao wako busy kuhakikisha dunia haifikii MWISHO na binamu hawafi na kifo kisiwe tatizo tena!

Niliitoa kwa mara ya kwanza 01/14/2016, leo nimerudia baada ya maombi.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394.
Kweli kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa ila kwa kuwa watu hamumchi Mungu shetani anawaendesha atakavyo na elimu yake inayowaelekeza wengi motoni

Dunia na vyote vilivyomo jua, nyota, mwezi n.k vina umri wa miaka 6016 tu biblia imeliweka wazi hilo na biblia ni kitabu ambacho hakijawahi kukoseaga wala utabiri wake usitimie na dunia haitakaa ifike mwisho kwa staili hiyo hata siku moja labda tu wale wanaoamini hakuna Mungu wanaweza fikiria hivyo
 
Duuuuh haya mambo nayaogopa mimi!!!
Acha tu nimrudie Mungu kwakweli.
Hawa waongo utafiti wao umebase ktk guessing hakuna hata kimoja walicho na uhakika nacho kama ww ni mkristo nakushauri soma sana biblia utagundua elimu waliyonayo haina mashiko yoyote na utatishwa na hizi ramli za hao wanaoijita wanasayansi pia kama sio mkristo nakushauri soma tu biblia kama unavyosoma vitabu vingine unavyovipenda
 
Kila kitu kwenye universe kipo kwenye motion!,jua Lina zunguka kwenye galaxy yake!, Na katika Galaxy yetu ambayo ni milky way jua kuchukua miaka million 230 kumaliza mzunguko wake!,na linazunguka kwa speed ya 828,000km/hr.
 
Mtu anaweza kuuliza kwanini viko ktk mzunguko,,, jawabu ni BING BANG!
 
Haya mambo bana... jua ndilo linaloizunguka dunia... dunia haina shape ya yai bat flat disc.... kuna another earth within our earth inaitwa shambala.... kuna ufos sights daily znakuwa posted youtube.... kuna project blue beam... kuna lucifer experiment iliyofanya sayari ya mars kuwa vile... kuna kina annunaki na sayar yao ya NIBIRU..... kuna thot mungu wa hekima aliyetoa ufaham kwa watu wa kwanza katika kisiwa cha atlantis kabla hakijazama na majini.... kuna kina Mayans ambao walishatabili mwisho wa dunia na mambo bado yanaendelea, mara ooo tumeshindwa kuisoma vizur calander yao so tutakuja na jibu halisi.... kuna aliens among us... Kuna secret base ya aliens huko southern hemisphere.... kuna time travell... kuna big bang... kuna illuminati.. kuna freemasons... kuna kila aina ya vitu ambavyo mwisho wa siku maisha yanaenda kama kawaida
 
Hawa wanaanga wanazingua sasa...mara Nibiru itaigonga dunia ooh miaka bil5 dunia itamezwa na jua..wenyewe wanajichanganya na tafiti zai! Ni kweli kuwa itafikia kipindi maisha hayatakwepo tena duniani maana hata sayari zipo ambazo zilishasambaratika miaka iliyopita na zipo zinazoendelea kusambaratika na hivyp zamu ya dunia itafika...lakini kwa hizi tafiti za hawa wanasayansi kamwe hazitaweza kutoa majibu ya moja kwa moja juu ya ni lini dunia itafika mwisho wake...
 
View attachment 356025

Jua ndio kitu pekee ambacho kiko katikati ya mfumo wa jua. Jua ni 99.86% ya uzito(mass) wa mfumo wa jua.

Kimsingi jua ni mkusanyiko wa hydrogen na helium, 74.49% hydrogen na 23.8% helium.

Joto la kitovu cha jua linakadiriwa kufikia nyuzi joto milioni 15, wakati tabaka la nje lina nyuzi joto 5500.

Jua huchukua mwezi mmoja kumaliza mzunguko wake katika mhimili wake, na hii inakadiriwa tu na sababu kubwa umbo la jua ni kama mpira wa plasma. Kutokana na umbile lake, mzunguko hutofatiana tabaka na tabaka.

Mathalani, sehemu ya tabaka la nje karibu na ikweta yake, humaliza mzunguko wake kwa siku 25.4 wakati karibu na "poles" huchukua siku 36. Imethibitika tabaka la ndani la jua huzunguka sana kuzidi tabaka la nje.

Wastani wa umbali kati ya jua na dunia ni km milioni 150 na mwanga husafiri kwa spidi ya km 300,000 kwa sekunde, ukiwa mwanahisabati na ukikokotoa utagundua mwanga wa jua hutumia dakika 8 kusafiri kutoka katika jua na kutufikia duniani.

Cha kufurahisha hapa, hii nishati hutumia dakika nane kutufikia duniani, lakini pia hutumia mamilioni ya miaka kusafiri kutoka katika kitovu cha jua na kufika katika tabaka la nje la jua(ambapo kutoka hapo ndio hutumia dakika 8 kufika duniani)

Hii ina maanisha nini? ina maanisha mwanga wa jua unao uona sasa si wasasa bali ulianza safari yake hadi kukufukia hapo ulipo mamilioni ya miaka.

