Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
1. GOAL LA TSHABALALA
Goli la ufunguzi la Siphiwe Tshabalala alilolifunga dhidi ya Mexico kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango Oscar Perez. "Goal for Bafana Bafana, goal for all Africa, First goal in South Africa" (Goli kwa Bafana Bafana, Goli kwa Waafrika wote, Goli la kwanza ndani ya Afrika ya Kusini) ilikuwa ni sauti ya juu sana ya mtangazaji mahiri raia wa Uingereza Peter Drury iliyowafurahisha wengi wakati huo.
2. WAKAWAKA NA WAVIN FLAG
Nyimbo za Waka waka na Wavin Flag ziliimbwa na wasanii mashuhuri kwenye nchi zao Shakira na Knaan zilizopamba bara la Africa zilitumbuiza na kuvutia watu wengi.
3. SAVES ZA IKER CASILAS NA KIFO CHA SHABIKI
Saves mbili za hatari za Iker Casillas dhidi ya Arjen Robben mechi ya fainali (Netherlands Vs Spain). Saves hizo zilipelekea kupoteza maisha ya shabiki mmoja raia wa jamhuri ya Afrika kusini ambaye alibetia Netherlands kuchukua kombe. Kwa uwezo mkubwa wa Casillas, Robben hakuamini macho yake kwa maana hakuwahi kukosa kama vile kabla.
4. MAGOLI YA DIEGO FORLAN
Uwezo mkubwa wa mbinu na kuliona goli wa Diego Forlan aliyekuwa kiungo mshambuliaji hatari wa Uruguay uliomfanya apewe tuzo ya mchezaji bora akiisaidia Uruguay kutinga nusu fainali wakimaliza mshindi wa 4 nyuma ya Ujerumani.
5. TEKE LA DE JONG KWA ALONSO
Rafu ya hatari ya Nigel De Jong aliyomchezea Xabi Alonso kwa kumkita teke la kifua kwenye mechi ya fainali (Uholanzi na Hispania), huku cha kushangaza ni mwamuzi wa kiingereza Howard Webb akimuonesha kadi ya manjano.
6. GOAL LA ANDREAS INIESTA
Goli la ushindi la Andreas Iniesta (dk 116) Hispania wakitwaa ndoo mbele ya Uholanzi, goli lililomfanya rais wa Afrika Kusini wakati huo Jacob Zuma kunyanyuka na kushangilia huku watu wakilipuka kwa shangwe kwenye dimba la Soccer city jijini Johannesburg.
7. VUVUZELA
Staili ya kushangilia ya vuvuzela ambayo FIFA waliifungia kutumika kwenye michuano yake yote inayofuata kutokana na Robin Van Persie mechi dhidi ya Denmark kukwepa adhabu ya kadi nyekundu kwa kujitetea kuwa hakusikia filimbi alipoendelea kucheza mpira ilhali mwamuzi alishapuliza filimbi ya mpira wa kuotea.
8. TUZO YA DOGO MULLER
Thomas Muller (akiwa na miaka 20 wakati huo) alichukua kiatu cha dhahabu akilingana magoli na Wesley Sneijder, David Villa na Diego Forlan wote wakiwa na mabao matano, tuzo akapewa Muller kwa kuwa na pasi 3 za mabao huku waliobaki wakiwa na pasi moja moja.
9.UMAARUFU WA PWEZA PAUL
Utabiri wa pweza Paul aliyetabiri jezi ya orange itafika fainali
Ulikuwa wapi miaka 15 iliyopita? Tukio lipi lilikusisimua zaidi.