Umenikumbusha one time kuna huyu binti kwenye basi la mkoa alileta huu uswahili. Amepanda kwenye basi amevaa jeans, sweater, na kablouse. Basi hana hata pochi yaani yupo kisela sana.
Kilichotokea ni period ilimuanza ghafla bila kujua. Kilichofanya nijue ni alivua sweater lake na kulitumia kama kujifunika sasa mimi nilikuwa na sweater na zile shuka za kimasai. Nikamuuliza mbona umevua sweeter na gari wamewasha AC haikutesi?!
Akajibu kama vile mtu mwenye mawazo na aibu fulani. Ilinichukua dakika chache kunotice kuwa hakuwa sawa na nikashajua huyu ametumia sweater kujificha. Nikamwambia kwa sauti ya chini sana unahitaji msaada. Hakunijibu zaidi ya kuinama kama anaona aibu halafu anaweka lile tabasamu la aibu fulani.
Nikamwambia niandikie kwenye sms unataka msaada gani. Nikampa simu yangu aandike namba yake nikamtext akaanza kuchat akanambia ameingia Period hapo hana uhakika na kinachoendelea ila anahisi amechafua siti sasa hajui pa kuanzia.
Aiseee ni MUNGU tu alisimamia ile situation maana gari lilikuwa na utingo mwanaume tu. So ikabidi nimfuate nimpange kuwa atusaidie wakiona hata kituo cha mafuta wasimame konda akanielewa. Tukasimama akasema abiria tuchimbe dawa kidogo. Watu wakaanza shuka. Akachukua sweta akaliweka pale kwenye siti halafu nikampa shuka langu la kimasai akajifunika mwili mzima so muda tunatoka nashuka nae hakuna mtu alishtukia chochote hadi tunafika chini. Nikamwambia atangulie chini me nakwenda tafuta pedi. Nikaenda mnunulia duka liko huko barabarani kipande kidogo toka pale kwenye sheri nikamletea.
Akajiweka sawa suruali yake ilikuwa imechafuka akaisuuza na maji akavaa hivyo hivyo nikamwambia valia na hilo shuka la kimasai. Tukarejea kwenye gari. Aisee ikawa kama ni mke wangu sasa namna tulivyorudi na kukaa kwenye gari alijiegemesha kwenye kioo me namwambia niegemee kama unataka kulala.
Tulishuka sote stand ya Moshi alikuwa anataka kwenda nikamwambia sidhani kama utakuwa katika hali nzuri kuendelea na safari katika hali hiyo na muda umekwenda twende nyumbani sio mbali na hapa ukaweke mambo sawa uwe safi kesho utaendelea na safari ndugu zako waelezee situation wakitaka watumie picha kabisa halafu tukimbie na huu msala wa kuchafua siti.
Akakubali. Tulishuka sote akafika nyumbani akatoa nguo zote akazifua na kuzianika. Ilibidi nimnunulie kufuri mpya na pedi zingine za brand nzuri.
Nilimpa risala sana ule usiku. Kwamba kwann mtoto wa kike unasafiri kirahisi vile huoni namna umejihatarisha. Yaani unasafiri haubebi kitenge hata viwili na hata pedi tatu za dharula maana hata usipopata wewe anaweza pata mwanamke mwenzako ukamsitiri. Nikamwambia sasa usingekutana na mimi leo si ungefedheheka sana.
Kesho yake nikamsindikiza jioni aende kwa kwao huko Arusha. Na baada ya hapo tuliendelea kuwasiliana she is someone very close to me now.
Kunakitu hata siwaelewi wasichana/Wanawake?
Hivi unasafiri safari ya zaidi ya masaa matatu, kwa nini usivae pedi kabisa kwani inakupunguzia nini? Naona mambo mengine ni kujidhalilisha tu kwa kukosa maarifa