Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
- Thread starter
- #21
Aisee 2010 ulikuwa form four?Asamoah Gyan kukosa penalty ya mwishoni mwa muda wa nyongeza iliyokuwa iipeleke Afrika nusu fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.
Nilikuwa naishabikia Spain kipindi kile nikafurahi wao kuchukua kombe, ila baadaye nimekua kila nikirudia ile mechi natamani kulia kwanini Uholanzi walikosa lile kombe. Walikuwa bora katika kila kitu!
Spain walipoteza mechi ya kwanza, nakumbuka Pique aliumia kichwa wakati anapambania mpiga golini, na Uholanzi hawakuwahi kupoteza mechi ila ya mwisho pekee. Very sad!
Nilikuwa Form Four, na mimi ndiye nilikuwa mchambuzi wa kombe hilo kwa familia kila mechi bila mimi Mzee haangalii mpira kwa raha, ikabidi niwe naangalia naye mechi hadi usiku na bahati nzuri nilikuwa likizo.
Nilikuwa team Spain pia na hii ni kwa sababu nilikuwa naipenda sana Barcelona.
Nilipata uzi OG kabisa wa Spain