Mambo ya kuzingatia kwa wanunuaji wa used fridge

Mambo ya kuzingatia kwa wanunuaji wa used fridge

Lumbi9

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
8,666
Reaction score
12,178
Habari,

Kama inavyofahamika baadhi yetu hatujaweza kumudu gharama za kununua fridge mpya, na mahitaji ya chombo hiko tunayo hivyo tunalazimika kupitia maeneo ambayo tunaweza tukapata kwa bei tunayoimudu na mara zote inakuwa ni used.

Kama mjuavyo vitu hv vina changamoto sana hasa kwa sie tusiokuwa na abc za kutosha kuhusiana na ilo, hivyo kwa wenzetu wenye ufahamu zaid huko watujuze kipi hasa cha kuzingatia ktk manunuzi, changamoto na mengine mengi naamini tutasaidika wengi.

Karibuni.
 
So kikubwa ni compressor inafanya kazi
 
Kwenye kompresa nini cha kuangalia ili kuijuwa kama iko vizuri?
Iwe inatoa baridi kwa maana ya coolling ili uijue kama iko vizuri zaidi mwambie muuzaji akuwashie griji kisha subiri dkk kumi lizime kisha baada ya dkk tano liwashe na usubiri kuangalia kama litaweka baridi ndani lisipofanya ivyo huo utakuwa ni mkeka achana nao utakuchanikia ndani
 
Kinacho matter ni compressor tu liwe linafanya kazi kwa maana ya kugandisha ama kutoa mabarafu
 
fuata ushauri wa ankai, cha kuongezea tu

raisi aghali: kuna vitu vya kununua kama 'used' sio friji! hujui iyo 'kompresa' ina 'age' gani, imezeeka kiasi gani, iandalie units 3 za umeme kwa siku kama ni friji izi za 50Watts
 
Apana iyo haijalishi mkuu frost na defrost izo mifumo tu ya utengenezaj ni sawa na manual an auto ivyo iyo haimat kabisa
Kuangalia na brand je?
Binafsi nilienda dukani nikachukua SHARP na kuacha BOSS.
So far ipo good.
 
fuata ushauri wa ankai, cha kuongezea tu

raisi aghali: kuna vitu vya kununua kama 'used' sio friji! hujui iyo 'kompresa' ina 'age' gani, imezeeka kiasi gani, iandalie units 3 za umeme kwa siku kama ni friji izi za 50Watts
Johnhance umemaliza kila kitu.

Fridge used nyingi ni za kizamani na zinakula umeme balaa. Kama unakaa nyumba ya kupanga utagombana na wapangaji wenzako siku zote au hata kama una biashara itabidi faida mgawane nusu kwa nusu na Tanesco.

Lingine ni warrant au guarantee. Utatest fridge mwanzo mpaka mwisho, ila siku mbili tatu likianza kuwa bovu, gharama yake ni bora ungesubiri ununue fridge mpya.
 
Kuna vitu vya kununua used ila fridge sikushauri,sisemi usinunue nunua kama anayekuuzia ni mtu mnaeheshimiana sana maana risks za kuikuta tofauti na matarajio yako ni nyingi mno.

Brother angu mwaka flani alifanya hiko kitendo,alijuta maana inafika home wiki tu ikazingua peleka kwa mpemba mpemba kamwambia iache ipitie jioni akaifikisha tena kwake siku ya nne imekataa tena akaipeleka tena ikirudi yale yale yaani ikifanya kazi muda mrefu ni wiki 3......

Alikaa akapiga hesabu zile route za kuitoa K/koo mtaa wa Uhuru hadi kwake Kibamba na kirikuu changanya na muda aliopoteza na vifaa alivyonunulishwa akakuta kumbe angeongeza 85,000/= tu angepata fridge mpya yenye ukubwa sawa na ile ile na siku iliposumbua tena akaibeba kuipeleka akaambiwa anunue compressor aliiacha huko huko akajichanga akanunua mpya dukani.

Wakati wa kununua hakikisha contract unayoingia na muuzaji inam'bana yeye maana wana kawaida ukiishawapa hela ukabeba zigo nakuambia hata ukija kesho yake asubuhi na mapema ukawaambia ina tatizo basi wataongea na wewe as if umekuja kuwaomba ushauri,yaani hawakujali kabisa!
 
Kuangalia na brand je?
Binafsi nilienda dukani nikachukua SHARP na kuacha BOSS.
So far ipo good.
Mkuu trst me kwenye friji kinachomatter ni compressor haya mambo ya brand sijui samsung sijui boss sijui sharp hayana maana zaidi ya ufahari tu kwa washkaji na majirani wanaokuzunguka na kuja geto kwako lakini kinachomatter kwenye friji lolote lile ata iwe brand gani ni uhai wa compressor ni uzima wa compressor ni ukamilifu wa compressor

Je utaujuaje utimamu wa compressor ya friji unalotaka kulinunua fata au fanya huo mchakato nilio usema apo juu kwenye comment yangu ya mwanzo natumai nimeeleweka compressor ndo kila kitu kwenye friji izo brand ni ufahari kwa majirani zako na ndugu zako isu compressor iwe timamu
 
fuata ushauri wa ankai, cha kuongezea tu

raisi aghali: kuna vitu vya kununua kama 'used' sio friji! hujui iyo 'kompresa' ina 'age' gani, imezeeka kiasi gani, iandalie units 3 za umeme kwa siku kama ni friji izi za 50Watts
Kinachoharibika kwenye "Compressor" ni "Relay" dumu la compressor kama halijatoboka linaweza kukaa hata miaka mia moja 100yrs,kwahiyo hamna kuzeeka kwenye compressor.Relay ni kitu kiko juu ya compressor ambacho unaweza kukitoa na kukibadilisha,ubora wa Relay inatokanana nchi gani imetengenezwa..

Comressor bora kuliko zote ni Danfos..
 
Kwako wewe haijalishi. Ila tunaojua Quality tunajali.
Mkuu sijajua unaongelea quality gani mimi si muuza mafriji tafadhali sana nafanya kazi nyingine lkn nina uzoefu na iyo kazi pia nishawahi kuifanya na naijua vizuri sana nje ndani ivyo.

Unapoongelea frost na no frost fridge iyo ni mifumo imetengenezwa kutokana na matakwa ya watu kwamba kuna watu wanapenda mafridge ya kugandisha mabarufu kwa ndani (frost fridge) na ndo wanaona kuwa linafanya kazi pia kuna wanaopenda (nofrost fridge) lisilo gandisha mabarafu kwa ndani ila vitu vikiwekwa vinaganda.

Ivyo iyo ni mifumo tu kama manual na automatic lkni cha msingi ni engine ambayo ni compressor
 
Hakikisha ni Frost Free...haligandi mabarafu kwenye kuta, kutoa chakula mpaka upasue barafu
Frost free uswahilini wapi na wapi mkuu sisi huku likitengeneza mabarafu ndio linafanya kazi sana,hiyo tabia ya kugonga freezer kupata barafu ni kawaida sana na kama zile line za gas zikitoboka tunafanya winding na zile copper tubes ! [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Back
Top Bottom