Uchaguzi 2020 Mambo ya kujibizana kwenye kampeni ya nini wakati mnaweza kumaliza kila kitu kwenye mdahalo?

Sasa mtu kama Lowassa ambaye hakuwa vizuri kiafya bado tu mtu huyo ilihitaji afanye mdahalo ndio mjue kama kuna shida? Alihojiwa na Zuhur Yunus akaanza kusema anamuonea.
Pamoja na yote hayo ila bado watu wakampigia kura kutaka awe rais.

Lissu kama kweli ana nia ya kufanya mdahalo basi sio lazima hadi afanye mdahalo na Magufuli,wote tunajua kuwa Magufuli hawezi mdahalo na ndio maana hata 2015 hakufanya ila bado mdahalo unaweza kufanyika na tukaona huo uwezo wa Lissu kama tulivyoonaga uwezo wa Mama Anna Mghwila.
 
Nani kakwambia haeleweki..... Watu haeaelewi kuhusu ndege na madaraja na ujenzi wa chato int airport.....

Hakuna mwanaccm mwenye akili za kufanya mdahalo na Mh Tundu Antipas Mugway LISSU......
 
Sasa huoni na sisi Tanzania ni bora tuanzishe utawala wa majimbo kabla ya kufikia huko kwenye kutwangana, na inawezekana tukafika maana haiingii akilini watu walime korosho kwa nguvu na jasho lao wewe upore pesa ukajengee uwanja wa ndege kijijini kwenu,

Kama mmeshindwa kuigawa keki ya taifa kwa usawa ni bora utawala wa majimbo ili rasilimali za eneo husika zianze kuwaneemesha wakazi wa eneo mahalia
 
Jiwe hana uwezo kiakili hata kifikra kufanya mdahalo na Lissu juu ya jambo lolote sembuse Sera ya majimbo! Ufafanuzu wake Jana kuhusu Sera hii umezua mjadala zaidi ya ufinyu wa uelewa wake. Ni heri angekaa kimya. Sera ya majimbo ndiyo mwendo wa dunia sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…