Mambo ya kuzingatia ukiwa katika nchi za bara la Asia, Ulaya na Marekani

*Bado tupo South Korea tukitoka South tunaenda North kwa Kiduku

Ukiwa South Korea Usitarajie Wakorea kuzungumza nawe. Watakukwepa na Wala usihisi kubaguliwa, Wengi wao ni wenye haya na wanajaribu kuwaepuka wageni ili kuepuka aibu ya kuongea Kingereza kibovu

*Katika mazungumzo Wanawake hufunika midomo yao wakati wa kucheka.

Hapo awali, wasichana walifundishwa kwamba kucheka sio tabia ya kike. Na ikitokea kitu kitakacho wafanya wacheke, basi watacheka huku wakitazama kando au kujaribu kuficha tabasamu zao (kwasasa, wanafunika midomo). Ukiona mwanamke wa Kikorea amefunika mdomo wake, usije kudhani anapiga miayo Bali anacheka
 
Umenifanya nicheke sana eti polisi mwenye kanzu teh teh... teh [emoji23]
 
Safi, Kuna mengine hata mm nilikuwa siyajua hapa. Itabidi nijitahidi nifike nchi za kiarabu
 
msaada wa nchi za ukanda wa Scandinavia counties…utaratubu wa maisha upo upoje (lifestyle) na kipi na kipi kinatakiwa na kipi hakitakiwi, natanguliza shukrani ..
 
Kuna yule inshomile alitaka kuleta ujuaji wa mambo ya kuwaiga black america yakamkuta. Don't mess up with american police be cooperative.
Kuna mtza simu ilimponza alisimamishwa na police mara simu ikaita mfukoni alifanya kosa kubwa Sana kuingiza mkono mfukoni Ili achukue simu apokee ikawa ndo mwisho wa maisha yake palepale askari walidhani anatoa bastola, hadi uchunguzi upite ijulikane ni simu ushapotea. Police wa USA au Ulaya ukiwapa ushirikiano unajiongezea maksi ni rahisi kukusikiliza.
 
Nchi yeyeto ukienda achana na mambo ya feki, shortcut, illegal hasa ukiwa mgeni. Kuishi vyema fanya KILA kitu halali, ubaguzi wao usikuathiri, wabaguzi wengi ni watu wasio na exposure, kuwa Mzungu hakumaanishi mtu ana exposure, wapo wazungu wengi tu primitives, hawana exposure washamba awajatembea. Ukifanyiwa dhihaka yeyeto usionyeshe hisia ya kuchukia wataendelea kukuumiza Ili wafurahi, wakiinuka kwenye siti lala kabisa siti zote kwa raha zako hadi mwisho wa safari au kuwa bize na simu
 
Yapi ya kuzingatia ukiwa Uingereza?

Nikisikia story kama hizi ndio naona bora kufia hapahapa kwa Nyerere.
 
Yapi ya kuzingatia ukiwa Uingereza?

Nikisikia story kama hizi ndio naona bora kufia hapahapa kwa Nyerere.
Story nyingi ni over exaggerated, jambo muhimu kwa watu wa nchi yoyote ni 'mean your own business' hutapata mshikira wowote.
 
Story nyingi ni over exaggerated, jambo muhimu kwa watu wa nchi yoyote ni 'mean your own business' hutapata mshikira wowote.
Haziko over exaggerated ndugu, Acha nikuambie kitu kimoja unachoshindwa kuelewa, Sheria zote unazozisikia kwenye hayo ma nchi baadhi huvunjwa kila wakati na wenyeji, ila ukivunja wewe mgeni ndio utajua kama ni over exaggerated au sio, Yani watakufanya kama wewe ndiye mtu pekee kuvunja hizo Sheria, kwa hivyo ni bora kuwa mpole
 
Kwanini unasema tusivae nguo za kitaliano ? Na hizo nguo zipoje ?
 
Asante kwa elimu.
Wenzetu mliopanda mwewe leten elimu
 
This is free education. Asante mkuu.
Ahsante sana! Ni material haswaa.
Nasikia pia japan mkiwa kwenye usafiri wa umma na jirani yako akasinzia na kukuegemea huruhusiwi kumsukuma (kumuamsha); ni ishara kuwa amefanya kazi vya kutosha katika kujenga taifa lao.....hii imekaaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…