Mambo usiyoyajua kuhusu online dating platforms

Mambo usiyoyajua kuhusu online dating platforms

Kwani lazima aende huko ili apate mzungu si angetumia hiyo $7000 kwenye mazingira halisia angeenda Massachusetts, USA huko wazungu Wengi tuu wanapenda Black chicks, yani asingekosa hata

[emoji419]Hio Strategy ni nzuri hata JF wanawez kuitumia kukuza mtandao wao Au pengine inatumika humu tayari nobody knows [emoji5][emoji3]

Nasikiaga kuna Jukwaa la wakubwa, lakini toka nijiunge JF nina miaka karibia 5 (My very first JF account) nilisahaugu password nikafungua nyingine tena yaani sijawahi pata fursa kuliona hilo jamvi. Sasa sijui ipo au ni maneno tu ya uongo [emoji19][emoji19]
 
Lakini inatokeaje unakosa mwanaume wa kuwa naye kwa hizi platforms za kikwetu kama JF na Insta na mengineyo hadi uanze kulipia duuh ??
Daah maajabu haishi kila kukicha. Mie mwanzo nilikuwa addicted na live webcams ambazo wanakuwa wanakuchatisha mwanzo alfu kuna kuwa live webcam sex video chats daah baadae wanakuambia ujiunge uanze kulipia na hapo ndio ulikuwa mwisho wa mimi kuwa pale nahamia kwingine. Daaah ugeni wa internet ulinitesa bila kujua aseee. Hapo ilikuwa first year nimetoka Jeshi, nikitumia wifi ya hostel [emoji23][emoji23][emoji23] na baada ya msuli wa usiku na panda na laptop yangu kitandani juu.
Daaah magonjwa ya akili yapo mengine sio lazima uokote makopo au uonekane violent with no reason.
Una bahati hukukutana na Philippine maana ndo cartel yao, unachart na dem mnaanaza sex chat aanavua nguo anakushawishi uvue basi ukivua tu kwisha habari yako. Baadae watakwambia uwalipe au wazitume mtandaoni na ndugu zako. Kuna sehemu ilikuwa kama kijiji mdada ndiye alianzisha huo mchezo, unaambiwa sehemu imeendelea sana ikawa mji mdogo kwasababu kila familia ina ndugu ameajiliwa na huyo mdada kwa ajili ya kazi hiyo.

Ofisi ya western union ya eneo hilo mwaka jana ndiyo iliongoza kupokea pesa kwakuwa walionasa walikuwa wanalipa kwa njia hiyo. Mwaka jana pekee inakadiliwa wamechukua dollar milion 1.9 toka kwa watu.

Na mdada wanampensa sana maeneo hayo. Mimi personality sijawahi penda ma video call kabisa. Na kuchat mtandaoni siyo hobby yangu nilikuwa napenda za mana enzi za yahoo messenger, the grid, mig33 na miaka 2007 facebook ila siyo kuanzia 2012 hiyo hobby ilikufa.
 
Nasikiaga kuna Jukwaa la wakubwa, lakini toka nijiunge JF nina miaka karibia 15 (My very first JF account) nilisahaugu password nikafungua nyingine tena yaani sijawahi pata fursa kuliona hilo jamvi. Sasa sijui ipo au ni maneno tu ya uongo [emoji19][emoji19]
Mkuu huwezi kuwa na miaka zaidi ya 15 JF maana JF ilianza mwaka 2006 na ilikuwa hapo ikiitwa jambo forums so ukipiga hesabu toka inaitwa jambo forums mpaka sasa ni miaka 14
 
Kuna siku nilikuwa nachat na mdada flani mwenye pesa zake, lakini ana ndoto za kuolewa na mzungu. Hivyo anatumia muda mwingi kwenye onlien dating platforms akitafuta bwana wa kizungu. Katika kuzngumza akawa amenitajia mtandao flani ambapo kila msg unayotuma inalipiwa. Akaniambia kuanzia mwaka jana mpaka mwaka huu mwezi wa saba ameshatumia $7000 kulipia hiyo huduma. Nilishtushwa sana inawezekanaje mtu kutumia pes ahiyo yote. Na mbaya zaidi pesa nyingi kazitumia kwa mtu mmoja tu ambaye anaonyesha interest ya kama wako karibu

