Mambo ya kutisha na yenye kuumiza hisia tunayokutana nayo tukiwa maskini

Mambo ya kutisha na yenye kuumiza hisia tunayokutana nayo tukiwa maskini

AlphaMale

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2019
Posts
613
Reaction score
1,416
Kudharauliwa, kuchekwa, kupewa maneno ya kejeli, kwa sababu ya kukosa kazi na umaskini ulionao, ingawaje anaekudharau ni maskini kama wewe..

Naapa kwa mbingu na ardhi siku nikija kufanikiwa sana kipesa, sitokuja saidia hata Mtu mmoja chini ya hili jua, nikitoa pesa ntakua nalenga faida ya mara 10 ya hela nliyotoa, nitajilimbikizia mabilioni ya shilingi kwa hasara ya wengine, hata kama jirani yangu atakufa njaa kwa kukosa elf 2.

Sitotoa hela na sitoona huruma, nitasaidia mke alienizalia watoto na watoto wangu tu, na sitotaka mazoea ya kijinga na watu wasio na faida na mm.

Nimegundua binadamu wengi ni wanafiki sana.
 
Huko ulaya na marekani wanaishi hivyo,tangu karne ya 17,wewe umechelewa sana,lakini utakapojikuta maisha yako yapo mikononi mwa hao wengine utajuta sana!! Hasa ukiwa unaishi huku mavumbini,utakuja kwa magoti nakuambia!
 
Baada ya movie huwa kuna BEHIND THE SCENE
 
Pole sana mkuu, ongeza juhudi kuzisaka noti ila usilipe kisasi.
 
Mjomba Idd tafuta pesa, toa sadaka, wasaidie wasiojiweza na usikumbuke waliokunyanyasa au kukutesa wakati ukiwa kwenye harakati.
 
Kwenye utafutaji kuna rough nyingi jitahidi upambane na kila fitna utayokutana nayo na ujue kwenye kutafuta vikwazo hautoviepuka ni kila siku vitakuja vikwazo vipya, hakikisha unasimama imara
 
Usikate au kukatishwa tamaa kwenye hustle zako, kumbuka kumuomba Mungu na uaminifu iwe nguzo yako kuu
 
Moja ya vitu ambavo nimejifunza na huenda binadamu wengine hawajui au wanapaswa wajue ni kuwa; daima mwenyezi Mungu hukupatia UNACHOSTAHILI na si UTAKACHO.

Pili; Mungu hakupi kitu ambacho mwisho wa siku utakuwa si msaada kwa wengine wenye uhitaji; bali akikubariki anataka ukawe baraka pia msaada kwa wengine.

Vinyongo; au kuweka vinyongo na visasi katika moyo daima tambua kabisa ni kujizuia baraka zako. Utaomba sana na mwisho kuona hujibiwi;

Mkuu; life is full so many challenges zingatia kusamehe; kusahau; usiweke vinyongo katika nafsi/roho yako; kumbuka pesa si kila katika maisha bali furaha na amani ya roho.

Let's all be Humble, when we die all materialistic things becomes useless for us.
 
Back
Top Bottom