Mambo ya kushangaza Biblia inapozungumzia Ngono kwa binadamu

Mambo ya kushangaza Biblia inapozungumzia Ngono kwa binadamu

Kizuio

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
845
Reaction score
521
Ngono
Maana: Tabia ya viumbe wa duniani ambayo ni njia ya kuzaana kutokana na wazazi wawili. Tofauti kati ya jinsia ya kiume na kike huleta mabadiliko mengi katika maisha ya wanadamu. Kwa kuwa Mungu mwenyewe ndiye Chanzo cha uhai na kwa kuwa wanadamu walikusudiwa waonyeshe sifa zake, uwezo wa kupitisha uhai kwa mahusiano ya ngono unapaswa uheshimiwe sana.

Je, Biblia inafundisha kwamba mahusiano ya ngono ni dhambi?

Mwa. 1:28: “Mungu akawabariki [Adamu na Hawa] na Mungu akawaambia: ‘Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia.’” (Ili kutimiza amri hii ya Mungu, ingekuwa lazima wawe na mahusiano ya ngono, sivyo? Kufanya hivyo hakungekuwa dhambi bali kungepatana na kusudi la Mungu la kuijaza dunia watu. Watu fulani wamefikiri kwamba lile ‘tunda lililokatazwa’ katika Edeni lilimaanisha kwamba labda Mungu aliwazuia au hata kuwakataza Adamu na Hawa wasiwe na mahusiano ya ngono. Lakini hilo linapingana na amri ya Mungu iliyonukuliwa juu. Pia linapingana na uhakika wa kwamba, ingawa Adamu na Hawa walikula lile tunda lililokatazwa katika Edeni, mtajo wa kwanza wa kufanya kwao ngono ulikuwa baada ya kufukuzwa kutoka humo.—Mwa. 2:17; 3:17, 23; 4:1.)

Mwa. 9:1: “Mungu akambariki Noa na wanawe, akawaambia: ‘Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia.’” (Baraka hii ya ziada, pamoja na kurudiwa kwa amri ya Mungu ya kuzaa, ilitolewa baada ya ile Gharika duniani katika siku za Noa. Maoni ya Mungu kuhusu mahusiano halali ya ngono hayakuwa yamebadilika.)

1 Kor. 7:2-5: “Kwa sababu ya kuenea kwa uasherati, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mke wake haki yake; lakini mke pia na amfanyie vivyo hivyo mume wake. . . . Msiwe mkinyimana haki hiyo, ila kwa makubaliano kwa wakati uliowekwa, . . . ili Shetani asiendelee kuwajaribu kwa sababu ya ninyi kukosa kujizuia.” (Jambo ambalo linaonyeshwa kuwa ni kosa ni uasherati, lakini si mahusiano ya ngono halali kati ya mume na mke.)

Je, ni makosa kuwa na mahusiano ya ngono kabla ya ndoa?

1 The. 4:3-8: “Haya ndiyo mapenzi ya Mungu . . . kwamba mjiepushe na uasherati; kwamba kila mmoja wenu ajue jinsi ya kukiweka chombo chake mwenyewe katika utakaso na heshima, si katika hamu yenye tamaa ya ngono kama ile waliyo nayo pia mataifa wale wasiomjua Mungu; kwamba yeyote asifikie hatua ya kudhuru na kuziingilia haki za ndugu yake katika jambo hilo, kwa sababu Yehova ndiye anayelipiza adhabu kwa ajili ya mambo yote haya, kama vile tulivyowaambia ninyi kimbele na pia tukawapa ushahidi kamili. Kwa maana Mungu alituita sisi bila kuruhusu nafasi ya uchafu, bali kuhusiana na utakaso. Kwa hiyo, basi, mtu anayepuuza hampuuzi mwanadamu, bali Mungu, anayeitia roho yake takatifu ndani yenu.” (Neno la Kigiriki por·neiʹa, lililotafsiriwa “uasherati,” linamaanisha tendo la ngono kati ya watu ambao hawajaoana, pia mahusiano ya ngono nje ya ndoa kwa watu waliooana.)

Efe. 5:5: “Hakuna mwasherati au mtu asiye safi au mtu mwenye pupa—maana yake ni kuwa mwabudu-sanamu—aliye na urithi wowote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.” (Hilo halimaanishi kwamba yeyote ambaye zamani alikuwa mwasherati hawezi kupata baraka za Ufalme wa Mungu, lakini ni lazima aache maisha hayo ili apate kibali cha Mungu. Ona 1 Wakorintho 6:9-11.)
Je, Biblia inakubali kuishi pamoja kama mume na mke bila kuoana kisheria bila shaka hairuhusu kabisakabisa

Biblia inasema nini kuhusu ngono kati ya watu wa jinsia moja?

Rom. 1:24-27: “Kwa kupatana na tamaa za mioyo yao, Mungu aliwaacha katika uchafu, ili miili yao ivunjiwe heshima kati yao . . . Mungu aliwaacha katika hamu za ngono yenye kufedhehesha, kwa maana wanawake wao walibadili matumizi yao wenyewe ya asili kuwa yale yaliyo kinyume cha asili; na vivyo hivyo pia hata wanaume waliacha matumizi ya asili ya mwanamke na kuwakiana tamaa kali katika uchu wao kuelekeana wao wenyewe, wanaume kwa wanaume, wakitenda mambo machafu na kupokea ndani yao wenyewe malipo kamili, yaliyostahili kosa lao.”

1 Tim. 1:9-11: “Sheria huwekwa, si kwa ajili ya mtu mwadilifu, bali kwa ajili ya watu wenye kuasi sheria na watundu, wasiomwogopa Mungu na watenda-dhambi, . . . waasherati, wanaume wanaolala na wanaume, . . . na jambo lingine lolote linalopinga fundisho lenye afya kulingana na habari njema yenye utukufu ya Mungu mwenye furaha.” (Linganisha na Mambo ya Walawi 20:13.)

Yuda 7: “Sodoma na Gomora na majiji yaliyoyazunguka, baada ya hayo . . . kwenda kufuatilia mwili kwa ajili ya matumizi yasiyo ya asili, . . . yamewekwa mbele yetu kuwa kielelezo cha kuonya kwa kupatwa na adhabu ya hukumu ya moto wa milele.” (Jina Sodoma ndilo msingi wa neno la Kiingereza “sodomy,” ambalo kwa kawaida humaanisha tendo la ngono kati ya watu wa jinsia moja. Linganisha na Mwanzo 19:4, 5, 24, 25.)

Wakristo wa kweli wanawaonaje wale ambao wamekuwa na zoea la kufanya ngono na watu wa jinsia moja?

1 Kor. 6:9-11: “Wala waasherati, wala waabudu-sanamu, wala wazinzi, wala wanaume wanaowekwa kwa ajili ya makusudi yasiyo ya asili, wala wanaume wanaolala na wanaume . . . hawataurithi ufalme wa Mungu. Na bado wengine wenu mlikuwa hivyo. Lakini mmeoshwa mkawa safi, lakini mmetakaswa, lakini mmetangazwa kuwa waadilifu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo na kwa roho ya Mungu wetu.” (Bila kujali matendo hayo ya zamani, ikiwa sasa watu wanayaacha matendo yao machafu ya zamani, wafuate viwango vya uadilifu vya Yehova, na kuwa na imani katika uandalizi wake wa msamaha wa dhambi kupitia Kristo, wanaweza kupata msimamo safi mbele za Mungu. Baada ya kujirekebisha, wanaweza kukaribishwa katika kutaniko la Kikristo.)
Wakristo wa kweli wanajua kwamba watu ambao kweli wanataka kumpendeza Yehova wanaweza kuzishinda hata tamaa mbaya zenye nguvu, kutia ndani zile ambazo huenda zikawa za kurithiwa au zile zinazohusisha visababishi vya kimwili au vya kimazingira. Watu fulani kwa asili wanakasirika upesi. Labda zamani walikuwa wepesi kukasirika; lakini kuyajua mapenzi ya Mungu, tamaa ya kutaka kumpendeza, na msaada wa roho yake huwawezesha kujizuia. Huenda mtu akawa mlevi, lakini, akiwa na kichocheo kinachofaa, anaweza kuacha kunywa na hivyo aepuke kuwa mlevi. Vivyo hivyo, huenda mtu akahisi kuvutiwa sana na watu wa jinsia yake, lakini akitii shauri la Neno la Mungu, anaweza kubaki safi bila kufanya ngono na watu wa jinsia yake. (Ona Waefeso 4:17-24.) Yehova haturuhusu tuendelee kufikiri kwamba mwenendo mbaya ni sawa tu; kwa fadhili lakini kwa uthabiti yeye hutuonya juu ya matokeo naye huwapa msaada mwingi wale wanaotaka ‘kuvua utu wa zamani pamoja na mazoea yake, na kujivika utu mpya.’—Kol. 3:9, 10.

Je, labda maoni ya Biblia kuhusu ngono yamepitwa na wakati nayo yanawazuia watu bure?

