Mambo ya kuvutia na kushangaza kombe la dunia mwaka 2010

Mambo ya kuvutia na kushangaza kombe la dunia mwaka 2010

Asamoah Gyan kukosa penalty ya mwishoni mwa muda wa nyongeza iliyokuwa iipeleke Afrika nusu fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Nilikuwa naishabikia Spain kipindi kile nikafurahi wao kuchukua kombe, ila baadaye nimekua kila nikirudia ile mechi natamani kulia kwanini Uholanzi walikosa lile kombe. Walikuwa bora katika kila kitu!

Spain walipoteza mechi ya kwanza, nakumbuka Pique aliumia kichwa wakati anapambania mpiga golini, na Uholanzi hawakuwahi kupoteza mechi ila ya mwisho pekee. Very sad!

Nilikuwa Form Four, na mimi ndiye nilikuwa mchambuzi wa kombe hilo kwa familia kila mechi bila mimi Mzee haangalii mpira kwa raha, ikabidi niwe naangalia naye mechi hadi usiku na bahati nzuri nilikuwa likizo.
Kumbe we mzee,kibibi kabisa kwisha habari yako huna jambo.
 
1. GOAL LA TSHABALALA
Goli la ufunguzi la Siphiwe Tshabalala alilolifunga dhidi ya Mexico kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango Oscar Perez. "Goal for Bafana Bafana, goal for all Africa, First goal in South Africa" (Goli kwa Bafana Bafana, Goli kwa Waafrika wote, Goli la kwanza ndani ya Afrika ya Kusini) ilikuwa ni sauti ya juu sana ya mtangazaji mahiri raia wa Uingereza Peter Drury iliyowafurahisha wengi wakati huo.

2. WAKAWAKA NA WAVIN FLAG
Nyimbo za Waka waka na Wavin Flag ziliimbwa na wasanii mashuhuri kwenye nchi zao Shakira na Knaan zilizopamba bara la Africa zilitumbuiza na kuvutia watu wengi.

3. SAVES ZA IKER CASILAS NA KIFO CHA SHABIKI
Saves mbili za hatari za Iker Casillas dhidi ya Arjen Robben mechi ya fainali (Netherlands Vs Spain). Saves hizo zilipelekea kupoteza maisha ya shabiki mmoja raia wa jamhuri ya Afrika kusini ambaye alibetia Netherlands kuchukua kombe. Kwa uwezo mkubwa wa Casillas, Robben hakuamini macho yake kwa maana hakuwahi kukosa kama vile kabla.

4. MAGOLI YA DIEGO FORLAN
Uwezo mkubwa wa mbinu na kuliona goli wa Diego Forlan aliyekuwa kiungo mshambuliaji hatari wa Uruguay uliomfanya apewe tuzo ya mchezaji bora akiisaidia Uruguay kutinga nusu fainali wakimaliza mshindi wa 4 nyuma ya Ujerumani.

5. TEKE LA DE JONG KWA ALONSO
Rafu ya hatari ya Nigel De Jong aliyomchezea Xabi Alonso kwa kumkita teke la kifua kwenye mechi ya fainali (Uholanzi na Hispania), huku cha kushangaza ni mwamuzi wa kiingereza Howard Webb akimuonesha kadi ya manjano.

6. GOAL LA ANDREAS INIESTA
Goli la ushindi la Andreas Iniesta (dk 116) Hispania wakitwaa ndoo mbele ya Uholanzi, goli lililomfanya rais wa Afrika Kusini wakati huo Jacob Zuma kunyanyuka na kushangilia huku watu wakilipuka kwa shangwe kwenye dimba la Soccer city jijini Johannesburg.

7. VUVUZELA
Staili ya kushangilia ya vuvuzela ambayo FIFA waliifungia kutumika kwenye michuano yake yote inayofuata kutokana na Robin Van Persie mechi dhidi ya Denmark kukwepa adhabu ya kadi nyekundu kwa kujitetea kuwa hakusikia filimbi alipoendelea kucheza mpira ilhali mwamuzi alishapuliza filimbi ya mpira wa kuotea.

8. TUZO YA DOGO MULLER
Thomas Muller (akiwa na miaka 20 wakati huo) alichukua kiatu cha dhahabu akilingana magoli na Wesley Sneijder, David Villa na Diego Forlan wote wakiwa na mabao matano, tuzo akapewa Muller kwa kuwa na pasi 3 za mabao huku waliobaki wakiwa na pasi moja moja.

9.UMAARUFU WA PWEZA PAUL
Utabiri wa pweza Paul aliyetabiri jezi ya orange itafika fainali

Ulikuwa wapi miaka 15 iliyopita? Tukio lipi lilikusisimua zaidi.
Mkuu nilifumaniwa kwa dem na kaka zake baada ya kutoka kwenye mpira. Nakumbuka ilikuwa nusu fainal nadhani ilikuwa Spain na german.

Demu akaniambia leo njoo wote wanaenda mpirani hadi baba mzazi wao.Bahati mbaya generator ilizingua hivyo watu wakarudi kabla ya game kuisha


Baada ya mzee yule kunifahamu akaamulu nisipigwe ila nikojolewe mwili mzima na vijana wake wakafanya hivyo kisha kunipeleka hadi getoni kwangu nikalale na mkojo wao bila kuoga.
 
Dah wakati huo 98 nilikuwa nanyonya sijui chochote kuhusu dunia kweli binadamu tunatoka mbali sana.
The Cup of Life (La Copa De La Vida) ya ricky martin huenda ndio ngoma bora zaidi ya world cup na maarufu, huenda hata wewe umeisikia.
 
One of the best world cup! Suarez kudaka mpira, wimbo vibe la wimbo wa wakawaka, tangazo la cocacola, goli la ushindi la iniesta
😃😃Kweli JF ina kila rika kuna watu eti huo mwaka walikuwa standard 4 wakati wengine ndo Kwanza tulikuwa na mandevu ya kutosha
 
Asamoah Gyan kukosa penalty ya mwishoni mwa muda wa nyongeza iliyokuwa iipeleke Afrika nusu fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Nilikuwa naishabikia Spain kipindi kile nikafurahi wao kuchukua kombe, ila baadaye nimekua kila nikirudia ile mechi natamani kulia kwanini Uholanzi walikosa lile kombe. Walikuwa bora katika kila kitu!

Spain walipoteza mechi ya kwanza, nakumbuka Pique aliumia kichwa wakati anapambania mpiga golini, na Uholanzi hawakuwahi kupoteza mechi ila ya mwisho pekee. Very sad!

Nilikuwa Form Four, na mimi ndiye nilikuwa mchambuzi wa kombe hilo kwa familia kila mechi bila mimi Mzee haangalii mpira kwa raha, ikabidi niwe naangalia naye mechi hadi usiku na bahati nzuri nilikuwa likizo.
Laana ya asili ya waafrica ilimkosesha Asamoah penaty

Robben alizingua sana kukosa magoli ila refa pia Howard web aliharibu mechi
 
Back
Top Bottom