SoC04 Mambo ya kufanya kuongeza nidhamu uwajibikaji na morali kwa wafanyakazi kuifikia Tanzania tuitakayo

SoC04 Mambo ya kufanya kuongeza nidhamu uwajibikaji na morali kwa wafanyakazi kuifikia Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

kagram

Member
Joined
May 1, 2024
Posts
5
Reaction score
3
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya huduma mbovu kutokuwajibika kuombwa rushwa na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma katika maofisi ya umma.

Ipo haja ya serekali kuanzisha dawati la huduma kwa wateja na kutoa namba maalum kama ilivyo kwa mitandao ya simu ili wananchi waweze kufikisha malalamiko yao kwa uharaka na usalama zaidi.

Ili kuepusha wafanyakazi kuchafuliwa na kuonewa namba hiyo iwekewe aina za makosa au kero ili mlalamika achague kabla ya kuongea na mtoa huduma.

Nashauri kwenye maofisi ya umma kuwe na camera za usalama (CCTV camera) na vinasa sauti ili yanapotokea malalamiko video na sauti kutoka kwenye camera hizo zitumike kama ushaidi ili hali itendeke bila uonevu.

Matumizi ya vifaa vya kusaini kwa alama za vidole kwa watumishi yazingatiwe na adhabu zitolewe kwa wachelewaji kwani katika maofisi mengi kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuingia na kuwai kutoka ofisini kwa baadhi ya watumishi.

Ili kuongeza morali kwa wafanyakazi kuwe na zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi bora kila mwezi na kuwepo na matukio ya kuwakutanisha wafanyakazi pamoja ikiwa ni pamoja na michezo kama ya kuvuta kamba kukimbiza kuku na michezo ya mpira wa mikono miguu na kikapu au sherehe ndogo ndogo. Matukio haya yafanyike walau mara nne kwa mwaka ili kuongeza morali na kuleta umoja na upendo kwa wafanyakazi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom