Mambo usiyoyajua kuhusu online dating platforms

Mambo usiyoyajua kuhusu online dating platforms

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Kuna siku nilikuwa nachat na mdada flani mwenye pesa zake, lakini ana ndoto za kuolewa na mzungu. Hivyo anatumia muda mwingi kwenye online dating platforms akitafuta bwana wa kizungu. Katika kuzungumza akawa amenitajia mtandao flani ambapo kila msg unayotuma inalipiwa. Akaniambia kuanzia mwaka jana mpaka mwaka huu mwezi wa saba ameshatumia $7000 kulipia hiyo huduma. Nilishtushwa sana inawezekanaje mtu kutumia pesa hiyo yote. Na mbaya zaidi pesa nyingi kazitumia kwa mtu mmoja tu ambaye anaonyesha interest ya kama wako karibu

Nikamuuliza kama washakuwa karibu kwanini wasipeane njia nyingine za kuwasiliana kama email, au whatsapp number ili wawe wanawasiliana bila kutumia pesa. Akasema yeye alimpa namba yake, na email ila jamaa hajawahi kumtumia any msg whatsapp wala kwenye email hivyo akitaka kuwasiliana naye mpaka aende kwenye huo mtandao. Nilianza kuhisi kuna jambo haliko sawa na nikahisi huenda jamaa hamtaki huyo dada huwa anachat naye tu.

Juzi juzi hapa ndipo nilikuja kupata jibu la swali langu. Mimi muda mwingi nakuwa online nafanya shughuli za freelancing as my full time job, sasa juzi juzi nikaona kuwa jamaa anatafuta watu wa kumanage customer support online services. Kumcheki, akaniambia nimchek whatsapp akanipa namba nikamcheck whatsapp akanipa link ya skype, kuiclick ikanipeleka kwenye group flani la skype. Kufika mle nikakutana watu kibao na halikuanza leo yani kuna members wengi sana na shared documents nyingi sana na wanajadili kuhusu seminars ambazo washapata.

Mimi nikatumiwa document moja ili niisome. Nilipoisoma ndipo nikajua nini kinaendelea. Kwanza, kumbe ni kazi ya kuchat na watu wanaotafuta wapenzi, yani mtu akiingia kwenye ule mtandao ataona profile ambayo itakuwa na picha fake na kila kitu fake atakuchagua mtaanza chat, na ni kwamba leo anaweza chat na mimi kesho akachat na mwingine akidhani ni same person. Na kwa wakati mmoja mtu anaweza kuwa anachat na watu zaidi ya watu wakiwa wao wanadhani wana chat na mtu mmoja au watu tofauti.

Kuna jinsi ya kuhandle unafundishwa, lugha utakayotumia na huruhisiwi kuwa unatuma sentence zinazofanana iwapo unachat na watu tofauti kwa wakati mmoja. Kitu kingine huruhusiwi kumfanya mtu aone kama umekubali kuwa mpenzi wake, au kupanga miadi ya kukutana, au kubadilishana namba au mawasiliano ya aina yoyote. Ikitokea akakupeleka huko au akakutumia mawasiliano we ignore anzisha topic nyingine.

Jambo lingine hakikisha mtu unamuuliza maswali ili umfanye asiondoke yani umfanye aendelee kuchat kwasababu kila msg anayotuma anakatwa pesa na wewe unalipwa kutokana umechatisha watu msg ngapi.

Kuna mengi hata document sikufika mwisho nikamwambia jamaa mimi siwezi kufanya kazi hiyo nikajitoa. Ila nikajua kumbe yule mdada alikutana na kitu cha namna hii. Ndiyo maana jamaa alikuwa hampi mawasiliano na alipompa ya kwake alikuwa ana ignore wala hata hashukuru kusema ameyaona.
 
Dada mtanzania katumia million 15 Ku chat??
Anatafuta mzungu yuko addicted na chating... Sina ushahidi juu ya hilo kama ametumia kiasi hicho cha pesa lakini that is what she told me. Na alikuwa anasifia huo mtandao kuwa ni mzuri ila ni expensive kwa kuwa kila msg unayotuma inakucost 0.05$
 
Kwani lazima aende huko ili apate mzungu si angetumia hiyo $7000 kwenye mazingira halisia angeenda Massachusetts, USA huko wazungu Wengi tuu wanapenda Black chicks, yani asingekosa hata

[emoji419]Hio Strategy ni nzuri hata JF wanawez kuitumia kukuza mtandao wao Au pengine inatumika humu tayari nobody knows [emoji5][emoji3]
 
Kwani lazima aende huko ili apate mzungu si angetumia hiyo $7000 kwenye mazingira halisia angeenda Massachusetts, USA huko wazungu Wengi tuu wanapenda Black chicks, yani asingekosa hata

[emoji419]Hio Strategy ni nzuri hata JF wanawez kuitumia kukuza mtandao wao Au pengine inatumika humu tayari nobody knows [emoji5][emoji3]
Mkuu huko Marekani ma Blacks ni 13% ya total population lakini mara nyingi utauta mweusi kamuoa mweusi na mzungu kamuoa mzungu.
 
Mkuu shughuli yote ilianzia upwork, Sina hakika kama kujiunga kwenye group bila kukuruhusu mhusika it will work maana mimi kuingia tu napokea na msg za kukaribishwa.
unga tu mzee baba hayo yatakuja mbele kwa mbele..
 

Lakini inatokeaje unakosa mwanaume wa kuwa naye kwa hizi platforms za kikwetu kama JF na Insta na mengineyo hadi uanze kulipia duuh ??
Daah maajabu haishi kila kukicha. Mie mwanzo nilikuwa addicted na live webcams ambazo wanakuwa wanakuchatisha mwanzo alfu kuna kuwa live webcam sex video chats daah baadae wanakuambia ujiunge uanze kulipia na hapo ndio ulikuwa mwisho wa mimi kuwa pale nahamia kwingine. Daaah ugeni wa internet ulinitesa bila kujua aseee. Hapo ilikuwa first year nimetoka Jeshi, nikitumia wifi ya hostel [emoji23][emoji23][emoji23] na baada ya msuli wa usiku na panda na laptop yangu kitandani juu.
Daaah magonjwa ya akili yapo mengine sio lazima uokote makopo au uonekane violent with no reason.
 
Back
Top Bottom