Mambo ya kuzingatia unaponunua tairi za gari


Land Rover gani? maana mimi nina 109 sijaona hiyo kitu hahahhaa
 

Mkuu hapa mimi nina mashaka na hilo nililopigia msitali. kama tutakubaliana na hili nadhani kutakuwa na tatizo kubwa sana hasa kwenye Science namna inavyotumika. Labda nikuulize Je unaweza kutumia kigezo cha tairi ndogo kwenye kesi ya ku-overspeed? si kila gari ina speedometer yake? kufuatana na size ya tairi. nimelisikia kwa watu wengi lakini mimi nalipinga kwani naamini speed ile ile bila kujari ukubwa wa gari au tairi.
 

hili swali akina Chacha Kisiri, Goodrich na Tcleverly walishalijibu kwenye post za nyuma kwa kifupi ni kwamba hiyo speed utaipata ila engine itakuwa na mzunguko mkubwa bila sababu na hivyo kukugharimu mafuta na vitu vingine pasipo sababu ya msingi
 
Mi nilivyoelewa ni kuwa kubwa au dogo compared to the specifications za gari husika
 
Umeyaelewa hayo maelezo au ume copy na ku paste ?
Nashauri usome upya maelezo hayo na kupata logic behind, reason between and conclusion within !

nimeyaelewa na nime-experience hio kitu,i had a front wheel drive car na wakasisitiza hawaweki matairi mapya mbele iwapo nitabadili mawili tu watayaweka nyuma.....wether ur car is front or rear wheel new tires should go on the rear axle and partly worn on the front axle if ur changing one pair....although if the car is front drive,front tires will wear out quicker than the rea and vice versa
 

Mkuu TCleverly,
Nikukumbushe tu kwamba ukiona matari ya mbele ya gari yako yameisha kuliko ya nyuma ujue kuna uzembe ulioufanya initially. Kimsingi hali hiyo inaelezea kuwa matairi hayo ya mbele yalikaa muda mrefu yakiwa mbele na hivyo yakaisha haraka (Assuming kulikuwa hakuna makosa kwenye kujaza na kupima upepo mara kwa mara). Technically other things remain constant, matairi yote yanatakiwa yaishe kwa pamoja. Unless hukuwa unafanya tire rotation ambalo ni kosa kubwa.

Turudi kwenye ishu yako. Hao watu waliokwambia hawaweki matairi mapya mbele wakati gari yako ni front wheel car ulipaswa uwaulize sababu ya kitalaamu ya kutofanya hivyo then utuambie ili tuendelee na mjadala.
 
Last edited by a moderator:


unaonyesha hujasoma post yangu yote....sababu zao za kitaalamu nimeweka
kuhusu rotation kwa kweli sifanyi kabisa kwahio sishangai ya mbele yakiwahi kuisha
 

Ameelezea kwenye post zake zilizotangulia.
 
Last edited by a moderator:
Tafadhali naomba kujulishwa kwenye cresta gx100 naweza kufunga tyre yenye kubwa mpaka size gani,bila modification YEYOTE.
 
Tafadhali naomba kujulishwa kwenye cresta gx100 naweza kufunga tyre yenye kubwa mpaka size gani,bila modification YEYOTE.

funga size 16 na kama unahitaji zipo sehemu rim sports panga 5 ila zote pamoja pamoja tairi lake ni mi 3.5 yani ww ukija unafunga na kuondoka
 
Ok kama rim size 16 Je, naweza weka mpira wenye specification hii 225/55/r 16????? Nauliza hivyo kwasababu niliona mpira wa size hiyo umefungwa kwenye chaser gx100 na gari imependeza sana, lakini nilivyoenda dukani kununua mipira size kama hiyo ili nifunge kwenye cresta Gx100 nikaambiwa haitofaa ni mikubwa labda gari ifanye kuamshwa kwa kuweka spensa, sasa Je mipira unayosema wewe ni ya specification gan? Na unatumia kigezo gan kujua size ya mpira unayoweza kufunga kwenye gari lako ambayo haitoleta shida bila kufanya modification yoyote kwenye gari????
 
Kwa kweli tumefaidika sana na maelezo haya msione wengine tumekaa kimya... Tunajifunza!! Wengine wetu tumegundua makosa mengi ambayo tumekuwa tunafanya kwenye magari yetu!

Bila shaka kuna watu hapa wamekaa kimya lakini sasa wanakwenda kufanya tyre rotation kesho!!
 
KUNA SWALI MOJA

JE KWA BONGO NI TAIRI AINA GANI NZURI KWA MAGARI YA KUTEMBELEA KAMA RAV 4 au SUZUKI

Ziko aina nyingi dukani na kila muuzaji anavutia kwake.
 
Tairi yangu inasomeka hivi 215/65 R16. Je ni aina gani ya tairi ni durable na ni kama bei gani?
 
Mkuu,
tatizo kutaja majina inakuwa ni biashara.
Lakini tyre just depend on your choice

Ndiyo mkuu lakini bei zinatofautiana sana kiasi ya kutuchanganya wengine. Unaweza kukuta aina moja wanauza 170,000/= aina nyingine wanauza 450,000 Tzs nk, nk. Pia tunasikia kuna nyingine ni feki. Ndiyo maana tunaulizia hapa Mkuu
 
Je tyre ya size 225/55R16 naweza kufunga kwenye CRESTA gx100 bila kufanya modification yoyote kama vile kuliamsha gari???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…