Nikamuuliza kama washakuwa karibu kwanini wasipeane njia nyingine za kuwasiliana kama email, au whatsapp number ili wawe wanawasiliana bila kutumia pesa. Akasema yeye alimpa namba yake, na email ila jamaa hajawahi kumtumia any msg whatsapp wala kwenye email hivyo akitaka kuwasiliana naye mpaka aende kwenye huo mtandao. Nilianza kuhisi kuna jambo haliko sawa na nikahisi huenda jamaa hamtaki huyo dada uwa anachat naye tu.

Juzi juzi hapa ndipo nilikuja kupata jibu la swali langu. Mimi muda mwingi nakuwa online nafanya shughuli za freelancing as my full time job, sasa juzi juzi nikaona kuwa jamaa anatafuta watu wa kumanage customer support online services. Kumcheki, akaniambia nimchek whatsapp akanipa namba nikamcheck whatsapp akanipa llink ya skype, kuiclick ikanipeleka kwenye group flani la skype. Kufika mle nikakutana watu kibao na halikuanza leo yani kuna members wengi sana na shared documents nyingi sana na wanajadili kuhusu seminars ambazo washapata.

Mimi nikatumiwa document moja ili niisome. Nilipoisoma ndipo nikajua nini kinaendelea. Kwanza, kumbe ni kazi ya kuchat na watu wanaotafuta wapenzi, yani mtu akiingia kwenye ule mtandao ataona profile ambayo itakuwa na picha fake na kila kitu fake atakuchagua mtaanza chat, na ni kwamba leo anaweza chat na mimi kesho akachat na mwingine akidhani ni same person. Na kwa wakati mmoja mtu anaweza kuwa anachat na watu zaidi ya watu wakiwa wao wanadhani wana chat na mtu mmoja au watu tofauti.

Kuna jinsi ya kuhandle unafundishwa, lugha utakayotumia na huruhisiwi kuwa unatuma sentence zinazofanana iwapo unachat na watu tofauti kwa wakati mmoja. Kitu kingine huruhusiwi kumfanya mtu aone kama umekubali kuwa mpenzi wake, au kupanga miadi ya kukutana, au kubadilishana namba au mawasiliano ya aina yoyote. Ikitokea akakupeleka huko au akakutumia mawasiliano we ignore anzisha topic nyingine.

Jambo lingine hakikisha mtu unamuuliza maswali ili umfanye asiondoke yani umfanye aendelee kuchat kwasababu kila msg anayotuma anakatwa pesa na wewe unalipwa kutokana umechatisha watu msg ngapi.

Kuna mengi hata document sikufika mwisho nikamwambia jamaa mimi siwezi kufanya kazi hiyo nikajitoa. Ila nikajua kumbe yule mdada alikutana na kitu cha namna hii. Ndiyo maana jamaa alikuwa hampi mawasiliano na alipompa ya kwake alikuwa ana ignore wala hata hashukuru kusema ameyaona.
Dola elfu saba na bado hajui mwelekeo ?

Aisee huyo dada mtafte mwambie aje hapa zanzibar akizurura siku mbili tu beach lazima atimize ndoto yake wazungu watamwopoa chap sana

Juzi hapa zimepita waka wiki mbili ivi kuna hotel moja hapa inaitwa kiwi kuna wazungu (warusi) wamechomana visu kisa wanagombania demu mweusi wa kiafrica.

Kwa hiyo mwambie aje zenji soko analolitaka lipo ndoto yake inatimia ndani ya wiki moja tu
 
Mkuu huwezi kuwa na miaka zaidi ya 15 JF maana JF ilianza mwaka 2006 na ilikuwa hapo ikiitwa jambo forums so ukipiga hesabu toka inaitwa jambo forums mpaka sasa ni miaka 14

Nilimanisha mitano mkuu.! Hiyo moja ni mambo ya kutype haraka haraka
 
Dola elfu saba na bado hajui mwelekeo ?

