Mambo ya kutisha na yenye kuumiza hisia tunayokutana nayo tukiwa maskini

Mambo ya kutisha na yenye kuumiza hisia tunayokutana nayo tukiwa maskini

Kudharauliwa, kuchekwa, kupewa maneno ya kejeli, kwa sababu ya kukosa kazi na umaskini ulionao, ingawaje anaekudharau ni maskini kama wewe..

Naapa kwa mbingu na ardhi siku nikija kufanikiwa sana kipesa, sitokuja saidia hata Mtu mmoja chini ya hili jua, nikitoa pesa ntakua nalenga faida ya mara 10 ya hela nliyotoa, nitajilimbikizia mabilioni ya shilingi kwa hasara ya wengine, hata kama jirani yangu atakufa njaa kwa kukosa elf 2.

Sitotoa hela na sitoona huruma, nitasaidia mke alienizalia watoto na watoto wangu tu, na sitotaka mazoea ya kijinga na watu wasio na faida na mm.

Nimegundua binadamu wengi ni wanafiki sana.


Umechelewa sana kulitambua hilo.

Ingia page yangu utapata masomo yangu ya namna ya kuwa bedui usiye na huruma
 
Moja ya vitu ambavo nimejifunza na huenda binadamu wengine hawajui au wanapaswa wajue ni kuwa; daima mwenyezi Mungu hukupatia UNACHOSTAHILI na si UTAKACHO.

Pili; Mungu hakupi kitu ambacho mwisho wa siku utakuwa si msaada kwa wengine wenye uhitaji; bali akikubariki anataka ukawe baraka pia msaada kwa wengine.

Vinyongo; au kuweka vinyongo na visasi katika moyo daima tambua kabisa ni kujizuia baraka zako. Utaomba sana na mwisho kuona hujibiwi;

Mkuu; life is full so many challenges zingatia kusamehe; kusahau; usiweke vinyongo katika nafsi/roho yako; kumbuka pesa si kila katika maisha bali furaha na amani ya roho.

Let's all be Humble, when we die all materialistic things becomes useless for us.


Mungu akikupa hakupangii matumizi.
Tumia kwa kadiri upendavyo, Mungu akikupa hakugeuzi mtumwa wako. Huyo sio Mungu.

Mungu akikupa amekupa, anakupa vile atakavyo.
Usaidie usisaidie utajua mwenyewe, Muhimu usimuasi.
 
Back
Top Bottom