Mambo usiyoyajua kuhusu nyota Jua na mwisho wa sayari Dunia

Mambo usiyoyajua kuhusu nyota Jua na mwisho wa sayari Dunia

View attachment 356025

Wastani wa umbali kati ya jua na dunia ni km milioni 150 na mwanga husafiri kwa spidi ya km 300,000 kwa sekunde, ukiwa mwanahisabati na ukikokotoa utagundua mwanga wa jua hutumia dakika 8 kusafiri kutoka katika jua na kutufikia duniani.

Cha kufurahisha hapa, hii nishati hutumia dakika nane kutufikia duniani, lakini pia hutumia mamilioni ya miaka kusafiri kutoka katika kitovu cha jua na kufika katika tabaka la nje la jua(ambapo kutoka hapo ndio hutumia dakika 8 kufika duniani)

Hii ina maanisha nini? ina maanisha mwanga wa jua unao uona sasa si wasasa bali ulianza safari yake hadi kukufukia hapo ulipo mamilioni ya miaka.

Call/whatspp 0622845394.

Unamaanisha nini unaposema mamillion ya miaka tena? Mwanga wa jua usafiri mamillion ya miaka kutoka wapi kwenda wapi? Ndani ya mipaka ya/ mzingo wa jua lenyewe? Kipenyo cha jua ni 2x69,5700km=1,391,400km, kitu ambacho kinamaanisha mwanga wa jua ukisfairi kwa kufuata kipenyo cha jua (ndani ya jua lenyewe) utachukua si zaidi ya sekunde tano (5) tu. Hayo mamillion ya miaka ulikuwa unamanisha kitu gani?
 
kumbe na jua linazunguka, kuna mdau alileta uzi hapa kuhusu kuzunguka kwa jua watu wakamtolea povu.
Jua linazunguka katika mhimili wake, na pia linazunguka pamoja na mfumo wote wa solar system yetu kwenye center of our galaxy,mzunguko wa solar system yetu kuzunguka center ya galaxy yetu unatumia miaka million 200 ku complete rotation

vitabu vyetu vingi vya secondary na msingi vimeandika jua halizunguki, inabidi wabadilishe tu hakuna namna
 
Linazunguka sababu kuna nguvu kubwa ya uvutano katikati ya galaxy yetu, ambapo kuna largest blackhole, hii blackhole ina gravity kubwa sana inaforce nyota zote and everything in our galaxy to revolve around, hapo ndio maana linazunguka
unaweza nifahamisha black holes ni nini..? na kazi yake..?
 
unaweza nifahamisha black holes ni nini..? na kazi yake..?
Kujua blackhole nini, kwanza kabisa ni muhimu kujua nyota zinafanyaje kazi?

Nyota yeyote hata jua letu zinatengeneza nishati yake kwa kubadilisha hewa ya hydrogen kuwa helium(ambayo hii ni nuclear fusion)

Nyota kubwa ambazo ni mara tano zaidi ya jua ndizo ambazo zina badilika na kuwa blackholes umri wake ukiisha isha yaani ikimaliza hydrogen yote, halafu helium inaanza kubadilishwa kwenda kwenye heavy elements kama carbon, iron

Hizi element nzito zinafanya nyota kuwa nzito zaidi, hapo nyota inakuwa unastable na kulipuka kuwa blackhole, nyota iliyokuwa kubwa zaidi mara tano zaidi ya jua ikilipuka inaweza kuwa ndogo kama dunia na inakuwa na gravity kubwa sana ambapo hata mwanga hauwezi kukimbia, nothing can escape from it

Kulipuka kwa nyota kunaitwa supernova, nyota ndogo kama jua hazilibuki wala kutengeneza supernova zinakua red giant

Kwa hiyo blackholes ni sehemu kwenye space ambayo ina gravity kubwa sana kiasi kwamba hata mwanga hauwezi kukimbia,wala chochote kile hakiwezi kukimbia
,kinachosababishwa na nyota kufa

Hapa kwenye blackhole hata nyota nyingine ikipita karibu inavutwa na kuwezwa

Kazi ya blackhole bado sijajua ni nini hasa
 
Mleta mada muendelezo basi mkuu. Huu uzi usingetakiwa kuishia hapa aisee
 
Back
Top Bottom