1 The. 4:3-8: “Haya ndiyo mapenzi ya Mungu . . . kwamba mjiepushe na uasherati . . . Kwa hiyo, basi, mtu anayepuuza hampuuzi mwanadamu, bali Mungu, anayeitia roho yake takatifu ndani yenu.” (Maoni ya Biblia kuhusu ngono si jambo tu ambalo lilisitawishwa na wanadamu fulani walioishi miaka mingi iliyopita. Yanatokana na Muumba wa wanadamu; yanaonyesha wazi jambo linalotakiwa ili kupata kibali chake; pia huandaa miongozo inayosaidia familia kuwa thabiti na safi, na kuwa na mahusiano yenye furaha nje ya familia. Wale wanaofuata shauri hilo wanajilinda wenyewe wasipatwe na madhara makubwa moyoni na magonjwa mabaya yanayotokana na mwenendo usio wa adili. Shauri la Biblia ni la kisasa kabisa katika kutimiza mahitaji ya wale wanaotaka kuwa na dhamiri safi mbele za Mungu na kuishi bila kukata tamaa.)

Nawasilisha
 
Somo zuri sana zile ndoa za zamani kabla ya kristu ni nani waliwafungisha? Je walifungishwa na Mungu mwenyewe au walipopatana tuu na ngono wakaianza??je ni kuoa ni lazima mpitie kwa viongozi wa dini ndo muwe mmeoana kisheria??
Natanguliza shukran zangu mkuu
 
Mkuu h

Mkuu huyu shahidi mleta mada, akikujibu nitag
 
Somo zuri sana zile ndoa za zamani kabla ya kristu ni nani waliwafungisha? Je walifungishwa na Mungu mwenyewe au walipopatana tuu na ngono wakaianza??je ni kuoa ni lazima mpitie kwa viongozi wa dini ndo muwe mmeoana kisheria??
Natanguliza shukran zangu mkuu
Hata uwe umelipa mahari basi mkuu inatosha yaani mnatambulika na pande zote kuwa hawa ni mtu na mkewe au ni mtu na mumewe
 
Ukiwa serious njoo pm tushauriane
 
Somo zuri sana zile ndoa za zamani kabla ya kristu ni nani waliwafungisha? Je walifungishwa na Mungu mwenyewe au walipopatana tuu na ngono wakaianza??je ni kuoa ni lazima mpitie kwa viongozi wa dini ndo muwe mmeoana kisheria??
Natanguliza shukran zangu mkuu

Umewaza kama mimi, yaani siku hizi vijana wanadai michango ya harusi ili tu wafunge ndoa, yaani binadam mwenzao ndio awaamulie kuwa sasa mnaweza fanya ngono (viongozi wa dini).
 
Umewaza kama mimi, yaani siku hizi vijana wanadai michango ya harusi ili tu wafunge ndoa, yaani binadam mwenzao ndio awaamulie kuwa sasa mnaweza fanya ngono (viongozi wa dini).
Mungu ndio huwaamulia watu kufanya ngono kwa sababu yeye ndie aliyeiruhusu ila ina masharti yake lazima wafanya ngono hao wawe mwanamke kwa mwanaume na sio vinginevyo lakini pia wawe wanatambulika kwanza na pande zote za familia zao yaani kulipa mahari
Ndoa sio tu ya Kufunga msikitini au kanisani ndoa huanza pale unapolipa mahari na pande zote kuwatambua kuwa huyu ni mume wa fulani na huyu ni mke wa fulani
 
Mkuu mbona Biblia inaonyesha kuna ndoa ambazo hazina mahari wala nini yaani unaweza kujichukulia mwanamke ukamfanya mke wako tu kwa mabavu.

Waamuzi 24 sura nzima tunaona kabila la benjamin wakila njama kuteka wanawake na kuwafanya wake zao!! Na sikuona wakipata adhabu yeyote unaliongeleaje hili??

2. Je ndo sahihi kibiblia ni ipi maana kuna watu walioa wanawake zaidi ya wawili throughout Biblia ilihali leo hii tunahubiriwa kuwa ndoa ni mme na mke mmoja?? Unaweza kutusaidia hapa.

3. Kwenye kitabu cha kumb. Torati tunaona kuna sheria inaruhusu ngono kabla ya ndoa yaani inasema ukimuingilia mwanamke kabla ya ndoa inatakiwa ulipe shekeli 50 tu basi anakuwa mke wako daima..... Je unaposema ngono kabla ya Ndoa hairuhusiwi kivipi Mungu aliruhusu hili la watu kuingiliana kabla ya ndoa kwa sharti la kutoa tu fine na unaachwa hai bila adhabu ya kifo!!