Katikati ya kitovu cha jua asilimia kubwa ya nishati ya jua huzalishwa kutokana na mlipuko wa kinyuklia ambao huvunja(converts into) hydrogen kuwa helium. 99% ya nishati ya joto(thermal energy) inayotengenezwa na jua hutokea katika kitovu chake.

Wanasayansi wanasema kuwa jua liliundwa(formed) miaka bilioni 4.57 iliyopita kutokana kupasuka na kusambaratika kwa "giant molecular cloud" lilosheheni kwa wingi hydrogen na helium. Mpasuko huo ndio ukazaa nyota nyingi ikiwemo na nyota jua

Ikiwa sasa na umri wa miaka bilioni 4.5 jua iko nusu ya umri wake kama vile mtanzania akiwa na miaka 30 yuko nusu ya umri wake. Dunia imeshachoma nusu ya akiba yake ya hydrogen na kiasi kilichobaki kinakadiriwa kumalizika miaka bilioni 5 ijayo.

Kwakuwa nyota jua iko katika jamii ya nyota zinazojulikana Yellow Dwarf, hivyo kuisha kwa hydrogen hakutasababisha kutokea kwa supernova(mlipuko mkubwa wa nyota), bali jua litabadilika na kuwa jekundu na kubwa zaidi kiasi cha kumeza sayari za karibu kama zebaki, zuhuru na dunia.

Kwa vyovyote vile hatutashuhudia kumezwa kwa kudunia, sababu kabla hata ya dunia kumezwa maji yote juu ya uso wa dunia na chini ta ardhi yatakuwa yatapotelea angani kama gesi, dunia haitakuwa na maji tena na joto lake litakuwa kubwa sana kiasi kila kiumbe hai afe. MWISHO WA DUNIA.

Hydrogen ikiisha na helium itaendelea kuchomeka kwa miaka milioni 130, kwa kipindi hicho jua na mfumo wa jua utakuwa umebadilika sana, na hilo likitokea orbiti ya dunia inakuwa si sehemu salama ya dunia.

Mambo yatakayo weza kufanyika ili kuwe na usalama ni kwa orbit hiyo kuahamishwa kabisa kutoka ilipo sasa, na kwakuwa jua litapoteza kabisa nishati yake ya sasa na kama tujuavyo uhai uliopo duniani unategemea sana nishati ya jua, hivyo salama zaidi ni kwa dunia na orbiti yake kuahamishwa kutoka katika mfumo wa jua na kwenda katika nyota nyingine ili mradi tu hiyo nyote iwe katika kundi la nyota za likenia katika galaxy ya milky way.

Inasemekana katika galaxy zote, ni galaxy ya milky way ndio kuna uhai(milky way is only known galaxy dat support life).

Wanaanga bado wanaendelea kuifanyia utafiti anga na ulimwengu kwa ujumla, tafiti zao huenda zitakuwa msingi mzuri kwa vizazi vijavyo kujua namna ya kuihamisha dunia au kugundua nyota nyingine yenye sayari inayoweza kuwa sawa na dunia hata watu wapate kuhamia huko pindi dunia ikifikia mwisho.

Wanasayansi wanakubali uwepo wa mwisho wa dunia na wanakubali kuwa nyota jua ina mwisho wake, lakini hawakubali kuwa hayo yanasabishwa na Mungu. Hata hivyo wakati wewe uko busy kufikiria ngono, kula bata, na kuwazia sukari ya Magufuli, wao wako busy kuhakikisha dunia haifikii MWISHO na binamu hawafi na kifo kisiwe tatizo tena!

Niliitoa kwa mara ya kwanza 01/14/2016, leo nimerudia baada ya maombi.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394.
Acha kutishatisha watu! Dunia ipo, na itakuwepo tu,Hakuna mzungu anayeweza kujua kiyama.
 
Hawa wanaanga wanazingua sasa...mara Nibiru itaigonga dunia ooh miaka bil5 dunia itamezwa na jua..wenyewe wanajichanganya na tafiti zai! Ni kweli kuwa itafikia kipindi maisha hayatakwepo tena duniani maana hata sayari zipo ambazo zilishasambaratika miaka iliyopita na zipo zinazoendelea kusambaratika na hivyp zamu ya dunia itafika...lakini kwa hizi tafiti za hawa wanasayansi kamwe hazitaweza kutoa majibu ya moja kwa moja juu ya ni lini dunia itafika mwisho wake...
Kinacho semwa ni ukweli lakini kipindi hicho tutakuwa hatua nyingine mwombe Mungu na ushike amri zake
 
Hiyo miaka billion 5 mie sintakuwepo wala kizazi changu hao watakao kuwepo na jamii forum itakuwepo nawwambie wajipange
 
Back
Top Bottom