Stuntman96
New Member
- May 13, 2013
- 4
- 2
Ukatili wa kijinsia ni kitendo anachofanyiwa mtu bila ridhaa yake na kumletea madhara mbali mbali kimwili, kiakili au kisaikolojia. Na huweza kutokea kwa wanawake, wanaume, wavulana na wasichana. Wanawake na watoto ni makundi ambayo yameonekana kuathiriwa zaidi na ukatili wa kijinsia kuliko wanaume.
UKATILI WA KINGONO KWA WATOTO
Ni kitendo cha kujaribu kufanya mapenzi ama vitendo vya kuashiria ngono na mtoto. Inaweza kuwa kwa kutumia nguvu,kushawishi, vitisho, kilevi, ndoa za utotoni na kumshika/kumpapasa kimapenzi. Mfano ni pamoja na kubaka, kulawiti, kuingiza vitu vigumu sehemu za siri, nk.
NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA UKATILI KWA WATOTO:
Dhibiti maudhui anayotazama mtoto kwenye televisheni. Yawe ni ya watoto tu ili asione vitendo vya ngono ni kitu cha kawaida
Mzuie mtoto kuhudhuria ngoma za mikesha 'vigodoro' kwakua ngoma hizo hushawishi na kuchochea vitendo vya ngono.
Tambua mazingira anayocheza mtoto pamoja na watu anaocheza nao ili kuona kama ni salama kwake
Asilale na wageni waliomzidi umri mkubwa
Jenga nae ukaribu ili akuamini aweze kukwambia lolote ikiwemo ukatili ikitokea amefanyiwa
Kubadilisha mitazamo ya wanajamii waone ukatili wa kingono ni kosa la jinai na sio jambo la aibu
Watoa huduma wawe na lugha rafiki na usiri ili kutomkatisha tamaa na kumtisha mwathiriwa
Kuripoti kesi za ukatili zilizoamuliwa ili kuhamasisha wengine kuripoti
Kuepuka kumaliza kesi nje ya mahakama ili watenda ukatili wasirudie tena.

Upvote
1