Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Sasa mtu kama Lowassa ambaye hakuwa vizuri kiafya bado tu mtu huyo ilihitaji afanye mdahalo ndio mjue kama kuna shida? Alihojiwa na Zuhur Yunus akaanza kusema anamuonea.L
Kama Magufuli na Lowassa wangeshiriki mdahalo na wagombea wengine wananchi wangegundua udhaifu wa hao wawili na hata kama wangechaguliwa wasingeshinda kwa kishindo na wananchi wangekuwa wanajilaumu wenyewe. Magufuli ndo Rais pekee toka Uhuru ambaye wananchi walitambua udhaifu wake kwa matendo na maneno yake miezi michache tu baada ya kushika madaraka. Wananchi walinunua mbuzi kwenye kiroba bila kujiridhisha kuwa wamenunua mbuzi kumbe wameuziwa mtoto wa fisi bahati nzuri wamegundua kosa lao itabidi wammalize kabla hajawa mkubwa awamalize. Fisi ni fisi huwezi kumbadili kuwa mbuzi hata ujaribu kwa nguvu zako zote!
Pamoja na yote hayo ila bado watu wakampigia kura kutaka awe rais.
Lissu kama kweli ana nia ya kufanya mdahalo basi sio lazima hadi afanye mdahalo na Magufuli,wote tunajua kuwa Magufuli hawezi mdahalo na ndio maana hata 2015 hakufanya ila bado mdahalo unaweza kufanyika na tukaona huo uwezo wa Lissu kama tulivyoonaga uwezo wa Mama Anna Mghwila.