Ni hayo tu kwa sasa
 
Hata uwe umelipa mahari basi mkuu inatosha yaani mnatambulika na pande zote kuwa hawa ni mtu na mkewe au ni mtu na mumewe
Waliooana wazamani walitambulika pande zote kabla hawajaanza kwichikwichi??
NB: kila mwanamke awe na mme wake mwenyewe na mume awe na mke wake mwenyewe refer kwa wakorinto mbona pande zote hazijawekwa hapo
 
Mkuu mbona Biblia inaonyesha kuna ndoa ambazo hazina mahari wala nini yaani unaweza kujichukulia mwanamke ukamfanya mke wako tu kwa mabavu.

Waamuzi 24 sura nzima tunaona kabila la benjamin wakila njama kuteka wanawake na kuwafanya wake zao!! Na sikuona wakipata adhabu yeyote unaliongeleaje hili??

2. Je ndo sahihi kibiblia ni ipi maana kuna watu walioa wanawake zaidi ya wawili throughout Biblia ilihali leo hii tunahubiriwa kuwa ndoa ni mme na mke mmoja?? Unaweza kutusaidia hapa.

3. Kwenye kitabu cha kumb. Torati tunaona kuna sheria inaruhusu ngono kabla ya ndoa yaani inasema ukimuingilia mwanamke kabla ya ndoa inatakiwa ulipe shekeli 50 tu basi anakuwa mke wako daima..... Je unaposema ngono kabla ya Ndoa hairuhusiwi kivipi Mungu aliruhusu hili la watu kuingiliana kabla ya ndoa kwa sharti la kutoa tu fine na unaachwa hai bila adhabu ya kifo!!

Ni hayo tu kwa sasa
Kumbuka kulikuwa na migogoro kati ya kabila la benyamini na waisrael wengine hivyo Baada ya vita vilivyoua maelfu ya watu wa benyamini waliofanikiwa kukimbia ni wanaume Mia sita tu wa benyamini sasa wao walitaka kuoa tena ila wenzao walikuwa wameapa hawatawaozesha binti zao kutokana na uovu walioufanya awali sasa wao waisrael walikuwa na utaratibu wa kukutana na Mungu kwa ajili ya maombi sasa kuna kabila halikufika hapo ambalo ni watu wa yabesh gileadi na waliapa yeyote ambaye hatafika kwenye maombi atauawa hivyo walienda kuua wanawake wote ambao sio mabikira na wanaume wote wa mji ule wa gileadi na kuwachukua wasichana mabikira wapatao Mia NNE lengo lao ni kupatata na wanaume Mia sita wa kabila la benyamini waliosalia ndipo wakawatumia ujumbe wa amani nao wakaungana nao katika maombi na wakawapa wale wanaume wale wasichana mabikira wa gileadi wawe wake zao lakini hawakuwatosha kwa kuwa wasichana walikuwa Mia NNE tu wakati wanaume walikuwa Mia sita
So unaona waliozeshwa kwa taratibu zote kama ni mfatiliaji mzuri wa hiyo stori iliyotokea zamani huko Israeli
 
Ndoa sahihi ambayo Mungu aliagiza ni ya mke moja na sio wake wawili au zaid maana lengo la Mungu toka mwanzo ni mke mmoja na asipewe talaka ila watu kwa sababu ugumu wa mioyo yao waliamua watakavyo wenyewe na Yesu alilijibu vizuri swali hilo kwamba sababu za kuoa mke wa pili ni moja tu uzinzi tu zaidi ya hapo anazini tu mathayo 19/7-12
 
Waliooana wazamani walitambulika pande zote kabla hawajaanza kwichikwichi??
NB: kila mwanamke awe na mme wake mwenyewe na mume awe na mke wake mwenyewe refer kwa wakorinto mbona pande zote hazijawekwa hapo
Yaani kila mwanamke awe na mme wake mwenyewe na mwanaume awe na mke wake mwenyewe tayari hao ni watu ambao watakuwa wamefuata proses zote za kujitambulisha na kulipa mahari maana huwezi kuitwa mke au mume kama hujalipa mahari utabaki kuitwa tu mwanaume na mwanamke baasi
 
Mkuu mbona Biblia inaonyesha kuna ndoa ambazo hazina mahari wala nini yaani unaweza kujichukulia mwanamke ukamfanya mke wako tu kwa mabavu.

Waamuzi 24 sura nzima tunaona kabila la benjamin wakila njama kuteka wanawake na kuwafanya wake zao!! Na sikuona wakipata adhabu yeyote unaliongeleaje hili??

2. Je ndo sahihi kibiblia ni ipi maana kuna watu walioa wanawake zaidi ya wawili throughout Biblia ilihali leo hii tunahubiriwa kuwa ndoa ni mme na mke mmoja?? Unaweza kutusaidia hapa.

