Chacha Kisiri
Senior Member
- Nov 1, 2008
- 156
- 161
Ushauri wako mzur but Kuchek upepo kila baada ya wiki its too much unless ubora wa tire zako uwe hafifu mno i suggest may b monthly. Also rotation inategemea KM ulizotembea wataalam washauri ni KM ngapi ufanye rotation.
Mkuu, swala la how long kupima upepo na kufanya rotation za tairi are judgement issues and depend on circumstances. Mfano kama gari unalolitumia kila siku kwenda kazini na kurudi nalo nyumbani then unafanya mizunguko mingine ya kawaida, its most preferably kuwa unapima upepo kila wiki. Hii inatokana na tabia ya tubeless tire kuwa zinajiongeza upepo na saa nyingine zinajipunguza zinapokuwa barabarani. Mfani Mimi huwa napima kila wiki na mara nyingi naweka 38 PSI tairi za nyuma na 35 PSI tairi za mbele. Sasa huwa nikienda kupima tena in the following week naweza kuta tairi moja ya nyuma ina 42 PSI na nyingine 40 PSI. Za mbele nazo naweza kuta moja imeshuka to 30 PSI na nyingine may be imejiongeza to 37 PSI.
Sasa kama nikisema niwe napima kila mwezi maana yake by the time naenda kupima naweza kuta tairi moja ya nyuma ina 50 PSI na nyingine may be 43 PSI. Za mbele hivyo may be moja inaweza kuwa 38 PSI na nyingine 33 PSI (It depends). Maana yake ni nini? Maana yake kwamba nitakuwa natembea na gari kwa muda mrefu bila ya kuwa proper tire pressure. Hii inaweza ikapelekea baadhi ya tairi kuisha mapema kuliko zingine, gari kukosa balance kwa kuwa itakuwa imelala upande wenye upepo mdogo na hivyo kuumiza suspension system za upande mmoja zaidi. Kibaya zaidi baadhi ya tairi zilizojaa kupita kiasi zinaweza kupasuka na kupelekea kupata hasara zaidi.
Kwa hiyo kutokana na madhara yanayoweza tokea kwa kukaa muda mrefu bila kupima upepo na kwa kuwa kupima upepo ni gharama ndogo sana inashauriwa kwa gari linalotumika kila siku for domestic routes basi ni vyema ulipime upepo kila wiki. Kwa upande mwingine, kwa gari ambalo hulitumii kila siku, mfano gari unaliendesha mara moja kwa wiki then unalipaki, kupima upepo baada ya mwezi mmoja si vibaya.
Aidha, kwa gari ambayo inaenda safari ndefu mfano unatoka Dar kwenda Mwanza (KM 1200)unashauriwa upime upepo angalau mara moja unapokuwa umefika katikati ya safari kuepuka tairi kukupasukia njiani. So kwa mazingira ya safari ndefu huna sababu ya kupima baada ya wiki. Ndiyo maana hata mabasi ya safari ndefu ambayo yanapataga ajali za kupasuka matairi saa nyingine unakuta tairi ni mpya kabisa may be imenunuliwa last week na nembo zake inaonyesha ita-expire three years to come lakini inapasuka within a week! Kwa nini? Ni kwa sababu ya uzembe wa kutopima upepo mara kwa mara. Matokeo yake tairi inajijaza upepo na kupitiliza kiwanga cha juu na matokeo yake ni kupasuka kwa tairi na maafa kwa abiria na mali zao.
Kuhusu tire rotation
Kama ilivyo kupima upepo, tire rotation is also a judgment issue and depend on the circumstances. Kwa gari ambazo ni for domestic purposes. Ni vyema ufanye rotation kila unapofanya service (Yaani either after KM 3000 or after Six month - whichever is earlier). Kwa nini? Tairi za mbele zinapokaa kwa muda mrefu bila kufanyiwa rotation zinatabia ya kuisha kwanza kutokana na kuwa involved sana na friction during cornering na pia kutokana na kwamba zinabeba uzito wa engine na hazijazwi upepo mwingi kuliko za nyuma. So ni vyema na zenyewe zikapata unafuu within a short period kukaa nyuma na zile za nyuma ziende mbele ili zote ziishe kwa pamoja.
Kwa upande wa gari ambayo inatembelewa may be kwa wiki mara moja tena kwa route fupi fupi then unai-park. Kufanya rotation even after six month sio vibaya.