Aisee huyo dada mtafte mwambie aje hapa zanzibar akizurura siku mbili tu beach lazima atimize ndoto yake wazungu watamwopoa chap sana

Juzi hapa zimepita waka wiki mbili ivi kuna hotel moja hapa inaitwa kiwi kuna wazungu (warusi) wamechomana visu kisa wanagombania demu mweusi wa kiafrica.

Kwa hiyo mwambie aje zenji soko analolitaka lipo ndoto yake inatimia ndani ya wiki moja tu
Atajua mwenyewe, halafu ni mtu mwenye status yake anafanya kazi yake nzuri tu usidhani ni mdada wa mjini mjini.
 
Baada ya kugundua Hilo, umemsaidiaje au unamsaidiaje huyo dada atoke usingizini na asiendelee kutapeliwa!?
 
Nilimanisha mitano mkuu.! Hiyo moja ni mambo ya kutype haraka haraka
Mimi nilijiunga JF 2010 na ID yangu nikaitumia baadae sijui ilikuwaje wakaipiga lifetime ban na nilikuwa nimeungwa jukwaa la wakubwa
 
Baada ya kugundua Hilo, umemsaidiaje au unamsaidiaje huyo dada atoke usingizini na asiendelee kutapeliwa!?
Nimsaidie nini sasa mkuu, nina zaidi ya miezi minne sijawasiliana naye huenda hata mwenyewe ashagundua kuwa anapoteza pesa tu
 
Una bahati hukukutana na Philippine maana ndo cartel yao, unachart na dem mnaanaza sex chat aanavua nguo anakushawishi uvue basi ukivua tu kwisha habari yako. Baadae watakwambia uwalipe au wazitume mtandaoni na ndugu zako. Kuna sehemu ilikuwa kama kijiji mdada ndiye alianzisha huo mchezo, unaambiwa sehemu imeendelea sana ikawa mji mdogo kwasababu kila familia ina ndugu ameajiliwa na huyo mdada kwa ajili ya kazi hiyo. Ofisi ya western union ya eneo hilo mwaka jana ndiyo iliongoza kupokea pesa kwakuwa walionasa walikuwa wanalipa kwa njia hiyo. Mwaka jana pekee inakadiliwa wamechukua dollar milion 1.9 toka kwa watu.
Na mdada wanampensa sana maeneo hayo. Mimi personality sijawahi penda ma video call kabisa. Na kuchat mtandaoni siyo hobby yangu nilikuwa napenda za mana enzi za yahoo messenger, the grid, mig33 na miaka 2007 facebook ila siyo kuanzia 2012 hiyo hobby ilikufa.

Mwenyewe hobby ya kuchati huko ilikufa, sasa hivi imehamia kwenye kuchati Fb messenger na Whatsapp..!
 
Kwani kuna mtandao mtu anachat free of charge!??
Ipo Facebook, na kuna mmoja jina limetoka ni maarufu sana umejaa madem wanajiuza wanajifanya wa chuo ni bure unless ukitaka premium package. Lakini sasa hii ninayoongelea hapa mtu analipia kwa kila msg anayotuma.
 
Sijajua mpendwa..binafsi sijawahi vutiwa na wazungu hata chembe

Mi pia, navutiwagwa machotara wa mzungu na mwafrika ila sijawahi fikiria ujinga wa level ile. Ni changamoto sana mpenzi.
Labda ana ugonjwa wa akili .. mweeeh mil. 15 kabisa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Sio dating sites tu, hata online games.
Atleast online games hata nikijua nacheza na system sina noma sasa mtu anachat na mtu akijua labda kuna mahusiano yatatokea kumbe jamaa yuko kazini 😂 😂 😂
 
Mi pia, navutiwagwa machotara wa mzungu na mwafrika ila sijawahi fikiria ujinga wa level ile. Ni changamoto sana mpenzi.
Labda ana ugonjwa wa akili .. mweeeh mil. 15 kabisa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
😂😂😂😂 Kwakweli .
 
Mkuu huu ugonjwa wa wanawake kuolewa na wazungu wanao wengi sana. Wengine hawasemi live ila wanao na uliletwa na kizazi cha akina Mange
 
Back
Top Bottom