3. Kwenye kitabu cha kumb. Torati tunaona kuna sheria inaruhusu ngono kabla ya ndoa yaani inasema ukimuingilia mwanamke kabla ya ndoa inatakiwa ulipe shekeli 50 tu basi anakuwa mke wako daima..... Je unaposema ngono kabla ya Ndoa hairuhusiwi kivipi Mungu aliruhusu hili la watu kuingiliana kabla ya ndoa kwa sharti la kutoa tu fine na unaachwa hai bila adhabu ya kifo!!

Ni hayo tu kwa sasa
Hapo namba3 siyo iliruhusiwa ,Bali ilikuwa ukimbaka yaani kumuingilia pasopo mapenzi yake na kwakuwa inakuwa umesha mbikiri ili usimuache ni lazima ulipe hiyo adhabu na awe Mke wako ,ilikuwa ni desturi mwanamke asiye na bikira haolewi.
 
Kuzini ni kufanya tendo la ndoa kabla hujaoa au kuolewa au kutoka nje ya ndoa huko ndio kuzini mkuu au kumtamani mwanamke asiye mke wako wa ndoa
Unapofanya romance yaani kushikana na kiss hiyo siyo zinaa mkuu
 
Kumbuka kulikuwa na migogoro kati ya kabila la benyamini na waisrael wengine hivyo Baada ya vita vilivyoua maelfu ya watu wa benyamini waliofanikiwa kukimbia ni wanaume Mia sita tu wa benyamini sasa wao walitaka kuoa tena ila wenzao walikuwa wameapa hawatawaozesha binti zao kutokana na uovu walioufanya awali sasa wao waisrael walikuwa na utaratibu wa kukutana na Mungu kwa ajili ya maombi sasa kuna kabila halikufika hapo ambalo ni watu wa yabesh gileadi na waliapa yeyote ambaye hatafika kwenye maombi atauawa hivyo walienda kuua wanawake wote ambao sio mabikira na wanaume wote wa mji ule wa gileadi na kuwachukua wasichana mabikira wapatao Mia NNE lengo lao ni kupatata na wanaume Mia sita wa kabila la benyamini waliosalia ndipo wakawatumia ujumbe wa amani nao wakaungana nao katika maombi na wakawapa wale wanaume wale wasichana mabikira wa gileadi wawe wake zao lakini hawakuwatosha kwa kuwa wasichana walikuwa Mia NNE tu wakati wanaume walikuwa Mia sita
So unaona waliozeshwa kwa taratibu zote kama ni mfatiliaji mzuri wa hiyo stori iliyotokea zamani huko Israeli
Hiyo incident ya kwanza naifahamu nachoongelea ni baada ya wanawake kutokutosha wakapanga njama hii

Waamuzi 21
20 Basi wakawaagiza hao wana wa Benyamini wakisema, Haya, endeni, mkaotee katika mashamba ya mizabibu,
21 mkaangalie, kisha tazameni, kwamba hao binti za Shilo watoka ili wacheze katika hiyo michezo, basi tokeni ninyi mizabibuni, nanyi kila mtu na amshike mkewe katika hao binti za Shilo, kisha rudini nchi ya Benyamini

Biblia iko wazi kabisa kuwa walijificha kwenye mashamba alafu wanawake walivyokuwa wanarudi makwao wakawavamia na kila mmoja akamteka wake na kurudi naye kwake.....

Sasa swali langu lipo hapo mstari wa 21 je ni kwanini walichukua wanawake kwa mabavu bila kufuata taratibu na bado Mungu akawaacha tu?? Je ni sahihi na mimi kumteka mwanamke tu kwa mabavu na kumfanya mke wangu bila kwanza kufuata taratibu??

Hapa ndio mzizi wa swali langu mkuu
 
Hapo namba3 siyo iliruhusiwa ,Bali ilikuwa ukimbaka yaani kumuingilia pasopo mapenzi yake na kwakuwa inakuwa umesha mbikiri ili usimuache ni lazima ulipe hiyo adhabu na awe Mke wako ,ilikuwa ni desturi mwanamke asiye na bikira haolewi.
Mkuu Biblia ilisema ukibaka kwenye torati lazima uuawe ila kama mwanamke ni bikra basi hauuawi bali unamlipia mahari umuoe ndio nachouliza kama anasema ngono kabla ya ndoa ni haramu kwa mujibu wa Biblia je ni kwanini wanaobaka mabikra wanakuwa exempted na adhabu?? Hapo ndio sijaelewa
 
Back
Top Bottom