ndio maana tunapaswa kukemea sana ndoto chafu zote
Huwa naota ndoto jamaa yangu aliyefariki Januari 2021 anakuja ndotoni. Mara ya kwanza alikuja, akanifunua shuka halafu alivyoniona ni mimi akasonya na kuondoka (ni kama alikuwa anamtafuta mtu mwingine akakasirika baada ya kuona mimi sio yule anayemtafuta). Nikamsimulia bi mkubwa kuhusu ndoto hii (si unajua mama zetu wana-tuombea sana) akaniambia, kuwa jamaa alishakufa kwa hiyo tulio hai hatuchangamani na wafu, nikimuota tena nimfukuze.
Kweli baada kama ya wiki 2 hivi nikamuota tena, jamaa amekuja msafi sana (akiwa hai alikuwa mtu smart msafi), safari hii akawa na jamaa mwingine ambaye yupo hai, nikaanza kumharibia huyu marehemu kuwa anafuata nini kwetu na ilhali alishakufa, akawa hajibu kitu ila anamwangalia jamaa aliyehai amtetee, mshkaji aliye hai akasema tumwache tu, huyu ni mwenzetu, nikakomaa kuwa yeye ni mfu na hatuwezi changamana na wafu hivyo sio mwenzetu, nikamwambia atoke, jamaa (marehemu) akaondoka zake na kutokomea gizani.
Imepita miezi kibaooo kumetulia, majuzi hapa nikamuota tena, yupo umbali kama wa mita 800 hivi akaniita kwa jina, anasema nisubiri mwanangu - nikaogopa sana nikasepa home. Akaja akawa hawezi kuingia ndani, akaja dirishani kwangu chumbani anachungulia kwenye kioo, nikashtuka ndotoni na kuikemea ndoto hiyo.
Sasa sielewi kwa nini huwa naota ndoto za jamaa, na hata ndotoni huwa ninaona kabisa kuwa jamaa ni marehemu (yaani ninakuwa na akili kuwa jamaa alishakufa). Ingawa alipokufa niliona ni kama utani, sikuamini kama amekufa.
Kifo cha jamaa
Tarehe 17.12.2020 jamaa alipata maumivu makali ya kichwa akapelekwa hospitali na akaanza kupoteza akili akawa mkali na anaongea visivyoeleweka, ikabidi apigwe dawa za usingizi. Vipimo vinaonesha hakuna ugonjwa. Akahamishiwa Benjamin Mkapa Dodoma, wakampiga picha na kusema anaonekana ana ufa kwenye fuvu la kichwa na ndio linalosababisha maumivu maana kuna damu kidogo kama ilivujia kwenye ubongo, wakampa dawa atumie kuwa zitayeyusha na kuondoa hiyo damu zenyewe hakuna haja ya oparesheni. Bado maumivu yakawa makali, jamaa akawa haongei analia tu. Siku moja akamwambia mama yake, "nikipona mama nitakwambia kitu" - Alikufa na hajasema hicho kitu. Familia ilipoona hali ngumu ikaamua afanyiwe tambiko, wakanunua ng'ombe, ilibaki siku 1 tambiko kufanyika, usiku wake jamaa akaishiwa oksijeni na akakata moto akiwa ICU. Tukasikitika sana na kumzika kijijini kwa babq yake, sasa baadae tukasikia story kuwa jamaa alimchukua demu ofisini kwao kumbe ni demu wa mtu, huyo mwenye demu alimfuata jamaa na kumwomba aachane na manzi wake, jamaa yetu akajibu mbovu kuwa jamaa aongee na demu wake. Hatuna uhakika kama alikuwa ni demu tu au mchumba au mke. Inasemwa kuwa jamaa mwenye demu akasema kuwa poa tutaona, siku mbili mbele ndio jamaa akaanza kuumwa kichwa.
Kwa hiyo jamaa alikufa kiutani utani hivyo.
CC:
Mshana Jr LIKUD